Hili la kuweka vibao viwili Kwa Nchi Moja Tanzania na Zanzibar limekaaje?

Hizo ni mbwembwe tu ila hata wao wanajua muungano hauvunjiki na Zenji si nchi na wataishia kwenye kuweka vibao vya uwakilishi wa Zenji tu. Siku jeshi likigawanyika pande mbili miaka zaidi ya 1000 ijayo ndo itakuwa mwisho wa Tanzania.
 
Wewe ni Lawyer uliyegraduate University of Dar , lakini huna knowledge ya Diplomasia. Cha ajabu unapotosha. Zanzibar hakuna Embassy (Ubalozi); bali kuna Consulate (Ubalozi mdogo). Kila nchi inaruhusiwa kuweka Consulate kama wanataka kutokana na uwigo wa shuguli zao. Kuwa na consulate ni gharama kwa nchi maskini. Siyo special treatment kama usemavyo wewe. Na kuna Ambassador na Consular General huyu ndiyo yupo Zanzibar siyo Ambassador
 
Duh...!, na hivi ni vitu vidogo kuhusu ubalozi na ubalozi mdogo!.
P
 
Kwa tafsiri ya uswahilini huku bila kuweka maneno kama giant na minority, ni sahihi nikisema mwl nyerere alikubali kuiua Tanganyika na kukubaliana na masharti kama yalivyo katika muungano huu chao chao, chetu chao, maana sioni dalili ya Mtanganyika kuwa rais wa zanzibar ila wao wanapeta tu kwetu sio kwamba mm ni mbinafsi kutumia neno kwetu ila kama umefika kwao na kuona siasa zao wao bado wana ubinafsi. Kwa nini nyerere alikubali masharti haya? je aliona kuilinda Ikulu na Dar es salaam kupitia bahari ya Hindi njia pekee ni kuimiliki zanzibar?
 
Nikuletee picha ya Mzee wangu yupo kikaoni na bango la Zanzibar toka miaka iyo ya 80 to 90? Picha zipo hapa home ila kuziweka ni ngumu
 
basi itabidi urudie kugoogle uelewe maana ya muungano,halafu uje uniambie kama kuna nchi ya zanzibar, nchi ya tanganyika iko wapi?
unaniuliza mimi nchi ya tanganyika iko wp? Yaulize maccm wenzio mbona hushangai zanzibar ipo na ina kila ktu chake kama nchi wakati huohuo tanganyika hata kutajwa tu ni kosa. Nenda katafute katiba ya zanzibar uisome uone yaliyomo ajabu tanganyika haipo hakuna bendera, hakuna katiba, hakuna wimbo wa taifa nk. Ila tanganyka imemezwa na tanzania wkt huohuo zanzibar haikumezwa. Au nikuulize tu kwann zanzibar kuptia katiba yao inasema n nchi wkt tanganyka haisemwi popote. Funguka akili wewe hata mtoto mdogo nikimwelewesha ananielewa we unaleta propaganda za kiccm kwa watu wenye uelewa haya kawaambie vijijin huko.
 
Kwahiyo hata Bendera ya Zanzibar huijui.?

Zanzibar ilipata Kiti UN kabla ya Tanganyika na Kimsingi ndio hiki tunachomitumia sasa kwenye Union 😄😄🔥
Ilipata kiti UN lini Jee Tanganyika na Zanzibar nchi ipi ilianza kupata uhuru
 
Cha msingi ni kuvunja kabisa wala hauna maana
 
Hivi nchi hii kweli kuna Bunge? Au bunge alikuwa Ndugai peke yake? Hii picha ni ushahidi tosha
 
Ni suala la muda tu Zanzibar itakuja kujitenga, Unajua why SSH anamkubali lissu sababu lissu haungi muungano wa kitapeli huu hata mama yenu pia hakubali huu muungano coz upo kihuni kihuni.
Tatizo la Tz na pia Muungano, ni wa kisiasa, pili kama ilivyo kwenye vitu vingi, haujengi nidhamu na usawa, Bali unajenga, uhuni, upendeleo, na hujuma.hivyovkuondoavfaida za Muungano na kujenga picha hasi juu ya uwepo wa Muungano.
 
Ndio za waafrika hizo kukuinga sahani mbili kwenye sherehe. Hiyo inaitwa huku na huku.
 
Umekomaa na vibao vowili huna kazi za kufanya aisee hata kikiwa kimoja utalipwa nini?acha ukinga fanya mambo yako yanayokuhusu hayo ya vibao viwili hayakuhusu
 
Swali zuri sana! Swala la kuwepo kwa vibao viwili katika baadhi ya matukio yanayohusisha Tanzania na Zanzibar ni jambo ambalo limekuwa likizungumzwa na kujadiliwa kwa muda mrefu.
Angalia video hii HAPA

Sababu Za Kutokea kwa Hali Hii:

1. Muundo wa Muungano: Tanzania ni nchi ya muungano inayojumuisha Tanganyika na Zanzibar. Muundo huu unaruhusu kila upande kuwa na kiwango fulani cha uhuru katika masuala fulani.
2. Utambulisho: Wananchi wa Zanzibar wana utamaduni na historia ndefu ambao wanautambulisha na kuutumia katika kuonesha upekee wao.
3. Masuala ya Siasa: Kumekuwa na masuala ya kisiasa yanayohusu uhusiano kati ya Tanganyika na Zanzibar, na hii inaweza kuchangia katika kuonekana kwa vibao viwili katika baadhi ya matukio.
4. Mtazamo wa Kimataifa: Katika baadhi ya mikutano ya kimataifa, Tanzania na Zanzibar zinaweza kuwakilishwa tofauti ili kuonyesha utofauti wao wa kihistoria na kitamaduni.

Mtazamo wa Sheria na Sera:

MSheria ya Muungano: Sheria ya Muungano wa Tanzania inaelezea wazi wazi uhusiano kati ya Tanganyika na Zanzibar. Hata hivyo, tafsiri na utekelezaji wa sheria hii unaweza kuwa na mtazamo tofauti katika hali tofauti.
Sera za Serikali: Sera za serikali zinaweza kuathiri jinsi ambavyo uhusiano kati ya Tanganyika na Zanzibar unavyoonekana.

Athari za Kuwepo kwa Vibao Viwili:
Cheki HAPA
Utambulisho: Kuwepo kwa vibao viwili kunaweza kuimarisha utambulisho wa Zanzibar kama sehemu muhimu ya muungano, lakini pia kunaweza kuongeza hisia za kutokuwa na umoja.
Uhusiano wa Kimataifa: Katika ngazi ya kimataifa, kuwepo kwa vibao viwili kunaweza kuonekana kama ishara ya utofauti na hivyo kuathiri jinsi nchi nyingine zinavyotutazama.
Maendeleo: Kuna wanaoamini kuwa kuwepo kwa vibao viwili kunaweza kuchelewesha maendeleo ya nchi kwa ujumla, huku wengine wakiona kuwa kunaweza kuleta faida kwa pande zote mbili.
Zaid bonyeza HAPA
 
Lipi ni jepesi kufanyika?

1-kuifuta Zanzibar isiwepo na tuwe na serikali moja tu ya Tanzania

2-kuirudisha Tanganyika na tuwe na serikali tatu

Au
3- kila moja abaki kwake kama zamani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…