Hilda Newton: Siwezi kukubali Ubunge wa kuhalalisha haramu

Hilda Newton: Siwezi kukubali Ubunge wa kuhalalisha haramu

Kosa kubwa upinzani tulifanya kususia bunge la katiba ni heri tungebaki ikapitishwa ile katiba ya ccm maana ni heri ilikuwa na tume huru na raisi kupunguziwa madaraka .Tusingejikuta natulio kutana nayo uchaguzi huu 2020 .lazima viongozi wa upinzani wakubali walikosa hekima na maarifa kwa ajili ya gadhabu ,ushauri wangu viongozi wetu haijalishi umetegewa au bahati mbaya au ni kwa uzembe umeanguka ,cha msingi kuinuka na kusonga mbele safari kwa kutumia maarifa na ustadi mkubwa .Kwa wacha wabunge viti maalumu waende bunge na uwe mwanzo wa harakati za kudai katiba ile ilipitishwa na ccm iletwe tuipigie kura bila masharti yale yalio tutoa bunge la katiba .angalau tupate tume huru na kupunguzwa kwa madaraka ya raisi .tuanzia hapo tujipange kwa uchaguzi ujao.vinginevyo kwa uzoefu ccm itaturudisha kwenye chama kimoja.yaani kosa la kususia bunge la katiba ilikuwa sawa na kumsusia nyani shamba lako la mahindi .napia haikuwa busara kutaka kila unacho taka upate 100% unapokwenda kuingia kwenye meza ya majadiliano ,lazima tukiri ili kosa tuanzi na akili mpya .

Hizi lugha ndio ziliwafanya cdm wakashiriki uchanguzi huu wa kishenzi. Matokeo yake imekuwa ni hujuma za wazi zaidi ya hapo awali. Tunasema hivi, mbunge yoyote wa cdm hasa wa viti maalum kujipeleka kwenye hilo bunge ni kutufanya kumpuuza moja kwa moja.
 
Namnukuu:

"Sifahamu chochote kuhusu orodha ya majina ya Wabunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA inayosemakana kuwa imepelekwa Tume hata hivyo hata kama kweli jina langu lipo siwezi kwenda kuapishwa kuwa Mbunge maana binafsi siwezi kushiriki mchakato wa kuhalalisha haramu kuwa halali"


My Take 1
Tunataka tusikie kauli ya Halima Mdee na Esta Bulaya.
Hahahaaa ww unajiliwaza tu nani akuchague?? Kwa umaskini ulionao ww wa kuacha ubunge?? Hahahaa sizitaki mbichi hizi
 
Kosa kubwa upinzani tulifanya kususia bunge la katiba ni heri tungebaki ikapitishwa ile katiba ya ccm maana ni heri ilikuwa na tume huru na raisi kupunguziwa madaraka .Tusingejikuta natulio kutana nayo uchaguzi huu 2020 .lazima viongozi wa upinzani wakubali walikosa hekima na maarifa kwa ajili ya gadhabu ,ushauri wangu viongozi wetu haijalishi umetegewa au bahati mbaya au ni kwa uzembe umeanguka ,cha msingi kuinuka na kusonga mbele safari kwa kutumia maarifa na ustadi mkubwa ..

..sikubaliani na hoja zako, au maoni kwamba katiba mpya ilikwama kwasababu Cdm / Ukawa walisusia bunge maalum la katiba.

..ukweli ni kwamba CCM walikuwa na akidi ya kutosha kuendelea na mchakato wa kuandika katiba mpya.

..kwa maneno mengine Cdm / Ukawa hawakuwa na akidi ya kutosha kupitisha au kuzuia jambo lolote lile ktk mchakato wa katiba mpya.

..pamoja na Cdm / Ukawa kujitoa bunge maalum la katiba liliendelea na vikao vyake, na lilikamilisha zoezi la kuandika katiba mpya.

..tatizo ni kwamba CCM wameweka "mfukoni" katiba waliyoiandika, wakati walitakiwa waendeleze mchakato wake kwa kuileta kwa wananchi ili kuwe na kura ya maoni.
 
Yaan kama chadema mmemuacha kumteua viti maalum yule mwanamke wa CHATO Basi nyie mtakua wa ovyo kabisa na hatutawaelewa utampaje ubunge mke wa mboe au mnyika sijui msigwa afu mpambanaji yule umuache
 
Then this time watakifuta, hakuna haya ya kuwa na chama ambacho wao kila kitu ni kususa tu

Nasema hivi wamechelewa. Mpigie Magufuli mwambie atangaze cdm kufutwa hata mchana huu, ila hatuko tayari kugeuzwa mazoba wa kuporwa haki, na kushiriki bunge lilipatikana kwa umwagaji damu. Kawapeni NCCR na CUF wao ndio wanamnyenyekea rais, na wanatetemekea vyeo vya mbeleko. Hilo bunge ni upuuzi kama upuuzi mwingine.
 
