Hili la Wachaga kutoajiriwa Serikalini na Taasisi za Umma awamu ya tano, Mbowe anadanganya umma?

Hili la Wachaga kutoajiriwa Serikalini na Taasisi za Umma awamu ya tano, Mbowe anadanganya umma?

Status
Not open for further replies.
Mbowe ni mpumbavu sana. Anapandikiza chuki na ubaguzi. Hili halivumiliki hata kidogo. Wakati hilo linatokea kwa nini asiliseme? Alikuwa wapi?
Ni propaganda ya Kishenzi sana kuwahi kuwapo nchi hii.
 
Sisi hapa kazini (taasisi ya serikali) mwaka juzi tuliajiri watu zaidi ya 130.Watu wa mkoa wa Kilimanjaro walikuwa zaidi ya 40.
Wachaga hata walimu na watumishi wa afya huwa ni wengi zaidi kwa sababu ndiyo waliosoma kwa wingi.
 
Nenda TRA Arusha wachaga watupu,wanaubaguzi sana hawa jamaa,zamani nijua Wahaya lakini nilipokaa Arusha ndo nakaona hawa ni kiboko.
hapo ndo nilielewa na maana ya chasaka.
 
Nenda TRA Arusha wachaga watupu,wanaubaguzi sana hawa jamaa,zamani nijua Wahaya lakini nilipokaa Arusha ndo nakaona hawa ni kiboko.
hapo ndo nilielewa na maana ya chasaka.
Chasaka ni nini ?
 
Uwe unajiongeza..Huyo ni wa awamu ya sita..anachosema mtoa mada ni awamu ya tano.
Awamu ya tano si alikuwa mtendaji mkuu wa wizara ya Utalii na maliasili? Ama hujui alikotokea? Unadhani nani alimtoa huko chuoni alikokuwa anafundisha kama sio Magufuli. Na hata uwaziri huu alionao sasa kapewa na Magufuli..Samia alipoingia akaendelea kumuacha na uwaziri wake...hujui lakini unajifanya wajua
 
Siyo vema sana kuongelea mambo ya ukabila hapa Tanzania, lakini kwa hakika vitendo vya Rais Magufuli vinatulazimisha tuingie huko.

Magufuli alikuwa very clear katika chuki yake dhidi ya Wachagga. Unaweza kuelewa chuki yake kwa kiasi fulani. Nyerere alikutana na "The Chagga Problem" katika elimu. Kutokana na uchagani kuwepo shule nyingi za msingi, Wachagga wengi zaidi walikuwa wakiingia sekondari kuliko makabila mengine. Hili lilikuwa bomu. Nyerere akaja na solution. Quota system. Idadi maalum ikagawanywa kila mkoa, ili kutoa fursa sawa kwa mikoa yote, hata kama inamaanisha kuna vijana wa kichaga waliofaulu vizuri wataachwa ili kuchukua wa mikoa mingine wenye ufaulu wa chini.

Nyerere alifanya haya bila chuki yoyote dhidi ya Wachagga.

Magu ni tofauti. Alibomoa Kimara kwa ukatili usio na kipimo, akijua wamejaa Wachagga, wakati kule Mwanza alisitisha bomoabomoa, akitangaza bila aibu, mchana kweupe, MSIWABOMOLEE HAWA WALINIPA KURA!!
Magufuli alichukia sana Wachagga. Maeneo mengi kawaondoa, lakini badala yake kajaza wasukuma wengi mno, na kwa hiyo hatatui chochote, bali anatia chumvi nyingi mno kwenye kidonda.

Wakati Nyerere alikuwa anapambana na ukabila, Magu kaurejesha kwa kasi
Kwaiyo Magufuli alibomoa nyumba zilizo katika hifadhi ya Morogoro Road sababu wakiishi wachaga?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuliongelea swala la chuki za magufuli dhidi ya wachaga na hata wahaya nimewasikia wakilalamika kuchukiwa na magufuli haliwezi kuwa relevant kwa sasa kwani ameshafariki, labda kama una hoja kwamba wachaga wanachukiwa na kila rais atakayekuja na serikali nzima..
Hii hoja ya kwamba haifai kuongelea ishu za Magufuli kwa sababu tu amefariki, ni sumu tunalishwa. Magufuli aligombea urais kwa hiari yake. Alibeba majukumu ya kitaifa. Anawajibika kwa wananchi. Historia inatuwezesha kujifunza kutokana na yaliyotendwa zamani.

Kuna rafiki yangu tulikuwa tunabishana sana kuhusu Magufuli, mimi nikimpinga Magufuli na sera zake.
Alipofariki, huyu rafiki yangu hakuwa tayari tumjadili kwa hoja kwamba mazishi yafanyike kwanza. Ikabidi nikubali ili kuonyesha heshima kwa marehemu. Cha ajabu, baada ya siku kadhaa kupita, nilipojaribu kuleta hoja zangu dhidi ya Magufuli, hasa ilipodhihirika maeneo nilikuwa sahihi, rafiki yangu akasema siyo vizuri kumjadili marehemu, kwa hoja eti hawezi kujibu mashambulizi!! Yaani utadhani wakati akiwa hai, Magufuli alikuwa akijibu mashambulizi yangu!

Sababu ni wazi. Mashabiki wa Magufuli wanatafuta pa kujificha. Hawana hoja
 
Namnukuu Mbowe

''Miaka mitano ya Hayati Magufuli ilikuwa ni miaka ya mateso kwa watu wa Kaskazini hususan Wachaga, ilifika wakati Magufuli akatoa maagizo ya Wachaga kutoajiriwa Serikalini na kwenye Taasisi za Umma''

Huu ni ukweli mtupu Hayati alikuwa na mabaya yake mengi. Kaulize wachagga sio wakina Sabaya . Tatizo zuluma zina mwisho hata ukijiona wewe ni Mungu yule Mungu wa kweli anarekebisha huo ndiyo ukweli.
 
Kwakweli inasikitisha sana kwa hii kauli ya Mbowe ukizingatia wadhifa wake na heshima yake aliyonayo ktk nchi yetu

Inadhihirisha wazi sasa kwamba ajenda kuu iliyo chini ya kapeti ya chama chake ni kutetea watu wa kabila lake pekee, pengine kwa mbaaali anajifichia ktk ukanda wa kaskazini ili kupata back-up ya makabila yaliyo kanda ya kaskazini

Lakini pia ingekuwa vyema Mbowe akatueleza ni kwann anahisi Hayati JPM aliwachukia!??
Je ni ile propaganda iliyopo nchini kwamba Wachaga ni WEZI na wapiga dili ndio maana Magu ktk safisha safisha ikatokea automatic waathirika wengi wakawa ni wa kabila la wachaga!??

Pia, Mbowe anatueleza kuwa chama chao siku zote ni kuangalia wachaga wangapi wamepata teuzi/ ajira au kutenguliwa Serikalini,,,, Je tukisema yeye ndie MKABILA tutakuwa tunakosea!??

Je na sisi wa makabila mengine let say Wakinga tuanzishe vyama vyetu vya siasa kufatilia ni WAKINGA wangapi wanaopataga ajira/teuzi Serikalini!??

Mwisho kabisa naomba Rais wetu Mamá Samia agiza vyombo vya ulinzi na usalama kumkamata huyu kichwa maji Mbowe, kwani kwa kauli yake na kama anaendelea kuisema basi ni wazi inaleta na italeta mgawanyiko mkubwa nchini, italeta chuki ya kikabila.

Watu kama hawa kina Mbowe hawafai kuendelea kuexist kwa namna yoyote,,,NI HATARI KWA AFYA YA NCHI
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom