Hili la wamachinga kurudi kwenye maeneo waliyoondolewa, wasaidizi wa Rais Samia wajitafakari sana

Hili la wamachinga kurudi kwenye maeneo waliyoondolewa, wasaidizi wa Rais Samia wajitafakari sana

Mission ikifeli mnasingizia wasaidizi wa Rais lakini mission iki-tick mnaanza kusema mama anaupiga mwingi, kimsingi itoshe kusema kwamba wasaidizi wa Rais wana utu na wanatamani machinga waondoke lakini watawapeleka wapi kwa mara moja.

Na Rais ametoa agizo huku kura zao anazitamani maana wasaidizi wake (watendaji wa serikali) wakitekeleza agizo kwa kuweka mgambo na kuwaondoa, anarudi tena muwaondoe kwa staha bila kuwabudhi (how kwa kundi kubwa limekaa sehemu uliondoe bila bughudha)

Wameona watulie tu maana hali ya machinga ni tete maana huwezi kuwaondoa mara moja na kuwapeleka eneo lingine
 
Mwamba alipowaambia walipe 20,000 wapewe vitambulisho mkamuona hamnazo, wakaja wenye nazo, wakasema watoke wanachafua miji, mkasema ni kweli, ila hamkuishia hapo, mkaamua na kutukana yaliyofanyika nyuma kuwa vitambulisho sijui nini!

Yamewashinda sasa, mtuambie nini kinachofuata; hamkawii kutuambia mama ana huruma, kawaachia kwa kuwa vita imetikisa chumi zote za dunia
 
Back
Top Bottom