Wewe ndio unajitoa ufahamu na kutupangia maisha namna ya kuyaendesha.
Sentensi ya mwisho nimeandika Yanga ni bora sana na itaendelea kuimarika wewe unakuja na maneno msiboreshe kikosi. Timu inaimarikaje bila kuboresha kikosi?
Unazungumzia kimataifa gani ambayo Yanga imeshindwa kuonyesha uwezo wake? Hapa ndio inaonyesha unajitoa ufahamu. Yanga ilitotolewa club bingwa ikaenda shirikisho na kwenda fainali moja kwa moja. Timu ya kwanza toka Tanzania kufika fainali za shirikisho ni Yanga. Unataka uone nini hadi uamini ni timu bora? Kuna match fixing yoyote ilihusika kufika fainali?
Msimu huu Yanga alikuwa anashiriki mashindano ya club bingwa ya Afrika. Unaelewa maana yake? Haya mashindano hachukuliwi mshindi wa tatu au wa nne kwenye ligi ni mabingwa na runners up tu. Simba haikupata nafasi hiyo ikadondekea shirikisho kwa shingo upande. Eti leo mnajivunia mashindano ambayo alipokuwa akishiriki Yanga mliyabeza. Hivi ni vituko.
Ukweli ni kuwa mngeshindwa kuwatoa hao waafrika kusini mnengeabisha nchi na kuishusha thamani ligi yetu. Jambo zuri mmeshinda heko kwenu ila muache kudharau mashindano fulani halafu mkiwa huko mnayageuza kuwa champions league.
Ushauri wa mpinzani siku zote ni kituko hatuwezi kuuchukua hausaidii chochote kwetu.