Hili la watu (wakiwemo viongozi) kudhalilishwa na Watanzania kufurahia linanishangaza sana

Hili la watu (wakiwemo viongozi) kudhalilishwa na Watanzania kufurahia linanishangaza sana

Anapotukwa rais ni kuitukana nchi. Ni kuishushia heshima nchi. Baba au mama yako anapokosea kuna namna ya kusema naye na akaelewa.
NB: Si kila unachoshindwa kutafsiri kutoka kwa mtu itakuwa inamaana amekosea kwa kuwa kiongozi hawezi kuwa anaona kama wanavyoona wanaoongozwa. Nikiwa na maana ya kwamba kiongozi ni lazima atangulie miaka kadhaa mbele ndipo anaitwa kiongozi. Kuna vitu utakuja kuelewa baadaye kwamba vilikuwa ni vya muhimu kama kiongozi alivyona. (UKISOMA HABARI ZA FARAO NA NDOTO YA MIAKA SABA YA NJAA NA KILICHOTOKEA KWA WANANCHI KWA KUTOELEWA WALICHOAMBIWA KWA KUWA HABARI ZA NJAA ZILITOLEWA WAKATI WAPO KWENYE MAVUNO)
inategemea na aina ya kiongozi.
anyway, hata huo mfano ulioutoa, aliyeona si Farao, bali Yusufu ambaye aliletwa mbele ya Farao toka gerezani alikokuwa anatumikia kifungo.
 
Kipindi kile anatukanwa Magufuli na watu mbalimbali tulikuwa tunashangilia sana hasa sisi upande huu wa mkono wa kushoto katika mwili huu mmoja. Nilisema hatupo salama. What goes around comes around.

Waliwezeshwa sana watu wadumu kila siku kumtukana Magufuli. Mimi nyuzi zangu zipo humu. Kuna maamuzi kadhaa ya Magufuli nliyapinga. Kwa hoja. Sikuwa namtukana.

Hawa hawa watu ndiyo ambao sasa wamegeuka wanamtukana Rais aliyepo madarakani. Na anakaa nao mezani anacheka nao. Kama tu ilivyokuwa mwanzo na hata sasa ndivyo ambavyo itakuwa.

Huwa nawaza hicho kisichana kimangi kimekuzwa na nani? Kinachofanya ni ushenzi wa hali ya juu. Mliokuwa mkishangilia wakati anatukanwa Magufuli sasa mnaanza kuona unapomfuga chatu.

Yeye kumtukana Rais haiiniumizi kichwa. Inaniumiza kichwa kuwa ana wafuasi. Ana mashabiki. Hapo ndo naona tatizo la watanzania. Wengi hawna akili. Wengi hawajielewi. Mimi jana mtu wa karibu nami alinitaka nisome yale matusi akichekelea. Nilimwambia hana akili. Huwezi furahia mwanamke, rais anatukanwa vile. Hata kama unapishana naye kiitikadi. Si sawa.

Uhuru una mipaka. Hakuna uhuru usio na mipaka. Labda ukiwa kaburini tu. Duniani kila kitu kina mipaka. Mangi athibitishe maneno yake.
Wao, wametudhalilisha kwa, kutufanya maskini kwa, kuibq pesa zetu, kwanini tusiwatukane?
 
..Magufuli naye alikuwa na genge lake la watukanaji.

..Nakumbuka Maalim Seif aliitwa shoga na gazeti moja, na Msemaji Mkuu wa serikali Gerson Msigwa akatetea matusi hayo.

..Nashauri Rais avumilie tu matusi na kuonyesha ukomavu.

..Wapinzani wametukanwa matusi makubwa makubwa na hakuna aliyekufa kwa kutukanwa.
 
Mbona unakuwa mkali?

Ukiua kwa upanga nawe utauwawa kwa upanga

Mlitukana magufuli kila aina ya maneno hamkujua maana ya karma

Huu ni mwanzo mtalipa dhuluma zote
January ana sababu gani ya kumlipa amtukane mtu ambaye amemrudisha kwenye uongozi? Mange mwenyewe amemtukana sana January enzi za JK hadi urafiki wa Mwamvita na huyo dada ukafa.

Toa sababu moja inayokufanya ufikirie january anaweza kuwa ndiye anamtuma afanye hivyo.

Sioni sababu kwa sababu inaelekea hana shida na maza na maza ni mtu wa karibu wa January na Mzee wake kiasi kwamba miezi miwili nyuma alienda kwa Mzee Makamba wazo hapo kumtembelea na hii inaonyesha jinsi gani walivyo karibu.
 
Mbona unakuwa mkali?

Ukiua kwa upanga nawe utauwawa kwa upanga

Mlitukana magufuli kila aina ya maneno hamkujua maana ya karma

Huu ni mwanzo mtalipa dhuluma zote
Mkali kwa lipi? Soma mtililiko wangu. Nimesema huyu mtu wanayesema katumwa na January ameanza kutukana toka enzi za JK, tena alimtukana sana huyo January, ikaja enzi za JPM alianza anamsifu baadaye akaanza mtukana, same to Samia. Sasa kwanini wasema anatumwa na January...
 