Nasema hivi wamechelewa. Mpigie Magufuli mwambie atangaze cdm kufutwa hata mchana huu, ila hatuko tayari kugeuzwa mazoba wa kuporwa haki, na kushiriki bunge lilipatikana kwa umwagaji damu. Kawapeni NCCR na CUF wao ndio wanamnyenyekea rais, na wanatetemekea vyeo vya mbeleko. Hilo bunge ni upuuzi kama upuuzi mwingine.

Ndugu yangu hapa ni Africa hapa sio ulaya

Unaleta mambo ya kushindana na Serikali unadhan Nani atapata hasara?

Nenda road basi tujue kweli ww una hasira, unaongea umejificha kwenye keyboard?
 
Wabunge wanalipwa pesa nyingi Sana zinahujumu uchumi posho ya laki 3 ni nyingi Sana kwa siku wapewe elf 50,pia mshahara wao upunguzwe badala ya milioni 12 wapewe milioni na nusu, kuinua mgongo chao ni kingi Sana wapewe milioni 12,ili pesa zitumike kwenye ujenzi wa nchi kwa maana tunapoteza pesa nyingi Sana kuwalipa wabunge nao washiriki kwenye kufunga mkanda ili nchi ikishajengwa ndo waje walipwe pesa nyingi na sio sasa
 
Wapinzani walikuwa bungeni msimu uliopita, ni kipi kipya kilifanyika? Acha Magufuli kuzuia siasa afute hata hivyo vyama vya siasa ibaki ccm, sioni ni kwanini mtu akashiriki kwenye bunge lililopatakina kwa uharamia. Kama huna uwezo wa kupata hela nje ya bunge hapo sawa. Huyo Hilda hajawahi kuwa mbunge, umewahi kumuona akijipendekeza ili apate madaraka ya mbeleko? Mbona ana mvuto kuliko Tulia ambaye ni spika? Ubunge usiwatoe utu kisa pesa.

Sasa kuwepo bungeni ndio ulitaka kila jambo lao likubaliwe?
 
Ngoja ruzuku ikatwe, tutaelewana tu

Kukata ruzuku mbona hilo dogo futeni hicho chama kabisa. Tunajali utu kuliko kuendekeza siasa za tumbo, huku watu wameuawa, kuachwa na vilema na uporaji mkubwa wa kura.
 
Maisha mtaani ni magumu sana, CCM hizi hatua zote wanazochukua wanaelewa ya kuwa maisha ni magumu, Cement 35,000/-

Hata huyu Hilder N , jina lake likiappear ataenda, mark my words.

Mungu Ibariki CHADEMA, Mungu mbariki Tundu A Lissu.
 
Ni lipi limewahi kukubaliwa ili useme wasipokuwepo sasa hivi ndio watakacho hakitafanyika?

Sasa unajua sababu ni kuwa wao ni wachache, na mfumo wa bunge ni kupiga kura Sasa unategemea nn?
 
Kukata ruzuku mbona hilo dogo futeni hicho chama kabisa. Tunajali utu kuliko kuendekeza siasa za tumbo, huku watu wameuawa, kuachwa na vilema na uporaji mkubwa wa kura.

Sasa mkigoma ndio Hao watu wanafufuka au
 
Sasa mkigoma ndio Hao watu wanafufuka au

Hawafufuki lakini tunawapa heshima zao. Endeleeni nyie na karamu ya shetani, sio kila mmoja anashiriki uovu kwa ajili ya pesa za kujikimu na umaskini.
 
Hawafufuki lakini tunawapa heshima zao. Endeleeni nyie na karamu ya shetani, sio kila mmoja anashiriki uovu kwa ajili ya pesa za kujikimu na umaskini.
Weee jamaa bwana,
Heshima ni muende bungeni mkawasemee watu wenu, kuliko kususa then mnakosa platform ya kuongea

Nyie ndio mnatumika na ccm kuua upinzani
 
Mkuu Babati ,CHADEMA na ACT - Wazalendo kuna wadada majembe sana sana kwa kweli. Japo nipo mbali na nyumbani,lakini nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa hawa wadada kupitia video za mikutano yao ya kampeni.
Hakika hawa ni hazina ya taifa.
Mwenyezi Mungu awabariki na awalinde ili taifa linufaike nao.
Tuwasupport mkuu hata kwa kuwatia moyo
 
Back
Top Bottom