Last emperor
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 10,346
- 9,892
Kupewa misaada na kukopa Kama Magu lipi la kujivunia?Magu ameingia nchi hii tunadaiwa Trillion 36.. anaondoka tunadaiwa Trillion 59 kwa miaka 6 tu, Yeye peke yake kakopa trillion 23..wakati wenzake wanne wamekopa trillion 36 tu. Halaf Mnataka tumsifie kaleta maendeleo!Hilo la kufanya hadaa ili tupate misaada mingi kuliko nchi yoyote Afrika siyo jambo la kujivunia, aidha kwa Kikwete mwenyewe, au kwa nchi analiyokuwa akiiongoza.
Kupewa misaada ni ishara ya udhaifu, na ni udhaifu kwa unayepewa msaada.
Isingekuwa lazima kusema hayo, kumbuka Kikwete alimwambia pia Mzee Bilal na Mzee wa nyuki wote wagombee atawapa saport niambie aliwambia kwa nia gani kama si kuwapoteza maboya [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mzee wa nyuki alianza kutoa nia akiwa UK BBC haa haa haa chezea kijana wa msoga wewe,[emoji23]Hivi unamjua kikwete kweli? Kikwete ni mtu wa mwanadiplomasia,unafikiri angesema alikuwa anamtaka Membe pale kwenye msiba?
Haaa haaa kwahiyo ni Mzee wa chenga na penalty!Jk mwongo huyo.Hayati Mugabe aliwahi kusema story za JK akienda kwake anaongea tofauti na akienda kwa wazungu.
Nyie msichoelewa ni nini? Hivi nyie waafrika nani aliyewaloga?Kupewa misaada na kukopa Kama Magu lipi la kujivunia. Magu ameingia nchi hii unadaiwa Trillion 36.. anaondoka tunadaiwa Trillion 59 kwa miaka 6 tu Yeye peke yake kakopa trillion 23..wakati wenzake wanne wamekopa trillion 36 tu
Kwahiyo kukopa ndo akili?Nyie msichoelewa ni nini? Hivi nyie waafrika nani aliyewaloga?
Ni hivi humu duniani hakuna cha bure. Huo mnaouita msaada wanaowapa "msaada" ni watu strategic sana. Kwa kila shilingi moja watakayokupa wanachukua shilingi kumi. Bill Gate anasema "use millions to get billions". Ushawahi kujiuliza kwa nini nchi yenye msimamo wa kujitegemea hupigwa vita na wale wanaotoa "misaada"? Kama hujui misaada inalemaza akili, na wale jamaa wanapenda nchi zetu ziongozwe na viongozi mburula watembeza bakuli, badala ya kujitegemea.
Maneno ya mkosaji. Hata watoto walijua nani alikua Chaguo la JK na genge lake.Kikwete amesema jana kuwa yeye alimtaka Magufuli akamuweka namba moja.
Bwashee mbona una kichwa kigumu wewe?!
Sio miaka muwili, ILIKUWA nadhani mwanzo ni mwa awamu ya pili ya JK.Magu alishachaguliwa na system kumrithi JK miaka miwili kabla ya JK kustaafu.
Utafiti wa ndani wa TISS ulishaonyesha kuwa wananchi wanamkubali Magufuli kumrithi JK
Yaani nadhani kati ya watu wanaojuta kumfahamu JK ni Lowasa.Hawamjui JK alivyo..
Ndo maana hata Lowasa aliamini JK hawezi mzuia kuingia IKulu...
JK ana Sura nyingi sana
Mungu aliruhusuHakushindwa kuzuia Idi Amini Dada kuwa rais au?
Mbona sasa alikuwa rais wa Uganda, tena si kwa demokrasia bali kwa kufanya mapinduzi ya kijeshi?
Jiwe angefanikiwa. Ang-bulldoze. Ndo sababu kwa kuona hivyo Mungu akampiga counter attack.Magu alishachaguliwa na system kumrithi JK miaka miwili kabla ya JK kustaafu.
Utafiti wa ndani wa TISS ulishaonyesha kuwa wananchi wanamkubali Magufuli kumrithi JK
Kwa mataga hata wakiambiwa jamaa bdo anachapa kazi alipo watakubal tu,wao hawana tofaut na NGUCHIRO
JK hata ukimwangalia Hana huzuni na kifo cha JPM ,maneno na matendo yake hayana uwiano.
Huu msiba umejaa uongo mwingi Sana kuanzia maradhi, kifo NK . Unaonyesha Marehemu alikuwa muumini WA uongo.
Bado tuna safari ndefu sanaElimu ndugu haijatukomboa
Hii ya kumsifu Kikwete kupita kiasi ilikuwa ni stratergy yake kubwa ya kumfanya Kikwete amuamini, na kweli ilimlipa!Magu alikuwa bonge moja la chawa. Alikuwa anamsifu mnoooo Kikwete.
Alikuwa vizuri sana kwenye usimamizi, kosa walilolifanya ni kumpa mamlaka ya maamuzi. Hapo tu.
Magu alipaswa kusimamiwa.
JK mzee wa kunyoosha mamboHalaf Kikwete alivyokuwa mjanja alitaka kuwaambia sio kweli barabara za kuunganisha mikoa zilijengwa kipindi cha Magu.. akasema yeye ndo aliacha legacy ya kujenga barabara zote za kuunganisha mikoa,kasoro ya Kigoma na Katavi. Kazi kwa wale Walikuwa wanaita Magu ndo kajenga barabara zote za nchi hii
🙏 Kumbe na wewe umesanuka!JK mzee wa kunyoosha mambo
Alitumia dakika zake chache kulinda legacy yake ambayo MATAGA walijaribu kuiiba au kuipoteza kimkakati ili kumuinua Magufuli
We ukiwa na shida unaomba msaada kwa wanaume wenzako au unakopa ili arudishe ukipata?Kwahiyo kukopa ndo akili?
Magufuri kamuweka Hussein Mwinyi ZNZ usisahau !!!Katika historia ya Tz, jambo moja limekuwa linatokea mara kwa mara.
Rais aliyekuwepo madarakani kushindwa kumuweka anaemtaka anapoondoka.
Wengi walihisi Magufuli atatuwekea mtu wake akimaliza mda wake but haikutokea.
Nyerere alimtaka Salim, akatokea Mwinyi.
Mwinyi akamtaka Malecela, akaibuka Mkapa.
Mkapa akamtaka Kigoda, akashindwa na mtandao wa Kikwete.
Kikwete akamtaka Membe, akaibuka Magufuli.
Magufuli hatujui alikuwa na nani kampanga kichwani mwake Ila now tuna Samia.
Nna uhakika hata chaguo la Samia halitapita; ataibuka mwingine dakika za mwisho.
Hii ndo Tanzania. Ukipanga hivi the 'ancestors' wanapangua.