Hiki ni kiwango kilichopitiliza cha Ukatili kwa watoto

Mtoto unampa MACHAGUO? Jesu!
Yaani mkuu kuwaelewa hawa watu ni kazi.

Eti mtoto ana machaguo!!!! Waafrika mbona kila kitu sisi Tupo gizani. Tena na Elimu zetu uchwara hizi lakini Bado mambo madogo madogo kama haya tunashindwa kuyadadavua hadi tutumie akili za mabeberu!!!!
 
Kuna shule ya ipo karibu yangu hapa madogo wanakula sana mboko, sasa imagine dogo kala mboko skuli, kafika home msosi hakuna, anawahi madrasa huko nako anakutana na bakora 5 za moto.

Huyu akija kua kibaka kukutia bisu hataona kazi dadeki.
Kabisa. Hawa ndiyo wakiwa viongozi wanaamuru mtu ashushwe kwenye bus na kuuawa.
 
Yaani mkuu kuwaelewa hawa watu ni kazi.

Eti mtoto ana machaguo!!!! Waafrika mbona kila kitu sisi Tupo gizani. Tena na Elimu zetu uchwara hizi lakini Bado mambo madogo madogo kama haya tunashindwa kuyadadavua hadi tutumie akili za mabeberu!!!!
Peleka unyama wako huko huko kwa familia yako. Wengine tumebahatika kukulia kwenye familia za kistaabu.
 
Ni saikolojia unapotaka kumfanya mtu awe katili lakini mwenye nidhamu kwa bosi wake .
Hao watoto hua ni wakatili sana kwa watoto wenzao hasa wasio wa dini yao lakini wanawaogopa sana walimu wao na kuona kuwa kila wakachofundishwa ni sawa na halina makosa wala haliwezi kuhojiwa .

Saikolojia kama hiyo waliitumia wakoloni kuwafanya majahanti wa kiafrika kuwa waoga sana . Hali hiyo iliwafanya wawe dhaifu mbele ya wazungu lakini katili sana mbele ya waafrika wenzaonzao . Yaani Ndio maana walikua wanawabeba wazungu na kuwavusha salama kwenye Mto mkubwa wenye Mamba badala ya kuwatupa mtoni wakaliwe na mamba .

Na pia ipo gerezani kuna mtu anaitwa mnyapara . Ni mtu anayenufaika na maisha ya kikatili kwa wenzake na amelelewa kikatili na analipa ukatili huo kwa wenzake .

Watoto kama hao hawana huruma . Hatukatai watoto kudahibiwa lakini je, nani anaweza kujua kiwango cha adhabu kulingana na umri wa mtoto ,afya yake ,kosa lake na aina na ubora wa fimbo maana kuna mitiingine ina sumu inayowasha sana ngozi ya mtu.
.
Yote kwa yote wakoloni walitumia mbinu ya kikatili sana kueneza ukoloni ikiwemo baadhi ya dini .

Wamasai wanawafundisha vijana mila zao na ujasiri mkubwa huku wakiwa na nidhamu na heshima kubwa sana kwenye jamii yao kuliko mila zote duniani lakini wazungu na waarabu walitumia mbinu na uongo mwingi kuziita mila zote nzuri za waafrika kuwa ni ukafiri na upagani.
Matokeo yake tumetengeneza makafiri wakubwa zaidi
 
Ili washinde 30,000,000/= pale kwa Nkapa wakishinda sifa zote kwa Hostadh alowafundisha kwa kuwatia mikwaju hio ni moja tu imeenda viral ila ndio kinachoendelea huko Mudrasa
😁😁😁
 
Rudia kusoma nilichokiandika tena.
Bila shaka uliishia kujifunza tamaduni za Waarabu ama Wazungu.
 
Jiandae kutembelewa na Sheria ya mtoto na 21 ya Mwaka 2009 na marekebisho yake, labda tusisikie nakwambia
 
Sikiliza niwaelimishe, hakuna mtoa huduma yoyote kwa umma ambaye hajasajiliwa na Sheria yoyote. Nyumba zote za Imani yoyote ile zimesajiliwa mambo ya ndani kule. Kuna Sheria na kanuni zake. Ukikosea unatembelewa na sheria, full stop
 
Hawa wanaobisha ndugu yangu waulize hata kama wanajua hata tafiti moja tu ya madhara ya malezi ya kupiga watoto kwenye zama sasa, majibu hawana. Hizi Sheria zisingekuwepo nadhani tungekuwa sasa tunazika watoto kila siku kisa vipigo. Hivi sasa ninaye mmoja huko Tanga kaumizwa Yuko hospitali, kisa katoa ushahidi wa kweli mahakamani baada ya kufanyiwa ukatili.
 
Sikiliza niwaelimishe, hakuna mtoa huduma yoyote kwa umma ambaye hajasajiliwa na Sheria yoyote. Nyumba zote za Imani yoyote ile zimesajiliwa mambo ya ndani kule. Kuna Sheria na kanuni zake. Ukikosea unatembelewa na sheria, full stop
Asante sana kwa ufafanuzi Mheshimiwa.

πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
 
Yaani, eti mtu anazaa ila kulea, anayo sera ya kupiga. Watoto wengine wagonjwa wa akili, kadri unavyompiga anaugua zaidi.... Ndiyo maana baadhi ya Wazee kumbe bond na watoto hakuna, kumbe vita ya hisia ilianza zamani
 
Mbona mimi nimewahi, kupigwa viboko 30 nikiwa form three na bila kosa la maana kabisa, wanao one ukatili ni wale Walio lelewa kama yai Ambao wanahitaji uangalizi wa wazazi mpaka wafikapo miaka 30 hivi.
Hyo ni Hali ya kawaida ila kwa wale born town, shule magari ya njano hawawezi jua na hao ndio kizazi dhaifu kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…