Historia ya TANU siku zote imeandikwa na makosa

TUlia kalee wajukuu km huna lingine la maana kuichangia nchi hii. Nchi inahitaji kuunganishwa we unataka kuigawa kwa upotoshaji. Vitabu vilivyoandikwa vya historia viko sahihi.
 
TUlia kalee wajukuu km huna lingine la maana kuichangia nchi hii. Nchi inahitaji kuunganishwa we unataka kuigawa kwa upotoshaji. Vitabu vilivyoandikwa vya historia viko sahihi.
Saig...
Tufanye mjadala wa adabu na kuheshimiana.
 
alipigania uhuru kwaajili ya waislamu au kwaajili ya watanzania. kabla ya kuwa muislamu alipozaliwa si alikua mwafrika mtanzania. Unahisi mwingereza kipindi anatawala alikua anatofutisha waaafrika kisa dini au kisa uafrika wao
 
alipigania uhuru kwaajili ya waislamu au kwaajili ya watanzania. kabla ya kuwa muislamu alipozaliwa si alikua mwafrika mtanzania. Unahisi mwingereza kipindi anatawala alikua anatofutisha waaafrika kisa dini au kisa uafrika wao
Ed..
Kulikuwa na ushirkiano mzuri na wa karibu kati ya Wamishionari na serikali za kikoloni kuanzia Wajerumani hadi kuingia kwa ukoloni wa Waingereza.

Ukisoma maisha ya Kleist Sykes katika kitabu alichohariri John Iliffe, "Modern Tanzanians," (1973) anasema kuwa kabla ya wao kuasisi African Association Waafrika walikuwa wanawakilishwa na Father Gibbons kutoka Minaki Mission.

Hii ni katika miaka ya 1920.

Wamishionari wakawa wanawatahadharisha waumini wao kujiweka mbali na shughuli za siasa.

Hii ndiyo sababu ikawa Waislam kuwa wengi katika uasisi wa AA na ikaendelea hadi katika TANU.


Father Gibbons waliosimama wa kwanza kushoto​
 
Mm sikubaliani na maelezo yako ya udini mzee wangu na kumsifia mfanyabiashara dhalimu chotara wa kiarabu Abushiri bin Salim na udhalimu wake wa kuuza binadamu wenzie.
 
Mm sikubaliani na maelezo yako ya udini mzee wangu na kumsifia mfanyabiashara dhalimu chotara wa kiarabu Abushiri bin Salim na udhalimu wake wa kuuza binadamu wenzie.
Nelson...
Lakini Abushiri hakufanya biashara hiyo.

Wala Abushiri hakuwa Mwarabu.
Jifunze historia kwanza ndiyo useme.
 
Ndiyo ishatoka na hairudi hiyo, mzee baba alifanya yake na akasepa huyu Moud afanye yake na yeye.
Today,
Kitabu nilichoandika kinasomwa na kipo katika "ategory" ya "Corrective History."

Kitabu changu hiki ndicho kilichoniingiza katika Cambridge Journal of African History.

Kitabu changu hiki ndicho kilichoniingiza katika Dictionary of African Biography (DAB).

Kitabu changu hiki ndicho kilichonipa ufunguo wa kufungua milango ya vyuo vikuu vingi.

Haya yote sikutegemea.

Kitabu changu hiki ndicho kilichosababisha niwe mmoja wa watu walioshiriki katika kueleza historia ya Julius Nyerere wakati wa utafiti wa kitabu chake, "Nyerere Biography,"(2020).

Mnakesha na mimi hapa.
Mnashindwa kuondoka.

Kitabu miaka 25 toka kichapwe Uingereza 1998 bado kinajadiliwa hadi leo.
Kwa nini?
 
We mzee kila nikisoma mada zako unaelezea wazee wa kiislam. Inamaana wazee wa kikristo hawakuwepo kwenye hizo mambo unazotueleza? Halafu Mara kwa mara unaonyesha chuki za wazi kwa Nyerere, hii ina maana gani kwako?
Ukitaka watu wakuelewe leta historia zisizo na udini. Haiwezekani kila historia unasema imekosewa kisha unaanza kuwaingiza wazee wako wa kiislam. Udini unakufanya uonekane ni mzee wa ovyo sana. Inaonekana hata huko kwenye jamii yako una udini uliopitiliza.

Ukishakuwa mzee inabidi uwe na busara na kuwaunganisha watu sio kuwatenganisha. Umenizidi zaidi ya miaka 40 Ila kwa haya unayoandika kila siku nakuona kama mzee fulani hivi mwenye fikra za kijinga.
 
Uwongo mtupu ili kujusty fundamentalism yake kwenye Islam religion. Ila mze you are finished, dunia ya kistaarabu UDINI hauna nafasi. Hata uandike ujaze makataba ya Taifa kutetea wazazi wako itabakia ni riwaya tu au rumours. Wewe ni nani ubadili historia ya J K Nyerere?
 
Clever...
Ninaposoma mtu kaanza kuandika kwa, ''We mzee...'' najua kaghadhibika.
Lakini nini kinamghadhibisha?

Anasema kuna udini.
Udini kuandika historia ya kweli na kuwataja wahusika wa historia hiyo?

Ndiyo kusema wale walioandika historia ya TANU na kufuta majina ya Waislam katika historia ya kupigania uhuru walifanya hivyo kwa kuogopa udini ikiwa majina ya wazalendo Waislam yatatawala historia ya uhuru?

Umeuliza wazee wa Kikristo hawakuwapo?
Wakristo walikuwapo.

African Association iliasisiwa mwaka wa 1929 na waasisi ni hawa: Cecil Matola (President), Kleist Abdallah Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Raikes Kusi na Rawson Watts.

Unasema naonyesha chuki za wazi dhidi ya Nyerere.
Tafadhali weka ushahudi wa hizo chuki wasomaji wazione.

Waasisi wa African Association walikuwa tisa kati ya hawa Wakristo walikuwa watatu.

Nina mifano mingi sana ya namna hii.
Ikiwa ujaridhika na mfano huu nifahamishe nikuongeze mingine.


Mzee bin Sudi
Muasisi wa African Association (1929) na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika
(Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933​
 
Ukitaka vijana tukusome maandiko yako andika historia bila kuchagua zile zenye wazee wako wa kiislamu...nje na hapo tutakupuuza tu.
Mimi ni mkristo ila hata ajitokeze mtu humu kila siku yeye analeta historia ya nchi kwa kuyumbia kwa wakristo nitamuona ni wa ovyo tu na wewe unayependelea upande mmoja.
Ni ushauri tu, andika historia achana na haya unayoandika.
 
Huihui,
Mimi si niliyebadili historia ya Julius Nyerere.
historia ya Mwalimu imebadilika kwa utafiti na niliyoyakuta katika Nyaraka za Sykes.

''Mwezi June, makao makuu ya TAA yalitangaza kamati yake ya utendaji: J. K. Nyerere, Rais, Abdulwahid Sykes, Makamu wa Rais; J. P. Kasella Bantu, Katibu Mkuu; Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz, Katibu wa muhtasari.

Wajumbe wa kamati: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said Tewa, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.''

(Tanganyika Standard 19 June 1953)

Mifano kama hiii iko mingi katika kitabu cha Abdul Sykes na chanzo ni hizo nyaraka.
 
Clever...
Nani kakuambia kuwa mimi nataka kusomwa na vijana?

Mimi nimeandika kitabu wala sikumlenga yeyote.

Unasema niandike historia.

Kwani hapa wewe unasoma kitu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…