benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Ni muda kidogo sasa tangu kutekelezwa kwa agizo la kuwaondoa Wamachinga maeneo ya katikati mwa majiji na miji mikubwa kama Dar es Salaam, Mwanza na Arusha kwa lengo la kuwapanga vizuri lakini pia kuyaweka maeneo hayo katika hali ya usafi.
Habari mbaya ni kwamba katika maeneo mengi wafanyabiashara hao wamesharejea na wanafanya biashara kama zamani tu. Maeneo ya stendi, chini ya mti, Kilombero n.k jijini Arusha, Dar maeneo karibu yote kuanzia Mwenge hadi Kariakoo, Mwanza nako maeneo ya katikati ya Jiji hali ni kama zamani tu.
Maeneo yote haya yana viongozi lakini kama kawaidia wanafanya kazi kwa mazoea, wanasubiri kufanya kazi kwa zimamoto, wanasubiri ziara ya Rais ikaribie ndipo wafanye majukumu yao.
Hawa ni viongozi mzigo, wanaopaswa kujitafakari na kujipima.