January ana sababu gani ya kumlipa amtukane mtu ambaye amemrudisha kwenye uongozi? Mange mwenyewe amemtukana sana January enzi za JK hadi urafiki wa Mwamvita na huyo dada ukafa.

Toa sababu moja inayokufanya ufikirie january anaweza kuwa ndiye anamtuma afanye hivyo.

Sioni sababu kwa sababu inaelekea hana shida na maza na maza ni mtu wa karibu wa January na Mzee wake kiasi kwamba miezi miwili nyuma alienda kwa Mzee Makamba wazo hapo kumtembelea na hii inaonyesha jinsi gani walivyo karibu.
ni ww ndiye usieona sababu na siasa haingoji sababu kuwa karibu na familia sio kigezo cha kukubalika......
 
Wewe akili yako ndogo

Mange ni ukurasa unaotumiwa na wanasiasa wenye nia mbaya na hii nchi toka kipindi cha magufuli

Nenda kajadili mapenzi uwezo wako mdogo
Hakuna anayemtuma... wewe ndiye hufuatilii yule hajaanza kutukana serikali enzi za magufuli ni vile JK enzi zake kulikuwa hakuna machawa wa kufuatilia na kutoa matamko kama haya. Mange kaanza kutukana toka enzi za JK. Sema tofauti za enzi za JK na sasa hakukuwa na uchawa wa kila mtu kutoa tamko kama zama za JPM na za Mama Samia. Mfano issue ya kumtukana JK ze utam ingetokea zama hizi basi kelele zingekuwa hivi hivi.
 
Kipindi cha kikwete mange alikuwa yupo karibu sana na serkali

Mange alichukua hadi fomu ya kugombea ubunge wa wanawake
Hizi zote ni consipiracy shida ni kwamba watu mmeanza lalamika zama hizi. Na kipindi cha Kikwete je alikuwa analipwa na nani. Maana hakuna awamu amabayo hajaishambulia labda ya Mkapa na akina mwinyi kwa sababu alikuwa mdogo na mitandao haikuwepo.
Awamu ya Magufuli ilianza anamsifia, baadaye akaanza kumshambulia. Same hata hii awamu. Same awamu ya Kikwete.
Wewe unayeelewa hebu tuambie kigogo ni nani na mbona kama mnafahamu hadi leo mmeshindwa kumkamata na abdo anaendelea mashambulizi. Mlianza mara January, ikaenda mkaanza mara nape yani kigogo ashakuwa watu mbalimbali.
 
ni ww ndiye usieona sababu na siasa haingoji sababu kuwa karibu na familia sio kigezo cha kukubalika......
Lete sababu maana January Samia sio mshindani wake maana ni dhahiri lazima Samia amalize awamu zake unless labda angekuwa anatukanwa Mwigulu au mtu ambaye inasemekana anautaka urais baada ya Samia ungesema January kaanza kumchafua. Sasa amtukane samia kwa lipi wakati hata fomu ya kugombea 2025 hatoichukua...
Lete connection kwanini unahisi afanye hivyo.
 
Kipindi cha kikwete mange alikuwa yupo karibu sana na serkali

Mange alichukua hadi fomu ya kugombea ubunge wa wanawake
Alikuwa karibu wapi na serikali bwana wakati alikuwa anamtukana JK, na Rizwani na huyo January Makamba. Fomu ya kugombea alichukua lakini wakamkatilia mbali. Enzi za JK alikuwa hadeal na watu kwa nguvu kubwa kama hivi la sivyo alipotua tz angeipata pata. By the way bado pia aliondoka TZ faster hata yeye anakili alianza kuogopa juu ya uhai wake. Huyu mtu zama zote anatukana sema serikali ya Kikwete ilikuwa haifuatilii sana yaliyokuwa yanaendelea kwenye mtandao wala hakukwua na mawaziri wala wakuu wa mikoa machawa wa kusema atakaye msema JK tutakufa naye kama sasa na enzi za JPM
 
Ogopa sana

Usimtende

mabaya mtu asiye kuwa na hatia

Kina February walitumia ukurasa wa mange kumdhalilisha mzee wa watu Magufuli

Lkn

Karma is real...
Sikuona hizi nyuzi awamu ya 5 JPM alipokuwa akitukanwa

Sasa mkae kwa kutulia sindano ziwaingie

What comes around goes around

Mbona inasemakana hata baadhi ya siri za Ikulu yeye ndio alikuwa anavujisha????wacha KARMA imtafune

Muoshwa huoshwa muda wake sasa umefika hana wa kumlaumu atubu kwa muumba wake periodView attachment 2962351
 
Back
Top Bottom