Historia ya TANU siku zote imeandikwa na makosa

Wewe ndiyo una uhakika kuzidi J K Nyerere? Kawadanganye wapumbavu wenzio unaowaaandikia vitabu vya kidini
Huihui...
Kuna wakati hapa JF nilipata shida sana.
Nilkikuwa naitwa ''Ustadh,'' ''Sheikh'' ''Mufti'' nk. kwa kejeli.

Ilinichukua muda kutambua kuwa walikuwa wananiambia ''kistaarabu'' kuwa sina elimu ya kufanya na wao mjadala wa kisomi.

Taratibu nilibadilisha mwelekeo wa uandishi wangu nikawa najieleza kistaarabu.
Nilieleweka na kejeli ikakoma.

Lakini hawakuchoka wakaja na mbinu nyingine ya ''udini.''

Hili nalo limepita na wanatambua kutoka huko tulikotoka kuwa sina elimu ya kuweza kufutu masuala ya Uislam kwa hiyo siwezi kuandika kitabu kuhusu Uislam.

Hapo chini ni moja ya picha iliyonisaidia kujieleza.

London 1992

Kitabu hiki niliombwa kuandika na Abantu Publications, Nairobi kuadhimisha miaka 40 ya Azimio la Tabora.

Historia ya Azimio la Tabora ilikuwa haijaandikwa.
 
Tatizo mzee wangu anakosoa kila kitu kilichofanywa na watu wasiokua na mrengo kama yeye kidini na kisiasa.Kizazi cha sasa kipo tofauti ila mzee wangu haelewi
Huo ni mtazamo wako wewe mwana mirengo, ukiachana na hio unaita Mirengo utamuelewa.
 
Huo ni mtazamo wako wewe mwana mirengo, ukiachana na hio unaita Mirengo utamuelewa.
Aipo...
Mshtuko ni mkubwa kwa kila ambae hakujua kuwa historia iliyokuwa ikisomeshwa ilikuwa na makosa makubwa.

Na mshtuko huu uliwaumiza zaidi pale ilipowadhihirikia ukweli kuwa kuna wazalendo wengi hawakutajwa katika historia waijuwayo wao.
 
Mzee usitutishe. Hata watetezi wa mashoga huitwa huko Ulaya na hupendwa sana na wazungu. Wewe mwenye nia ovu na nchi yako lazima tu pia ungeitwa na hao wazungu na kukusifu upumbavu. Mzungu husapoti waafrika wote wenye nia ovu na nchi zao.
 
Kuwapo kwenye kamusi kunakuongezea nini? Hiyo si kamusi ya mambo ya uwongo na chuki tu!!
 
Kwani Wizara ya elimu wame adopt hivyo vipeperushi vyako unavyoandika kwa ujira ?
 
Aipo...
Mshtuko ni mkubwa kwa kila ambae hakujua kuwa historia iliyokuwa ikisomeshwa ilikuwa na makosa makubwa.

Na mshtuko huu uliwaumiza zaidi pale ilipowadhihirikia ukweli kuwa kuna wazalendo wengi hawakutajwa katika historia waijuwayo wao.
Wewe ndiyo unaandika historia ya uwongo na haiwezi kukubalika popote. Nyerere alikuta hao unaoita wazee wako wanacheza dhumna na bao la kete na chama cha TAA. Yeye ndiyo alaleta mawazo ya kupigania uhuru.

Wadanganye hao wanaofurahia uwongo wako tu
 
Ninini hao walichofanya binafsi hadi tukapata uhuru Tanganyika? Usilazimishe hisia binafsi kufanya iwe ndiyo historia ya nchi hii.

Nyerere aliwakuta hao wakiwa na TAA ikiwa ni chama cha social issues tu ila kuja kwake ndiyo aka transform. Kwanza wamshukuru sana Nyerere alikuja otherwise wangeishia tu kunywa kahawa na kucheza bao. Mzee Mohamed Said usitudanganye, wewe mwenyewe ulikuwa na miaka 5, huna jeuri ya kujifanya authority kwenye history ya nchi hii
 
Mzee usitutishe. Hata watetezi wa mashoga huitwa huko Ulaya na hupendwa sana na wazungu. Wewe mwenye nia ovu na nchi yako lazima tu pia ungeitwa na hao wazungu na kukusifu upumbavu. Mzungu husapoti waafrika wote wenye nia ovu na nchi zao.
Mama...
Umuhimu ni kuwa hapa tunasomwa na wengi.

Mimi naeleza niyajuayo katika historia ya Tanganyika na wewe unaandika yako kama hato hapo juu.
 
Mama...
Umuhimu ni kuwa hapa tunasomwa na wengi.

