Historia moja imebaki intact; hakuna Rais aliyefanikiwa kurithisha kiti cha Urais kwa amtakaye

Historia moja imebaki intact; hakuna Rais aliyefanikiwa kurithisha kiti cha Urais kwa amtakaye

Hilo la kufanya hadaa ili tupate misaada mingi kuliko nchi yoyote Afrika siyo jambo la kujivunia, aidha kwa Kikwete mwenyewe, au kwa nchi analiyokuwa akiiongoza.

Kupewa misaada ni ishara ya udhaifu, na ni udhaifu kwa unayepewa msaada.
Kupewa misaada na kukopa Kama Magu lipi la kujivunia?Magu ameingia nchi hii tunadaiwa Trillion 36.. anaondoka tunadaiwa Trillion 59 kwa miaka 6 tu, Yeye peke yake kakopa trillion 23..wakati wenzake wanne wamekopa trillion 36 tu. Halaf Mnataka tumsifie kaleta maendeleo!
 
Hivi unamjua kikwete kweli? Kikwete ni mtu wa mwanadiplomasia,unafikiri angesema alikuwa anamtaka Membe pale kwenye msiba?
Isingekuwa lazima kusema hayo, kumbuka Kikwete alimwambia pia Mzee Bilal na Mzee wa nyuki wote wagombee atawapa saport niambie aliwambia kwa nia gani kama si kuwapoteza maboya [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mzee wa nyuki alianza kutoa nia akiwa UK BBC haa haa haa chezea kijana wa msoga wewe,[emoji23]
 
Kupewa misaada na kukopa Kama Magu lipi la kujivunia. Magu ameingia nchi hii unadaiwa Trillion 36.. anaondoka tunadaiwa Trillion 59 kwa miaka 6 tu Yeye peke yake kakopa trillion 23..wakati wenzake wanne wamekopa trillion 36 tu
Nyie msichoelewa ni nini? Hivi nyie waafrika nani aliyewaloga?

Ni hivi humu duniani hakuna cha bure. Huo mnaouita msaada wanaowapa "msaada" ni watu strategic sana. Kwa kila shilingi moja watakayokupa wanachukua shilingi kumi. Bill Gate anasema "use millions to get billions". Ushawahi kujiuliza kwa nini nchi yenye msimamo wa kujitegemea hupigwa vita na wale wanaotoa "misaada"? Kama hujui misaada inalemaza akili, na wale jamaa wanapenda nchi zetu ziongozwe na viongozi mburula watembeza bakuli, badala ya kujitegemea.
 
Kikwete mtot wa mjini uyo ila namkubali san mzee wang nmemiss enzi za utawala wake
 
Nyie msichoelewa ni nini? Hivi nyie waafrika nani aliyewaloga?

Ni hivi humu duniani hakuna cha bure. Huo mnaouita msaada wanaowapa "msaada" ni watu strategic sana. Kwa kila shilingi moja watakayokupa wanachukua shilingi kumi. Bill Gate anasema "use millions to get billions". Ushawahi kujiuliza kwa nini nchi yenye msimamo wa kujitegemea hupigwa vita na wale wanaotoa "misaada"? Kama hujui misaada inalemaza akili, na wale jamaa wanapenda nchi zetu ziongozwe na viongozi mburula watembeza bakuli, badala ya kujitegemea.
Kwahiyo kukopa ndo akili?
 
Magu alikuwa bonge moja la chawa. Alikuwa anamsifu mnoooo Kikwete.

Alikuwa vizuri sana kwenye usimamizi, kosa walilolifanya ni kumpa mamlaka ya maamuzi. Hapo tu.

Magu alipaswa kusimamiwa.
Hii ya kumsifu Kikwete kupita kiasi ilikuwa ni stratergy yake kubwa ya kumfanya Kikwete amuamini, na kweli ilimlipa!
 
Halaf Kikwete alivyokuwa mjanja alitaka kuwaambia sio kweli barabara za kuunganisha mikoa zilijengwa kipindi cha Magu.. akasema yeye ndo aliacha legacy ya kujenga barabara zote za kuunganisha mikoa,kasoro ya Kigoma na Katavi. Kazi kwa wale Walikuwa wanaita Magu ndo kajenga barabara zote za nchi hii
JK mzee wa kunyoosha mambo
Alitumia dakika zake chache kulinda legacy yake ambayo MATAGA walijaribu kuiiba au kuipoteza kimkakati ili kumuinua Magufuli
 
Katika historia ya Tz, jambo moja limekuwa linatokea mara kwa mara.

Rais aliyekuwepo madarakani kushindwa kumuweka anaemtaka anapoondoka.

Wengi walihisi Magufuli atatuwekea mtu wake akimaliza mda wake but haikutokea.

Nyerere alimtaka Salim, akatokea Mwinyi.

Mwinyi akamtaka Malecela, akaibuka Mkapa.

Mkapa akamtaka Kigoda, akashindwa na mtandao wa Kikwete.

Kikwete akamtaka Membe, akaibuka Magufuli.

Magufuli hatujui alikuwa na nani kampanga kichwani mwake Ila now tuna Samia.

Nna uhakika hata chaguo la Samia halitapita; ataibuka mwingine dakika za mwisho.

Hii ndo Tanzania. Ukipanga hivi the 'ancestors' wanapangua.
Magufuri kamuweka Hussein Mwinyi ZNZ usisahau !!!
 
Back
Top Bottom