Hili la kuweka vibao viwili Kwa Nchi Moja Tanzania na Zanzibar limekaaje?

Hili la kuweka vibao viwili Kwa Nchi Moja Tanzania na Zanzibar limekaaje?

Lipi ni jepesi kufanyika?

1-kuifuta Zanzibar isiwepo na tuwe na serikali moja tu ya Tanzania

2-kuirudisha Tanganyika na tuwe na serikali tatu

Au
3- kila moja abaki kwake kama zamani?
Vingozi wanaapa kuulinda Muungano sidhani kama kuna Raisi anaweza Vunja Muungano suluhu ni kuwa na 3 Gvmnt.
 
Tumeona picha ya ujumbe wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ukiwa katika kikao huko China unavibao viwili. Kimoja kimeandikwa Tanzania na zingine kina wajumbe wameweka Bangor akiwa kibao cha Zanzibar
Mkuu kuna kile kitabu cha sungura alikuwa anakula share mbili
  1. cha wageni
  2. cha wote
Kama ulisoma hicho kitabu basi ukweli wake ndiyo huo pichani
 
Lipi ni jepesi kufanyika?

1-kuifuta Zanzibar isiwepo na tuwe na serikali moja tu ya Tanzania

2-kuirudisha Tanganyika na tuwe na serikali tatu

Au
3- kila moja abaki kwake kama zamani?
Kote ni shida tu kwasababu
  1. Patachimbika hapatakalika
  2. Kumlipa rais asiyesikilizwa upande mmoja na hasa huko Kiembembuzi ni hasara
  3. Watakufa na njaa watarudi kulialia huku
 
Kote ni shida tu kwasababu
  1. Patachimbika hapatakalika
  2. Kumlipa rais asiyesikilizwa upande mmoja na hasa huko Kiembembuzi ni hasara
  3. Watakufa na njaa watarudi kulialia huku
Hujajibu swali,

ila kwanini hakuna mtanganyika anaekubali zanzibar iwe kivyake?
Kama watakufa njaa, wataomba, watalia, watanuna nk nk si ni wao?
Kwannni watanganyika hili hatulitaki?
 
Hujajibu swali,

ila kwanini hakuna mtanganyika anaekubali zanzibar iwe kivyake?
Kama watakufa njaa, wataomba, watalia, watanuna nk nk si ni wao?
Kwannni watanganyika hili hatulitaki?
Tulishakubali siku nyingi ila wao hawataki kwasababu ndiyo loosers wamewekeza sana bara, na kwao hakuna ardhi
 
Mkuu kuna kile kitabu cha sungura alikuwa anakula share mbili
  1. cha wageni
  2. cha wote
Kama ulisoma hicho kitabu basi ukweli wake ndiyo huo pichani
Halafu anayekula share mbili tumbo lake dogo
 
unaniuliza mimi nchi ya tanganyika iko wp? Yaulize maccm wenzio mbona hushangai zanzibar ipo na ina kila ktu chake kama nchi wakati huohuo tanganyika hata kutajwa tu ni kosa. Nenda katafute katiba ya zanzibar uisome uone yaliyomo ajabu tanganyika haipo hakuna bendera, hakuna katiba, hakuna wimbo wa taifa nk. Ila tanganyka imemezwa na tanzania wkt huohuo zanzibar haikumezwa. Au nikuulize tu kwann zanzibar kuptia katiba yao inasema n nchi wkt tanganyka haisemwi popote. Funguka akili wewe hata mtoto mdogo nikimwelewesha ananielewa we unaleta propaganda za kiccm kwa watu wenye uelewa haya kawaambie vijijin huko.
Laahaula...ccm tena?
 
Tulishakubali siku nyingi ila wao hawataki kwasababu ndiyo loosers wamewekeza sana bara, na kwao hakuna ardhi
Sio kweli, watanganyika waliopo bara na wale wengine waliopandikizwa kule zenji ndio wanaoulinda muungano kwa nguvu zote,

Ila wazanzibari kama wazanzibari original hawautaki, na wakifurukuta kidogo wanatulizwa kilazima,
Unakumbuka uamsho? Uliona kilichotokea?
Walitolewa zenjiiiii wakashikilwa bara huku
Famchezo nini
 
Lipi ni jepesi kufanyika?

