Mwaka 2001 Wanafunzi wa kozi ya Unesi katika chuo Kikuu kishiriki pale Muhimbili wachagga walikua 24 Kati ya wanafunzi 28.
Unategemea nn katika soko la ajira?
Mkoa wa Kilimanjaro ndio Mkoa uliokua ukiongoza kwa shule za msingi na sekondari kuanzia miaka ya 1970-2010.
Fanya hesabu.
Ilikuwa ni fahari kwa kila familia ya Mchagga kuwa na Mtoto mwenye Digree au Padri katika miaka ya 1970-2010.
Takriban vitivo vyote pale UDSM 1970-2010 vilikua na aidha mkuu wa kitengo mchagga au msaidizi wake.
*********
Tuhuma za Mwenyekiti Mbowe...
Inawezekana kutokana na facts hizo hapo juu wimbi kubwa la wachagga walifanikiwa kuingia kwenye ajira rasmi na zisizo rasmi.
Mwendazake kuzuia ajira kwa wachagga serikalini, inawezekana ukawa ni ukweli ambao hauwezi kuthibitishwa popote... Zaidi ya hisia tu kama ambavyo wenyeji wa Mkoa wa Mara waliingia kwenye majeshi ya ulinzi na usalama.
VYOVYOTE IWAVYO
Yumkini ilikua ni wakati sasa wa kulitizama Taifa katika sura tofauti na ndipo mwendazake akaoneokana kuajiri ma Homeboy zaidi. Kitendo ambacho ni sahihi kwani kwa aina ya utendaji aliokuwa akiuhitaji alikua hana budi kuchukua watu ambao watakua loyal kwake.
APPROACH YA MBOWE
Bwashee angeweza kutafuta namna nzuri ya kuliongelea hili na sio kwa namna ambavyo ameamua kuli present kwa jamii ambayo madhara yake ni kwamba;
Makabila 130+ hayawezi ku sympathize na kabila moja ambalo kimsingi sio wanyonge wala masikini.
Tamko lake linaweza kuanza kuibua hisia za makundi mengine ambayo yamesahaulika na mfumo.
Mfano;
Waislamu, Wakristo lakini KKKT, Wanawake na kundi lenye watu wenye mahitaji muhimu (walemavu, Albino na Wasioona)
MY TAKE
CHADEMA kwa sasa kinahitaji Mwenyekiti mwenye vision kubwa zaidi. Uwezo wa Mbowe kwa sasa unafikirisha sana.
Wasalaam