Hiki ndicho kinachotuponza sisi Yanga. Tuambiane ukweli tu

Hiki ndicho kinachotuponza sisi Yanga. Tuambiane ukweli tu

Kwa hiyo timu ikiingia kwenye mfumo isipigwe tano? Ulikuwepo wakati wanaomba kulegezewa? Unataka kusema hizo timu haziwezi kufungwa na Yanga?

Yanga ina kikosi kizuri sana na bado itaendelea kuimarika.
Kikosi kizuri ungeishia Makundi?
 
Shida ni huyo Hersi amejificha kwny sura ya upole kumbe ni mpuuzi...mpenda sifa...
 
Mihemko katika ubora wao!!, kwahiyo unataka kuaminisha WATU na ww ni miongoni bumbu aliosema Rage?
 
Watu wanaongelea msimu huu wewe unaleta habari za kale, kwani kikosi cha sasa ndio kile kile kilichofika fainali cafcc, na kama mlikuwa na kikosi bora mlishindwa vipi kuchukua kombe lile
Yanga kama ni mbovu hiyo trh 8 mlikimbia nini?, Unaweza kumkimbia mnunua mechi?.
 
Mnapenda sana kujitoa ufahamu sasa ambacho hujamuelewa mtoa mada ni nini hicho kikosi huo uzuri wake mnashindwa vipi kuuonesha huko kimataifa mnaishia kuuonesha kwa kina kengold tu, mfano cafcl katika makundi yote kundi lenu ndilo lilikuwa jepesi na hata wenyewe mlishangilia mlivyopangwa nao ila cha ajabu mkashindwa kuvuka sasa huo ubora uko wapi, anyway mimi naona endeleeni kujiona mna kikosi kizuri msikiboreshe wala msiache kufanya match fixing ili kimataifa muendelee kuishia hatua za awali sisi ndio furaha yetu
Nyie kama mko bora mbona mlikimbia uwanjani?
 
kununua mechi mmeanza kitambo ila athari zake zinaonekana msimu huu na inayokuja, mtanyooshwa mpaka mmpate mchawi
Upuuzi wa wapuuzi kutoka mwamposa fc?, Yaani simba usisemwe kununua mechi kwa coast kuwazawadia gori 8 huku Saido anafunga gori 5!!
 
Kocha aliposema ligi yetu ni dhaifu alikuwa anaona matches ambazo tunacheza na teams zinavyolegea na kufanya makosa ya kipuuzi.

Lengo letu ni kuwapiga watu mkono na makono wakati mwingine. Lakini ilikuwa haisaidii team. Tunaona mikia jinsi wanavyokaziwa ndani ya ligi. Inawasaidia hata mashindano ya kimataifa. Mkazo huo ni faida kwao.

Sisi tunapowaambia watulegezee hatujifunzi kukaziwa. Matokeo yake matches ambazo hawatujui tunaumia sana na kuona hatujazoea. Mi nashauri viongozi waikomaze team. Tuache kuwaambia wapinzani walegee tuwafunge nyingi. Ni aibu kwetu.
CYo kuikomaza team tu ila kwenye team yetu kuna baadhi ya wachezaji hawana ubora wa kucheza yanga kwa mfano beki za pembeni
 
Mnapenda sana kujitoa ufahamu sasa ambacho hujamuelewa mtoa mada ni nini hicho kikosi huo uzuri wake mnashindwa vipi kuuonesha huko kimataifa mnaishia kuuonesha kwa kina kengold tu, mfano cafcl katika makundi yote kundi lenu ndilo lilikuwa jepesi na hata wenyewe mlishangilia mlivyopangwa nao ila cha ajabu mkashindwa kuvuka sasa huo ubora uko wapi, anyway mimi naona endeleeni kujiona mna kikosi kizuri msikiboreshe wala msiache kufanya match fixing ili kimataifa muendelee kuishia hatua za awali sisi ndio furaha yetu
Wewe ndio unajitoa ufahamu na kutupangia maisha namna ya kuyaendesha.

Sentensi ya mwisho nimeandika Yanga ni bora sana na itaendelea kuimarika wewe unakuja na maneno msiboreshe kikosi. Timu inaimarikaje bila kuboresha kikosi?

Unazungumzia kimataifa gani ambayo Yanga imeshindwa kuonyesha uwezo wake? Hapa ndio inaonyesha unajitoa ufahamu. Yanga ilitotolewa club bingwa ikaenda shirikisho na kwenda fainali moja kwa moja. Timu ya kwanza toka Tanzania kufika fainali za shirikisho ni Yanga. Unataka uone nini hadi uamini ni timu bora? Kuna match fixing yoyote ilihusika kufika fainali?

