tinkanyarwele
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 2,016
- 1,946
Dah, ni historis nzuri ya kupendeza na inavutia sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alizaliwa mwaka gani?Ukifika HOSPITALI YA MUHIMBILI kuna wodi inaitwa Sewahaji. Unamjua Sewahaji alikuwa ni nani??
Sewa Haji Paroo ndio hasa alianzisha hospitali ya Muhimbili. Alifika huku Tanganyika kupitia kisiwa cha Zanzibar akitokea katika mji wa Bhuj.
Sewahaji alikuwa ni mfanyabiashara, na alikuja Afrika Mashariki kutafta Maisha. Mwaka 1852 aliamua kufungua Duka la bidhaa mbalimbali kwenye visiwa vya Zanzibar.
Biashara ilikuwa kubwa zaidi, Hivyo mwaka 1860 alifungua Duka Lingine Kubwa
Bagamoyo, kisha akaamua kuweka Makazi yake.
Biashara zake ikawa kubwa mno, hivyo Sewahaji akawa ni mmoja kati ya matajiri wakubwa.
Alisaidia Watu wote bila kujali Rangi, Dini wala Kabila zao. Alinunua Majengo kadhaa na kuyafanya Makazi Watu wasiojiweza na wasio na makazi waliokimbilia mzizima.
Alijenga shule za msingi na Hospitali kadhaa katika Mji Wa Mzizima { Leo ni Dar es Salaam}.
Alijenga Hospitali akaiita Sewahaji Hospital ikawa inatoa Huduma bure kwa walalahoi wa Mzizima.
Mnamo Februari, 1897 Sheikh Sewa Haji Paroo alifariki Dunia.
Ilikuwa ni Huzuni na Simanzi kubwa wakazi wa Bagamoyo na Mzizima.Aliependwa sana!
Baada ya Kifo chake, Wakoloni wakabadilisha Jina Kutoka "Sewahaji Hospital" na ikaitwa "Princess Magreth Hospital"
Mnamo 1963 Iliitwa Muhimbili Hospital, Na Mojawapo ya Wodi inaitwa SEWA HAJI.
Leo jiulize mchango wako katika kuboresha hali ya watu wengine, Usijiulize kuhusu umaarufu kwani siku moja historia itasema.
Ujenzi mwema wa Taifa Letu.
Wakati utumwa umekwisha duniani 1873 alikuwa na kama miaka 22,kijana wa miaka 22,aliweza kufanya utumwa kivipi,au wataka kutuambia alianza kufanya utumwa akiwa na mwaka mmoja.Tumia akili,usilete habari za kukaririshwa,halafu pia huyu sio muarabu (japo habari ya waarabu kufanya biashara ya utumwa ni ya kutungwa pia)ni muhindi,wahindi hawakushiriki biashara ya utumwa,kwa afrika.Historia nzuri lkn nimesikitika sana maana wengi mmemuelezea Sewa Hadji kimahaba na kuficha baadhi ya mambo msiyopenda tuyajue!
Huyu Bwana alikuwa mfanyabiashara (dalali) mkubwa wa watumwa. Huo mnaoita utajiri aliupata kwa njia hii ya Kikatili. Aliwatesa na kuwanyanyasa sana Babu zetu (Weusi) ili afanikishe lengo lake la kupata utajiri haramu.
Sewa Hadji Hospital aliyoiasisi yeye haikuwa pale ilipo Muhimbili ya leo, Ile Wodi iliyopewa Jina lake ni kwa Heshima tu (Japo Hastahili heshima hiyo) na kutambua mchango wake katika sekta hiyo ya kitabibu.
Wakati utumwa unapigwa marufuku 1873,huyu hazidi miaka 22,kwa hiyo wataka kuniambia alianza hii kazi ana mwaka mmoja wa umri wa kuzaliwa?Halafu huyu sio muarabu(japo waarabu wanasingiziwa na hii biashara,wakati wao wenyewe waarabu wa asili ni watu weusi,hata jina Afrika,lilitokana na mfalme wa kiarabu,aliyekuwako maeneo ya Afrika ya kusini,hawa ndio wakahamia mashariki ya kati na kuoana na wazungu,ndio wakapatikana waarabu hawa unawaona sasa),huyu ni mhindi,hakuna historia inavyoonyesha kama kuna mhindi,aliyeshiriki biashara hii ya utumwa kwa Afrika.Historia nzuri lkn nimesikitika sana maana wengi mmemuelezea Sewa Hadji kimahaba na kuficha baadhi ya mambo msiyopenda tuyajue!
Huyu Bwana alikuwa mfanyabiashara (dalali) mkubwa wa watumwa. Huo mnaoita utajiri aliupata kwa njia hii ya Kikatili. Aliwatesa na kuwanyanyasa sana Babu zetu (Weusi) ili afanikishe lengo lake la kupata utajiri haramu.
Sewa Hadji Hospital aliyoiasisi yeye haikuwa pale ilipo Muhimbili ya leo, Ile Wodi iliyopewa Jina lake ni kwa Heshima tu (Japo Hastahili heshima hiyo) na kutambua mchango wake katika sekta hiyo ya kitabibu.
Darul salaam - City of peace
Mussa Hassani - Msasani.
Muhimbili ni spitali iliojengwa na wazee wetu waliothamini utu na taifa lao. Tanganyika ilikuwa ni taifa la kuheshimika na wazee wetu ndio waliopigania UHURU wa taifa letu.
Baada ya UHURU walioshika hatamu walihakikisha UISLAMU unadhibitiwa kwelikweli.
Wengi wenu ni watu wakuja hapa daresalaam na hata historia hamuijui ndio maana munajisemea maneno ovyo. Nyerere alitaka kuufanya mji mkuu kuwa DODOMA lakini imeshindikana.
Historia haifutiki na itabaki pale pale. Walioijenga nchi hii ni waislamu.
Safi sana mkuu Sky Eclat; Leo umeamua kutumegea a down memory lane. Umeanza na Uzi wa ndoa ya Oscar Kambona na Flora Oriyo kule London. Asante.View attachment 1053135
View attachment 1053136
Sewa Haji Paroo alikuwa tajiri sana katika miaka ya 1851-1897. Alikuwa pia muumuni thabiti wa imani ya Kiislam na aliamnini katikawkusaidia wasiojiweza.
Bwana Sewa Haji, alikuwa mfanya biashara wa nguo, shaba, na banking. Alijenga hospitali ya Sewa Haji ili kuwasaidia wasio na uwezo.
Hospital hii chini ya utawala wa Uingereza ilipanuliwa na ilifunguliwa na mdogo wa Malikia Elizabeth, Princess Margaret na kupewa jina lake.
Baada ya uhuru jina lilibadilika na kuwa Muhimbili lakini kuna wodi ya Sewa Haji.