Hili la Dkt. Mpango kuwa Makamu wa Rais ni "mchafukoge" tafakari

Hili la Dkt. Mpango kuwa Makamu wa Rais ni "mchafukoge" tafakari

Wewe unajuaje?Huenda Bwana Mpango ndiye aliyemtonya Mama kuhusu hilo sekeseke la ukwapuaji!!
 
Pengine yeye ndiye sababu ya kuonekana huo ufisadi, Time will tell
Good point.
Paymaster General huwa ni Katibu Mkuu. Waziri husimamia sera na mipango. Katibu mkuu ndiye msimamizi wa utawala na matumizi.

Hata hivyo, tunaendelea kurudia makosa yale yale. Tunajenga watu na sio taasisi. Je "Utawala wa Rais Suluhu" utajenga taasisi au watu?

Kama ulivyo malizia, time will tell.
 
Toeni majungu yenu serikali imevipa vyombo huru kuchunguza na tayari kazi imeanza, jana mmemsifu CAG leo mnamkana kwamba hana meno, tulieni mpeni muda CAG na TAKUKURU. Tumetekeleza Kazi inaendelea
 
Hoja mujarab...!!!
You know what? CCM ni walewale pengine hii ni kujaribu kuficha uozo wa BOT!!
Huwezi kuhoji upotevu wa Fedha BOT ukamtenga Waziri wa Fedha, Gavana BOT na Mweka Hazina Mkuu wa Serikali. Hapa ni kupigwa changa la macho tu!
 
Nitafutie mtu ambaye HANA kasoro ili na sisi tukueleze KASORO zake. Anyway, una haraka gani? TAKUKURU na CAG wanachunguza, ukisema hivyo maanake hata yule wa bandarini basi hata waziri wa uchukuzi na yeye awe nje ya ofisi hadi majibu yapatikane. Watanzanai wengi ni mabingwa wa KUKOSOA but sio wazuri saana wa kutoa solution ya kile wanacho kilalamikia. Big up mama kwa kuficha SIRI, yaani Mpango hadi anakwenda jadiriwa bungeni, hakuna mwenye alikua anajua? Strange.
 
Kwann hujafikiri kuwa yeye alikuwa ni sehemu ya kutatua tatizo la matumizi ya hizo pesa?
 
Naenda kuuona kesi zote juu ya wapigaji wa BOT zikifa kwa maana watamtaja huyu mteule.
 
Cv yake ni kali ! Akiitumia vizuri Tz ya marehemu JPM itazidi kusonga mbele . Hongera Mama kwa kuona mbali .

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
Hii ni Tanzania ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan. Huwa hatuongozwi na wafu
Ya Magufuli ilikwisha siku aliyotoa Roho akabaki kwenye machine mpaka walipotangaza rasmi. Tuheshimu Utawala na ukiisha umeisha. Hatuna Tanzania ya Magufuli sisi.
 
Swali fikilishi,
Wewe unajuaje?Huenda Bwana Mpango ndiye aliyemtonya Mama kuhusu hilo sekeseke la ukwapuaji!!
Hapa naona Kama vp atatumiwa vizuri, wakaongezewa washauri wa uchumi wazuri,Kama mshauri wa rais atamsaidia Sana,lakini pia wizara ya fedha na mipango ndo uti wa mgongo ili taifa liweze kusonga, so KWA KUA anaijua na mianya ya upigaji anaijua,zikiwemo na account mbali za kufanyia ufisadi atasaidia Kama Kuna nia ya dhati,maana wizara ya fedha kunaupigaji huko sio wa dunia hii ,ni wizara ya connection,vinginevyo tusubili mda mwalim mzuri
 
Dr Mpango ni chaguo sahihi.

Yuko very professional,humble and very experienced kwenye masuala ya uchumi.

Kwamba kuna fununu ya upigaji BoT,pengine upigaji ulifanyika kipindi kile Mpango alipokuwa mgonjwa. Hata sasa, kwa muonekano,bado hajastabilize.
 
Back
Top Bottom