Tetesi: Hiki kinachofanyika hapa kwenye ligi kuu ya bongo ni dhahiri Yanga atakua bingwa kila msimu!

Mimi ni mwanachama halali wa coastal union moja ya wadhamini wetu ni GSM pia tunachangia ubingwa wa yanga kila msimu point 6!
Ingekuwa Coastal Union vs Yanga ni mechi nyepesi basi tungeona hilo uwanjani ila Yanga hupata tabu sana akicheza dhidi ya Coastal union na kama unakumbukumbu vizuri, mechi yao ya mwisho Yanga walishinda dakika za mwishoni kabisa goli moja tena kwa sub ya Mudathir na Moloko.

Ila Simba kumpiga Coast goli 4+ ni swala la kawaida walishafungwa goli 7 na Simba. Na Coastal haikuwa kuifunga Simba ila Yanga imeshawahi kufungwa na Coastal union.
Na la mwisho ni kwamba Karia ni kiongozi wa Coastal union na pia ni mshabiki na mwanachama wa Simba.
 
Mbumbumbu akili zenu ziko makalioni Yani kiufupi amjitambui mpo mpo tu Kama manyumbu, unaposema singida anaitengenezea yanga point za bure kwani kabla ajakutana na yanga kashinda mechi ngapi alipocheza na timu nyingine wanazolingana ubora? Yani apigwe na timu wanazolingana ubora alafu kwa yanga ambayo Iko juu kuzidi timu zote izo ifungwe na singida???? Uko sawa sawa kweli wewe kichwani ama Kuna fyuzi imeachia?
Mpira auchezwi chumbani ubora wa yanga ndio unaowapa matokeo ndio maana ata Simba alitandikwa goli 5 Ina maana na nyie mlinunuliwa pamoja na mhindi wenu!!!
 
Nani amekudanganya karia ni mwanachama wa simba!
 
Kama timu yako ni imara kwa nini haishindi? Mnakalia porojo badala ya kutengeneza timu. Msimu huu mtashika nafasi ya tatu labda ndiyo mtapata akili.
 
Kuna timu nyingine inakwenda kununuliwa muda wowote mtakua na uhakika mwingine muda si mrefu na mpira wenu wa kibongo bongo maendeleo hakuna timu ya taifa kifafa vilabu dege dege kwa mambo yenu ya rushwa mnalazimisha refa awape magoli yasiyostahili!
 
Games fixing ni kubwa sana ligi ya Tanzania. Matokeo halisi ni timu zikitoka nje
 
Kama timu yako ni imara kwa nini haishindi? Mnakalia porojo badala ya kutengeneza timu. Msimu huu mtashika nafasi ya tatu labda ndiyo mtapata akili.
Tupo nafasi ya nne tulimpiga mashujaa 2-1 lake tanganyika juzi!
 
Siyp powa kabisa aisee! Novemba 2023 tajiri alipenyeza pesa kwa kolon hivi hadi wakala 5. Yanga na matajiri wake wanaharibu ligi sana.
Tajiri huyu huyu akapenyeza pesa kwa amamelodi hadi kidogo watolewe isingekuwa janjajanja ya kulinunua goli halali.
 
crystal palace amempiga liverpool,Aston villa amempiga Arsenal mpira unachezwa hivyo sio timu sita zote za mtu mmoja mnafukuza mwizi kumbe wale walio mbele karibu yao ni wenzie wanamsadia mwendo hatari sana kwa hii janja janja!
Saa zingine ujaribu kufikiria kiunamichezo ukiacha huo usimba uliokuwa nao.
Kama Yanga ingekuwa inashinda kwa ujanja ujanja basi isingeweza kufuzu robo fainali mbele ya timu kubwa mbili zilizomzidi kwa rank na jeuri ya pesa na timu zinazotokea kwenye mataifa makubwa kimpira ( Al Ahly na Belouizdad)
Lakini Belouizdad atakufa goli 4 ndio wakina Singida watafanya nini?
Kama Simba imekula goli 5 ndio wakna Singida watamuweza Yanga?
Kama Al Ahly ametoshana nguvu na Yanga, na kule Misri wameruhusu goli moja pekee huku timu yako ikipigwa ndani nje, ndio utegemee wakina Singida wataiweza Yanga?
Kama nyie kwenye droo mlifurahia kumkwepa Mamelodi ambaye alikuwa anaohopewa na kila timu wasipangiwe nao na mwisho wa siku Yanga wakapangiwa nao lakini Mamelodi hakufua dafu kwa Yanga ndani ya dakika 180 ndio utegemee wakina Singida wataiweza Yanga?

Kaa kufikia hivyo vitu halafu ujione ulivyokuwa unaongozwa na mihemko ya kishabiki.
 
Siyp powa kabisa aisee! Novemba 2023 tajiri alipenyeza pesa kwa kolon hivi hadi wakala 5. Yanga na matajiri wake wanaharibu ligi sana.
Tajiri huyu huyu akapenyeza pesa kwa amamelodi hadi kidogo watolewe isingekuwa janjajanja ya kulinunua goli halali.
Mngeshinda kwa penati au walipiga peke yao!
 
Mpango WA wazi kabisa

Kwanini waliukimbia uwanja wao WA singida kwenda mwanza
 
Nazungumzia mjumbe wa baraza la wadhamini la klabu ya yanga ndie mmiliki wa klabu mbili za singida je kuna fair hapo hapo mdhamini wa hizo klabu ndie mdhamini mkuu wa yanga!
 
Kwa wanao ijua vizuri yanga kauli mbiu yao ni daima mbele nyuma mwiko bishana mpaka ufe!
 
Nazungumzia mjumbe wa baraza la wadhamini la klabu ya yanga ndie mmiliki wa klabu mbili za singida je kuna fair hapo hapo mdhamini wa hizo klabu ndie mdhamini mkuu wa yanga!
Weka ushahidi hapa, Simba tunajuwa mmiliki wake ni Mo Dewji, Lete ushahidi wa Mwigulu kuwa ndio mmiliki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…