Kwanza kabisa limewashutua watu wengi sababu kwa mujibu wa muongozo utoji taarifa ni Rais,waziri mkuu au waziri wa afya, kwa nini hawajatupa taarifa kuwa kuna maabukizi ya covid 19 hapa nchini?
Ok fine kama kiongozi wa serikali ambae ni makamu wa kwanza wa rais Zanzibar amepata Covid 19,je muuza vitumbua huko forodhani Zanzibar? Je, haiwezi kuwa imeshavuka mpaka Dar es salaam maana kuna muingiliano mkubwa wa watu kati ya Zanzibar na Dar es salaam.
Kwa nini serikali ya rais JPM haitaki kutupa ukweli kuwa kuna maambukizi ya Covid 19? Mnataka yaliyotokea Brazili yatokee hapa Tanzania? Maana kama kuna maambukizi kwa nini tusiambiwe ukweli ili tuchukue tahadhali kwa hali ya juu?
Watanzania tuchukue hatua kujilinda maana tutapukukutika kama njugu. Maana kama viongozi wakubwa wanapata maambukizi alafu serikali inafanya siri,je sisi makabwela tukipata maambukizi tutaweza kutoboa?