Hili ni jambo la mafanikio kwa nchi pia au kwa kampuni binafsi tu?

haha halafu kwenye paket ataandika made in tanzagiza hata juice zake hivyo hivyo anaimport concentrate na kuandika made in tanzagiza, fikiria meli imetoka australia wakati manyara tunalima ngano nafikiri hata tbl ya makaburu walijaribu kuwekeza huko sababu ya kubrew bia, utapeli mtupu huyo fake investor …
 
Bakhresa wanataka reliability of supplies na wakulima wetu sio reliable wameona isiwe kesi wameagiza nje
 
Mkuu wala hamna shida ni Kama unavyoona Asas anaagiza maziwa Rwanda na Kenya.

Sisi ni wazee wa substance tunapambania tumbo na sio kukuza uchumi
Inasikitisha sana.
 
Halafu kuna watu fulani sijui chawa wanasema serikili ya mama imewezesha wizara ya kilimo kiasi cha kuiuzia afrika na dunia chakula!
 
Tunaweza uchawa na siasa za majitaka TU!
 
Mimi siyo mkulima. Huko ngano inakotoka wana seriakli zenye viongozi wenye akili na siyo hawa wanakwenda kufanya utapeli kwa Mwamposa, tapeli mwenzao. Chuo kikuu cha Sokoine kinaweza kufanya makubwa kwa vitendo. Wajinga nini.
Sasa kama sio mkulima unaongeaje vitu usivyovijua, kesho na keshokutwa mtaanza kulalamika kwanini Serikali yetu haijaleta snow,

Ngano ina hali ya hewa maalum ili ilimike vizuri, unahitaji hali ya hewa ya baridi hadi nyuzi 14 ambazo ni maeneo machache nchi hii inaweza kulimwa, Africa nzima Sehemu chache sana wanalima Ngano, labda uikute Moshi huko na hawawezi waste maeneo yao Kulima ngano wakati kuna mazao ambayo ni profitable zaidi.
 
Nani kakuambia Tanzania ina maeneo machache ya hali ya hewa ya baridi hadi ya nyuzi 14?
Unajua wakoloni wamelima ngano sana Tanganyika na waliacha mashamba makubwa tu ya ngano wakati wanaondoka??
 
Hakuna mafanikio yeyote hapa. Ngano hii tulipaswa kuilima sisi wenyewe, halafu SSB aje kuinunua kwa wakulima wetu wa ndani, hiyo ndiyo dhana ya kujitegemea kiuchumi. Lakini juzi nimesikia Wasafi Media, wale wazee wakipiga kelele wakimsifia DP na kuimba sifa za DP World. Nikajiuliza, Hawa wazee wana matatizo ya kiakili, au njaa na uchawa vimewageuza kuwa mawakala wa kuuza nchi kwa maneno matamu?
 
Huu ndiyo upumbavu wa baba Mwajuma. Mpaka uwe mkulima ndiyo unajua mambo ya kilimo. Jina lako linasadifu asili yako (uvivu + kubweteka). Arusha na Kilimanjaro inastawi. Sehemu zote za baridi inastawi. BTW ni kitu gani tumeweza kulima na tukajitosheleza? Mchele wenyewe tumeshindwa. Narudia tena. Asili yako ni uvivu na kubweteka bila kusahau maneno mengi.
 
Hao wazee wa wasafi ni wahuni tu wachumia tumbo wanaoishi kwa bahasha na uchawa zaidi.
 
So hoja umeshindwa unaanza personal Attack?

Nimekaa Kilimanjaro nimesoma Kilimanjaro huko ambapo Ngano inastawi, sijawahi kuona Ardhi isiotumika, hakuna Ardhi ambayo imekaa kiboya boya ukalime ngano.

Wanacholima huko ni kahawa na mazao yanayofanania, kahawa ina bei, Kahawa nzuri inaenda kilo zaidi ya 10,000 hizi bei toka bodi ya kahawa


At minimum 4000 at maximum 11,000

Then una ngano ambayo inauzwa kilo 1400-1500

Je ungefanyaje?
1. Ungeacha kulima kahawa ya bei uka panda ngano isio na issue kumfurahisha Bakhresa.

2. Ungelima kahawa yenye Bei upate hela nyingi zaidi na kununua Ngano ya bei rahisi.

Pia Nchi hii kuna vitu kibao tunalima na kujitosheleza, fuatilieni mambo acheni kushinda JF na kuongea mipasho kila siku.

Nimewahi ongelea pamba humu kitu ambacho nina uzoefu nacho pia.
1. Tunazalisha pamba kwa wingi sana kutosheleza soko la Ndani hadi kuuza nje.

2. Tunawatengenezea Jeans Wamarekani Levis na Wrangler

3. Viwanda Vya Metl pekee ambavyo hutumia Pamba ya ndani vinazalisha Zaidi ya Mita milioni 100 kwa mwaka

4. Tuna viwanda vya nyuzi vya jambo etc

5. Viwanda vingine kama Nida, vya Arusha etc

So msikae mkafikiri hawa Mamilionea wetu, mabilionea, Serikali etc ni wajinga wajinga tu kwamba wewe no name humu unajua zaidi ila wao ni clueless hupati Bilioni 900 ama matrilioni ya hela bila kuwa na watu smart ambao soko la dunia lipo kiganjani wanalijua ndani nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…