Mimi naeleza niyajuayo katika historia ya Tanganyika na wewe unaandika yako kama hato hapo juu.
Nitolee upumbavu wako hapa wewe Mzee mwovu. Kwenye moja ya nyuzi zako uliandika jinsi ulivyoshiriki vurugu za kuwavunjia wafanyabiashara mabucha yao huko Kimara. Wewe una nia ovu mno. Lakini unajua hii nchi huwa haichezewi.... kawaulize mashehe wa uamsho watakusimulia.
 
Stux...
Kuna nengi walifanya.

Mwaka wa 1950 vijana wakiongozwa na Abdul Sykes walifanya mapinduzi kuondoa uongozi wa wazee katika TAA.

Nyuma ya vijana hawa: Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Dossa Aziz na Dr. Vedasto Kyaruzi kwa kuwataja wachache alikuwa mtu mzima Schneider Abdillah Plantan.

Vijana wakachukua uongozi na kuunda TAA Political Subcommittee kuitia TAA katika mapambano dhidi ya Waingereza.

Mkutano wa Abdul Sykes na Jomo Kenyatta Nairobi.

1952 TAA ikishirikiana na Meru Citizens Union ya Japhet Kirilo ilishughulikia mgogoro wa ardhi ya Wameru hadi UNO.

1953 TAA ilipeleka wajumbe wawili Ally Sykes na Denis Phombeah Northern Rhodesia kuhudhuria mkutano wa vyama vya siasa ulioitishwa na Kenneth Kaunda.

Uamuzi wa kumtia Julius Nyerere katika uongozi wa juu wa TAA Nansio nyumbani kwa Hamza Mwapachu.

Uchaguzi wa Arnautoglo Hall baina ya Abdul Sykes na Julius Nyerere.

Hizi ni baadhi tu ya "land marks," katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Haya yote nimeyaeleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.
 
Mama...
Siwezi kuwa nimefanya jambo hilo ikiwa unasema nimesema kwenye uzi nimefanya weka hapa huo ushahidi badala ya kunitukana.
 
Wewe ndiyo unaandika historia ya uwongo na haiwezi kukubalika popote. Nyerere alikuta hao unaoita wazee wako wanacheza dhumna na bao la kete na chama cha TAA. Yeye ndiyo alaleta mawazo ya kupigania uhuru.

Wadanganye hao wanaofurahia uwongo wako tu
Mimi niandike historia ya uongo ilhali nimepewa Nyaraka za Sykes?

Nyaraka hizi ndizo zilizowatia Sykes katika Cambridge Journal of African History 1989.

Nyaraka hizi ndizo zilizowatia Sykes katika Dictionary of African Biography (DAB) 2011.
 
Yaani tukanunue vitabu vyako msikitini? Hapohapo unadai huna udini. Inasikitisha sana
Mama...
Mimi nimekuwa nikinunua vitabu Cathedral Bookshop miaka yote.

Kitabu changu kinauzwa duka la vitabu Ibn Hazm Media Centre karibu ya msikiti wa Mtoro halikadhalika duka la Ibn Hazm Media Centre jirani ya Msikiti wa Manyema Mtaa wa Mafia.

Hivyo hivyo Ibn Hazm Media Centre duka karibu ya Msikiti wa Mtambani.

Kwani hairuhusiwi kwa Waislam kuwa na bookshop kama waliyokuwanayo Wakatoliki pale St. Joseph's Cathedral?

Kitabu cha Bergen, "Religion and Development," na "Kanisa Katoliki na Siasa Tanzania Bara," vilikuwa vinauzwa hapo.
 
Ndo maana tunasema kitabu chako ni cha kuhusu uislamu na sio TANU wala historia ya nchi hii.
 
Hivyo siyo vitabu ni mkusanyiko wa maandishi ya kiislamu tu. Endelea kufanganya hao wanaokupa nauli ya kwenda Cambridge.
 
Watu wenyewe wote anaowatetea Nyerere aliwapa kazi wao na watoto wao. Mohamed Said sijui alikuwa anataka Nyerere awabebe wazee wa Mohamed Said awabebe mgongoni??
 
Kuwapo kwenye kamusi kunakuongezea nini? Hiyo si kamusi ya mambo ya uwongo na chuki tu!!
Huihui...
Siku hizi kama unafanyiwa usaili kwa ajili ya jambo fulani mwisho huwa unapewa nafasi ya wewe mwenyewe kujieleza kwa nini unadhani wewe ni "special," kwa hiyo upewe nafasi hiyo.

Wamarekani wana mtindo huo wanaita, "Bragging."

Umeniuliza mimi kuwa mmoja wa waandishi wa Dictionary of African Biography (DAB) kunanisaidia nini?

Mimi sitakupa jibu.

Nataka uhangaishe ubongo wako kutafuta jibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…