Hili la wamachinga kurudi kwenye maeneo waliyoondolewa, wasaidizi wa Rais Samia wajitafakari sana

Njia pekee ni kuufanya uchumi wetu usizalishe wamchinga, bodaboda na mama ntilie wanaouza vyakula kwenye ndoo kwa mwendokasi.
 
Wewe na sisi tunawaona wamerudi, lakini ukimuuliza mkuu wa mkoa wa Dar atakuambia wamefanikiwa kuwaondoa na hawatarudi.

CCM hili la wamachinga limewashinda je, wataweza kuikwamua nchi kwenye umasikini?
 
Yote unayoyasema siyapingi na hayo ndio matokeo chanya ya ukuaji wa miji na mipango ya maendeleo, kuna watu au kundi la watu wataumia tu, haikwepeki.
 
VIATU VIKUBWA SANA KWAKE
 
Mpaka sasa inaonesha serikali zote zilizopita na iliyokuwepo,wameshindwa kuwa tafutia suluhishi la kudumu hawa wamachinga

Ova
 
Kwa huu utitiri wa tozo...
Unataka wakaze kila kona.
Hakika itakua wanatengeneza bomu la kujitakia.

Watu wana chuki,hasira na makasiriko.
Kitaumana.
Time will tell
 
machinga wanaongezeka kila uchwao hilo ni swala mtambuka,siku hii nchi pakiwa na mazingira mazuri kwenye ajira,kilimo na ufugaji,viwanda vikubwa na vidogo,kupunguza utitiri wa kodi n.k itachochea kupunguza utitiri wa machinga.
Hapa ndo PA kutibiwa. Yani tatizo mikakati inakata matawi na shina. Mzizi sehem hizo, ambaz hazipokei mabadiliko. Ndo mambo yanastawi upya
 
Na sisi tuache kununua vitu vyao, tununue kwenye maeneo rasmi yaliyotemgwa na mamlaka ya miji.
Mkuu, tatizo huu mikakati pia una eksikyuzi. Usiku wanaruhusiwa, hawa wa usiku wanaanzaga jioni saa 10.siku nyingine wanawahi wanakuja saa 9,mara nane, Mara 5 ndo wanarudi hivyo
 
Hapa ndipo serikali inapofeli sana kukusanya kodi, inapoteza mabilion kila mwaka kuwachekea hao machinga,
Ingekua mimi raisi hakuna kiumbe anaitwa machinga tz angekaa mtaan bali sokoni tu.

Umachinga unafunza wafanyabiashara chipukizi kukwepa kodi sana.
 
Sawa kabla ruksa ya magu mlikua wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…