1-kuifuta Zanzibar isiwepo na tuwe na serikali moja tu ya Tanzania

2-kuirudisha Tanganyika na tuwe na serikali tatu

Au
3- kila moja abaki kwake kama zamani?
KILA MMOJA ABAKI KWAKE TANGANYIKA KIVYAKE NA ZANZIBAR KIVYAKE maswala ya serikali 3 n kuyapa nafas tu maviongoz majiz kuneemeka kwa kodi zetu tu. kila mtu apambane na hali yake
 
Wamenikera walivoweka kibao cha Tanzania ilhali TANGANYIKA ipo haijafa.
 
Hivi ni vitu vidogo, kuna nchi nyingi kabla ya Muungano zilikuwa na ubalozi Tanganyika na ubalozi Zanzibar, baada ya Muungano, nyingi zilifunga balòzi zake za Zanzibar na kubaki za Tanganyika zilizogeuka za Tanzania, miongoni mwa nchi ambazo hazikufunga ubalozi wake Zanzibar ni pamoja na yale mataifa makubwa matano yenye veto UN, Marekani, Urusi, Uingereza, Ufaransa na China, India pia haikufunga, bali walizigeuza balozi hizo kuwa balozi ndogo. Nchi hizi zinai treat Zanzibar with a special treatment of autonomous, hivyo wakitoa mualiko Tanzania inàalikwa kama nchi Tanzania na Zanzibar inaalikwa kama autonomous part of Tanzania hivyo kila mtu na mwaliko wake na kibao chake, bali Tanzania kama nchi ni nchi moja tuu, JMT!.
P
Are these the facts or are just your feelings and imaginations brother Pascal Mayalla...?

Do you have constitutional justifications on all of these you have said..?
 
Muungano wa ovyo kuwahi kutokea duniani! Binafsi siupendi kabisa kwa sababu Tanganyika inatumika kuineemesha Zanzibar huku Tanganyika ikiwa haifadiki na chochote.
Leo hii Tanganyika tunatawaliwa na Mzanzibari, ardhi yetu imekuwa ya wote lakini ya Zanzibar ni Wazanzibar tu,Wazanzibar huku Tanganyika wanashika cheo chochote, wanaajiriwa kwenye kazi yoyote lakini ni marufuku Mtanganyika kugombea nafasi yoyote ya uongozi Zanzibar wala kuajiriwa, Hata kupiga kura Mtanganyika haruhusiwi labda baada ya kuishi mfululizo kwa muda usiopungua miaka 3.
Huyo Rais anayeitwa wa Muungano hana madaraka yoyote Zanzibar hata DC wa kule anaweza kumvimbia na hana ubavu wa kumtengua labda akamshitaki kwa Rais wao! Uwa nashangaa sana hata sifa wanazopewa wale wanaoitwa waasisi wa Muungano sijui wanasifiwa kwa lipi wakati waliamua kwa makusudi kuisambaratisha nchi yetu tukufu ya Tanganyika!
Unaota
 
Lipi ni jepesi kufanyika?

1-kuifuta Zanzibar isiwepo na tuwe na serikali moja tu ya Tanzania

2-kuirudisha Tanganyika na tuwe na serikali tatu

Au
3- kila moja abaki kwake kama zamani?
After 60 yrs ndio kila mtu abaki kwake kama zamani!? Ndoto za Alinacha hizi
 
Sis na Zanzibar ni nchi marafiki ieleweke hivyo haijawahi kua nchi moja na haiwezekani zaidi sana tuendelee kuwafadhili tu.
 
Ninyi Vichogo wa Bara (Watanganyika) tulishawaambia siye tuna nchi yetu iliyostaarabika miaka mingi sio ninyi Vichogo nywele ngumu

Tuachieni nchi yetu
 
Tumeona picha ya ujumbe wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ukiwa katika kikao huko China unavibao viwili. Kimoja kimeandikwa Tanzania na zingine kina wajumbe wameweka Bangor akiwa kibao cha Zanzibar. Hizi ndio Sera ya Nchi yetu sasa, baada ya kupata Waziri Mpya wa Mambo ya Nje au ilikuwepo kabla. Na nini tafsiri yake kimataifa na ndani ya nchi

Pia soma:Nchi zilizoungana ni Tanganyika na Zanzibar, kwanini Zanzibar ipo na sisi ni Tanzania bara, kwanini wasioitwe Tanzania Visiwani?
Naona wamesahau kuweka bendera yao.
 
Back
Top Bottom