Hili la Bandari, lawama hii iende kwa hayati Magufuli

Wakati hao wapinzani wako wengi bungeni waliwahi kuzuia hoja gani isipitishwe na ccm!
Suala sio kuzuia. Kama walikuwa wachache ulitaka wazuiaje?
 
Lakini wangekuwepo wale wabunge machachari wa upinzani wakiongozwa na Tundu Lissu Bungeni bado mambo mengi yangepitishwa na wabunge walio wengi ambao ndio hao hao waliopo sasa !! Wenye kuafiki waseme ndiooo na wasioafiki waseme siyooo ! Wenye kuafiki wameshinda 😅😅😅🙏
 
I like most of your posts and comments because you think straight.

Unajua, sisi binadamu ni watu wa ajabu sana. Tumepewa utashi wa kung'amua mambo lakini kwa bahati mbaya sana kuna baadhi ya watu hawautumii utashi huo na badala yake wanaendeshwa na mihemko.

Sawa tukubali Magufuli alikosea. Swali la msingi ni je, baada ya kuwapeleka ma-CCM mengi bungeni, aliyashikilia na utashi (akili) zao? Na anaendelea kuzishikilia hadi akiwa kaburini? Jibu ni hapana.

Walipaswa wasimamie ukweli wa mambo ambao hata huyo Magufuli angeusimamia kama angekuwa hai.

Siyo mtu anashiba makande yake yenye chumvi huko Manzese kwa Mfuga mbwa halafu anakuja kuharisha tu humu.

Rubbish!
 
Magufuli kaingiaje hapa, unaacha kumsema mtu aliyeamua mwenyewe kwa akili yake na hulka yake kusaini mkataba wa kijinga. Unamhusisha JPM Tena? Tafadhali leave the legend to rest in peace ,just tell your bad and merciless Mom.
 
Magufuli kaingiaje hapa, unaacha kumsema mtu aliyeamua mwenyewe kwa akili yake na hulka yake kusaini mkataba wa kijinga. Unamhusisha JPM Tena? Tafadhali leave the legend to rest in peace ,just tell your bad and merciless Mom.
Ulivyoanza kuniuliza kwenye huo mstari wa kwanza umethibitisha kuwa hujasoma.
 
Matatizo ya nchi hii ni njaa huwa inakimbilia kichwani!
 
CCM walilikoroga zege wenyewe, sasa ni wakati wa kulinywa bila kumhusisha hayati J.P. Magufuli. Ikumbukwe kuwa hiki ni kipindi cha pili cha awamu ya tano japo wao wameng'ang'ania awamu ya 6 na Rais ni wa 6.

Usanii uliotumika wa kulazimisha kuwa awamu ya 6 bila kuwepo kwa uchaguzi, yumkini yote yanayotendeka katika kipindi hiki ni ya Samia Suluhu Hassan na jopo la mawaziri na watendaji waliomo kwenye cabinet ya sasa..... Kumtafuta mtu wa kumlaumu baada ya kifo cha JPM si halali wala siyo haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…