Hilda Newton: Siwezi kukubali Ubunge wa kuhalalisha haramu

Aende akae kimya for 5 years, ale mpunga huo. Our MPs are paid handsomely!! Aje nimshauri. Napenda mabadiliko lakini hayatatokea kwa yeye kutoenda bungeni. Let her go, oiii
 
Mawazo ya mtu mwenye ufukara wa mawazo. Pole! Nyerere angemua kufundisha Pugu na kuacha kupigania uhuru wetu, Tanzania ingekuwa wapi leo!

Tofautisha ualimu wa mwaka 1954 na ubunge wa mwaka 2020.

Halafu huo uanaharakati wa kusakizia wenzenu sio uanaharakati, mwenyewe hapo unaandika kishujaa wakati umekumbatia kiajira fulani ambacho hiwezi kukiacha hata kwa wiki moja tu.
 
Motivation yako ni pesa kama Judas Escariot. Hilda yuko tofauti. Watanzania mil 60 hawezi kuwa na malengo ya pesa tu kama wewe. Nyie ndio mnaoua wenzenu kwa sababu ya pesa.

Unashindwa hata kuelewa kwa nini Baba wa Taifa aliacha kazi yake yenye mshahara na kwenda kufanya kazi isiyokuwa na mshahara ya kupigania haki za Watanganyika. Kama ni mjinga kiasi hicho siwezi kukubadilisha. Endelea kuua kwa ajili ya pesa. Mungu anakuona.
tofautisha ualimu wa mwaka 1954 na ubunge wa mwaka 2020.

halafu huo uanaharakati wa kusakizia wenzenu sio uanaharakati,mwenyewe hapo unaandika kishujaa wakati umekumbatia kiajira fulani ambacho hiwezi kukiacha hata kwa wiki moja tu.
 
Unaweza shangaa watu wanabwabwaja na kumsifu kamanda #madam-twita kumbe hata jina lake halijapitishwa 😂😂😂😂
 
Mkuu hizi ni kauli za kishujaa mitandaoni na hazina uhalisia wowote

Nyerere ni sawa na Dr Slaa alipokubali kuachia kugombea ubunge aliokua na uhakika nao kwa asilimia mia na akakubali kugombea urais ambao alijua fika hawezi kushinda kwa makubaliano ya kulipwa haki za sawa na mbunge atakaposhindwa.........same applied to Mnyika mwaka huu
Nyerere alihakikishiwa kipato na maisha zaidi ya mshahara wake na wazee wa Dar
Walimchangia na kuhakikisha anapata mahitaji yake yote

Sasa huyu Hilda anakua muhanga kwasababu tu akina Mbowe hawajapa ubunge na wao
2015 hatukuyatambua matokeo lakini sikuwaona akina mbowe na lema wakiukataa ubunge wao

Sasa hizi ni kesi mbili tofauti kati ya nyerere na hilda
 
Unaweza shangaa watu wanabwabwaja na kumsifu kamanda #madam-twita kumbe hata jina lake halijapitishwa 😂😂😂😂
Mkuu mimi naamini wanasiasa wamepigana vita vyao vya kutosha....tena wamepigana kiume wanapaswa kupongezwa
Tulioshindwa kumalizia hii vita tupate ushindi ni sisi ambao kwa bahati mbaya sana tuliishia kujificha nyuma ya keyboard zetu na kuendesha mapambano yasio na tija mitandaoni

Nashangaa hata kasehemu kadogo sana ka matunda ya upambanaji wao kanataka kupotweza as if ndio italeta matokeo chanya yoyote
Maisha lazima yaendelee watu wanahitaji kula pia na chama kinahitaji watu wakukisemea bungeni
Kwa mwendo huu wa kukataa huu ubunge baada ya miaka 5 cdm itakua imekufa kisiasa
 
Huyu dada CHADEMA wamepata jembe
Mkuu Babati ,CHADEMA na ACT - Wazalendo kuna wadada majembe sana sana kwa kweli. Japo nipo mbali na nyumbani,lakini nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa hawa wadada kupitia video za mikutano yao ya kampeni.
Hakika hawa ni hazina ya taifa.
Mwenyezi Mungu awabariki na awalinde ili taifa linufaike nao.
 
Hakuna asiye na njaa upinzani, wote wanasubri baba yao mbowe atoe ruhusa utawaona wanavyo kimbizana kama fisi.
 
Sifa za kijinga zitampa umasikini.. wenzake wana connection na Balozi yeye anahangaika tu na Twitter utadhani itampeleka Ulaya na Marekani.
Tunamuomba Mungu awanusuru wa uzao wako, wajitambue walinde thamani na utu wao, wasije wakawa wa 'kununulika na kuchezewa' hivyo. AMEN
 
Umetoa wazo zuri sana, lakini ‘mama Tanzania na NCCR yake, pamoja na Mrema na TLP yake, wameshalitendea kazi wazo hilo! Tuoneshe mafanikio ya huo ‘ustaarabu’ ili CHADEMA nao wafanikiwe!
 
Kosa kubwa upinzani tulifanya kususia bunge la katiba ni heri tungebaki ikapitishwa ile katiba ya ccm maana ni heri ilikuwa na tume huru na raisi kupunguziwa madaraka .Tusingejikuta natulio kutana nayo uchaguzi huu 2020 .lazima viongozi wa upinzani wakubali walikosa hekima na maarifa kwa ajili ya gadhabu, ushauri wangu viongozi wetu haijalishi umetegewa au bahati mbaya au ni kwa uzembe umeanguka, cha msingi kuinuka na kusonga mbele safari kwa kutumia maarifa na ustadi mkubwa.

Kwa wacha wabunge viti maalumu waende bunge na uwe mwanzo wa harakati za kudai katiba ile ilipitishwa na ccm iletwe tuipigie kura bila masharti yale yalio tutoa bunge la katiba .angalau tupate tume huru na kupunguzwa kwa madaraka ya raisi .tuanzia hapo tujipange kwa uchaguzi ujao.

Vinginevyo kwa uzoefu ccm itaturudisha kwenye chama kimoja.yaani kosa la kususia bunge la katiba ilikuwa sawa na kumsusia nyani shamba lako la mahindi .napia haikuwa busara kutaka kila unacho taka upate 100% unapokwenda kuingia kwenye meza ya majadiliano ,lazima tukiri ili kosa tuanzi na akili mpya .
 
Ameona haya tu huyo.[emoji6][emoji16]

Ndio sifa ya mtu muungwana kuona haya, kwa mtu ustaarabua ni ngumu kushiriki bunge kibogoyo lililopatikana kwa kunajisi uchaguzi na umwagaji wa damu.
 
Huo ni ujinga kama siyo uboya!

Anafikri harakati za siasa zimeanza leo?

Ngoja CHADEMA Ife kabisa, iko siku ataikumbuka hii bahati

Ccm ndio wanatetemekea pesa, hii ndio inayopelekea wao kutumika hata kwa mambo ya kipumbavu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…