Huu ndiyo upumbavu wa baba Mwajuma. Mpaka uwe mkulima ndiyo unajua mambo ya kilimo. Jina lako linasadifu asili yako (uvivu + kubweteka). Arusha na Kilimanjaro inastawi. Sehemu zote za baridi inastawi. BTW ni kitu gani tumeweza kulima na tukajitosheleza? Mchele wenyewe tumeshindwa. Narudia tena. Asili yako ni uvivu na kubweteka bila kusahau maneno mengi.
So hoja umeshindwa unaanza personal Attack?
Nimekaa Kilimanjaro nimesoma Kilimanjaro huko ambapo Ngano inastawi, sijawahi kuona Ardhi isiotumika, hakuna Ardhi ambayo imekaa kiboya boya ukalime ngano.
Wanacholima huko ni kahawa na mazao yanayofanania, kahawa ina bei, Kahawa nzuri inaenda kilo zaidi ya 10,000 hizi bei toka bodi ya kahawa
At minimum 4000 at maximum 11,000
Then una ngano ambayo inauzwa kilo 1400-1500
Je ungefanyaje?
1. Ungeacha kulima kahawa ya bei uka panda ngano isio na issue kumfurahisha Bakhresa.
2. Ungelima kahawa yenye Bei upate hela nyingi zaidi na kununua Ngano ya bei rahisi.
Pia Nchi hii kuna vitu kibao tunalima na kujitosheleza, fuatilieni mambo acheni kushinda JF na kuongea mipasho kila siku.
Nimewahi ongelea pamba humu kitu ambacho nina uzoefu nacho pia.
1. Tunazalisha pamba kwa wingi sana kutosheleza soko la Ndani hadi kuuza nje.
2. Tunawatengenezea Jeans Wamarekani Levis na Wrangler
3. Viwanda Vya Metl pekee ambavyo hutumia Pamba ya ndani vinazalisha Zaidi ya Mita milioni 100 kwa mwaka
4. Tuna viwanda vya nyuzi vya jambo etc
5. Viwanda vingine kama Nida, vya Arusha etc
So msikae mkafikiri hawa Mamilionea wetu, mabilionea, Serikali etc ni wajinga wajinga tu kwamba wewe no name humu unajua zaidi ila wao ni clueless hupati Bilioni 900 ama matrilioni ya hela bila kuwa na watu smart ambao soko la dunia lipo kiganjani wanalijua ndani nje.