Msimu huu Yanga alikuwa anashiriki mashindano ya club bingwa ya Afrika. Unaelewa maana yake? Haya mashindano hachukuliwi mshindi wa tatu au wa nne kwenye ligi ni mabingwa na runners up tu. Simba haikupata nafasi hiyo ikadondekea shirikisho kwa shingo upande. Eti leo mnajivunia mashindano ambayo alipokuwa akishiriki Yanga mliyabeza. Hivi ni vituko.

Ukweli ni kuwa mngeshindwa kuwatoa hao waafrika kusini mnengeabisha nchi na kuishusha thamani ligi yetu. Jambo zuri mmeshinda heko kwenu ila muache kudharau mashindano fulani halafu mkiwa huko mnayageuza kuwa champions league.

Ushauri wa mpinzani siku zote ni kituko hatuwezi kuuchukua hausaidii chochote kwetu.
 
Yanga kama ni mbovu hiyo trh 8 mlikimbia nini?, Unaweza kumkimbia mnunua mechi?.
Tatizo mkiambiwa ukweli mnabisha, kwa taarifa yenu simba waligomea ile mechi sababu walikuwa na wasiwasi wachezaji wa yanga wanaweza kukamia mechi, wakawaumiza baadhi ya wachezaji wa simba maana mechi pekee ambayo yanga huwa wanaikamia ni ya simba tu

Yani yanga wako radhi wafungwe na timu nyingine yoyote ila siyo simba mradi tu wawafurahishe mashabiki wao mazumbukuku, sasa simba hawakutaka kurisk kuingia robo fainali timu ikiwa na wachezaji kadhaa majeruhi, maana wao yanga hata wachezaji wao wangeumia wasingekuwa na cha kupoteza sababu hawakuwa wakishiriki michuano yoyote migumu

Na lengo la simba limetimia kwamba hakuna kucheza mechi yoyote na yanga hadi wamalizane na mechi za kimataifa kwanza, baada ya hapo sasa simba hawatakuwa na hofu tena ya kukamiwa na yanga, na sidhani kama kuna watu wanatamani derby ichezwe kama mashabiki wa simba maana kwa sasa wanajua hakuna wa kuwafunga simba tena
 
Mnapenda sana kujitoa ufahamu sasa ambacho hujamuelewa mtoa mada ni nini hicho kikosi huo uzuri wake mnashindwa vipi kuuonesha huko kimataifa mnaishia kuuonesha kwa kina kengold tu, mfano cafcl katika makundi yote kundi lenu ndilo lilikuwa jepesi na hata wenyewe mlishangilia mlivyopangwa nao ila cha ajabu mkashindwa kuvuka sasa huo ubora uko wapi, anyway mimi naona endeleeni kujiona mna kikosi kizuri msikiboreshe wala msiache kufanya match fixing ili kimataifa muendelee kuishia hatua za awali sisi ndio furaha yetu
Kimataifa wapi?

Kama klabu bingwa hata kushiriki ulishindwa kwa ubovu wa timu yako ukadondokea kombe la waliofeli shirikisho ambalo sasa hivi mashabiki wa simba mmelipa thamani kubwa kuliko kombe la dunia.

Kwa kushiriki klabu bingwa tu na wewe kushindwa inathibitisha Yanga ni bora kuliko wewe.

Kama wewe ni bora mbona ulishindwa kushiriki klabu bingwa?
 
Tatizo mkiambiwa ukweli mnabisha, kwa taarifa yenu simba waligomea ile mechi sababu walikuwa na wasiwasi wachezaji wa yanga wanaweza kukamia mechi, wakawaumiza baadhi ya wachezaji wa simba maana mechi pekee ambayo yanga huwa wanaikamia ni ya simba tu

Yani yanga wako radhi wafungwe na timu nyingine yoyote ila siyo simba mradi tu wawafurahishe mashabiki wao mazumbukuku, sasa simba hawakutaka kurisk kuingia robo fainali timu ikiwa na wachezaji kadhaa majeruhi, maana wao yanga hata wachezaji wao wangeumia wasingekuwa na cha kupoteza sababu hawakuwa wakishiriki michuano yoyote migumu

Na lengo la simba limetimia kwamba hakuna kucheza mechi yoyote na yanga hadi wamalizane na mechi za kimataifa kwanza, baada ya hapo sasa simba hawatakuwa na hofu tena ya kukamiwa na yanga, na sidhani kama kuna watu wanatamani derby ichezwe kama mashabiki wa simba maana kwa sasa wanajua hakuna wa kuwafunga simba tena
Hovyoo kabisa... Huyu ni mmoja ya wale wa Rage.
 
Acha ujinga 🤣🤣🤣

Kuna mwenzio kaeleza vizuri sababu zenu kwa kiwango fulani nimeona zina mashiko.
 
Back
Top Bottom