punainen-red
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 1,731
- 451
Inferiority complex!
Huu ni muswiba mkubwa sana.
Inna Lillahi wainna Illaihi Rajihunna.
Mfano wa watu hawa umebainishwa katika Qur'an (al baqarah) 2: 14-16.
-Rais wa Kwanza na muasisi wa Tanzania.WC,
Kwa maneno mafupi sana. Hebu tupembulie na kutubainishia ni kitu gani hasa Nyerere aliifanyia Tanganyika mpaka apewe swifa ya Ubaba wa Taifa?.
Naomba u list down swifa hizo kama zipo.
-Rais wa Kwanza na muasisi wa Tanzania.
-Tanzania isiyo na DINI wala KABILA.
-Alilinda kwa nguvu MALI na RASILMALI za NCHI hii.
-Sera nzuri mno kwa huduma za jamii. Mimi na wewe tusingekutana humu kama si elimu bure niliosoma.
-TANU na baadaye CCM yenye nguvu na mtandao mpana sana.
-Ukombozi wa majirani zetu toka ukoloni.
Ya Mwalimu ni mengi mno kama haumchukii, haumwonei wivu kwa namna yoyote ile. Mpo mnaomchukia kwa misimamo yake, kwa dini yake, kwa kutofautiana na wazee wenu, kwa USAFI wake, kwa maamuzi yake mbalimbali,...

Mohames said.
Hakika ninajifunza mengi sana kutoka kwako kwani umechimba sana mambo haya kiasi kila siku nikikusoma napata jambo moja jipya ninaloweza kujifunza.
Ahmad rashad Ali nilimfahamu kama mzee wetu na nilimjua kama mtu wa story sana na mnyenyekevu na aliyewahi kujeruhiwa na historia za Tanganyika baada tu ya uhuru wake. Lakin sikujua haya mengine unayonipa.
Hakika ni furaha kubwa kupata darsa hili ili kujua mengi yaliyofichwa .
Allah akubarik sana
Njabu,
Nami nakupa mfano mdogo ulinganishe na huo wako:
Wakuu wa Shule za Umma Kanda ya Dar es Salaam
[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]Aina ya Shule[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Wakristo[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Waislamu[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Jumla[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]Serikali[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]11[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]0[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]11[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]Kata [/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]200[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]15[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]215[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Serikali inakataa kutunga sera za kuondoa upendeleo wa
Wakristo katika elimu na kuendeleza ulaghai dhidi ya
Waislam
Inakuwaje unasema 'hapana' halafu unaandika 'ndio?' Unasema tusiangalie nchi kwa miwani ya dini, sawa, lakini ww unafanya kinyume chake! Umewatambuaje wanaolalamikia utendaji mbovu wa serikali kuwa sio waislam? Na pia umewatambuaje wanaoitetea CCM kuwa ni waislam na kwa sababu ya uislam wa rais? Unataka kutoa kibanzi kwenye jicho la mwenzio kumbe kwako kuna boriti?Siku za hivi karibuni kumeibuka hoja kuhusu mchango wa Waislam katika mambo mbalimbali ya nchi hii. Nyingi zikihusu kupigania Uhuru na ukandamizaji wa kanisa katika Elimu. Kimsingi hakuna ubaya watu kuelezea mchango wa sehemu ya jamii moja katika mambo ya msingi ya nchi yao. Kinachoniumiza mimi ni kuhusisha kanisa katika mambo yanayodaiwa kupotoshwa katika kuandika historia. Pamoja kwamba Uhuru umepatikana wakati ndio nazaliwa lakini kuna wazee kule kijijini kwetu walijihusisha na harakati za kutaka Uhuru wa nchi hii. Bahati mbaya wakurya nao hawajapata nafasi ya kuandika mchango wao katika kudai uhuru. Sijui ni nini hasa kinacholengwa na historia hii ya uhuru lakini naamini hakuna jamii moja inayoweza kudai kwamba ndio ilileta Uhuru wa nchi hii. Huko kwetuu wazee walichanga ng'ombe na mbuzi kwa ajili ya TANU lakini sijaona majina yao popote katika historia. Itoshe tu kusema tulipata uhuru wetu na tutafute namna ya kuifanya nchi hii iondokane na umaskini uliokithiri kwenye rasilimali tele. Aidha, nashindwa kuelewa CHADEMA inahusishwaje na ukristo maana mara kwa mara nimeona watu wakilalamikia utendaji mbovu wa serikali iliyopo madarakani haraka haraka Waislam wanalaani na kutetea maovu hata ya wazi wazi. Akili za kawaida zinaonyesha wanaitetea CCM kwa kuwa inaongozwa na Mwislam mwenzao. Yafaa tukumbuke kwamba mikataba mibovu inaumiza wote bila kujali dini. Kwa hiyo inalazimisha wote tulaani anayetuletea mambo ya kututuesa sisi na watoto wetu bila kujali dini yake. Nawaomba tupanue mawazo yetu tuangalie nchi kwa mapana na sio kwa miwani ya dini
Vitu kama hivi ndivyo ambavyo vinanifanya kuone kuwa wewe ni mchochezi zaidi ya mtafuta haki! Umetuwekea statistics ambazo zitawafurahisha wakina Barubaru na wenzake bila kueleza lolote la maana. Haujatuambia hizo shule ni za awali, msingi, sekondari au nini? Haujutuambia msingi wa wewe kuamini kuwa hao uliowabandika hapa ni wenye dini hizo. Kumbuka kuna wakina Moses wengi tu ambao ni waislamu na wakina Ali ambao ni wakristu. Kutumia majina si ushahidi tosha. Haujatuambia ni mwaka gani hizi statistics zilichukuliwa. Mbaya katika yote ni kama kweli wewe ni mtafiti mahiri ni lazima utajua kuwa data za mwaka mmoja hazionyeshi dalili ya systematic ubaguzi. Tutajuaje kama kuna mwaka ambapo wamisheni walimu wakuu walikuwa wachache kuliko waislamu? Tutajuaje kama kuibuka kwa shule nyingi za kiislamu kunapunguza idadi ya waislamu wenye sifa za uongozi katika shule hizi? Ili kuonyesha bias, angalau ungefanya yafuatayo:Na haya ni mapungufu machache tu ya data zako unazotumia kujenga hoja yako ya unachoita mfumokristo.
- Ungetumia takwimu za muda mrefu. Kwa vile Nyerere yupo sana katika darubini lako basi takwimu hizo zingeanza wakati wake.
- Ungetuwekea uzoefu na qualifications za walimu waliokuwa wakifundisha kwa wakati huo pamoja na dini zao.
- Ungetueleza basis yako ya kujua dini ya mtu.
- Ungetuelezea matokeo ya mitihani ya wanafunzi wakati wa uongozi wa watu wa dini tofauti.
- Umetuambia shule za kata ziko 200 na wakuu wa shule waislamu 15. Namba hizi zinatia shaka kwa jinsi tu zilivyo! Angalia hapa takwimu wanazotoa wenzako halafu utueleze zako ulitolea wapi? SEKTA YA ELIMU MKOA WA DAR ES SALAAM
Amandla.......
Katika hao wakuu wa shule, Wazaramo ni wangapi, Wamanyema wangapi pia? Hili nalo ni muhimu pia. Mtu anazaliwa na kabila lake kwanza. Haya ya DINI na mengine yanafuata baadae. Makabila mengi mwamko wa elimu umekuja baadae sana hasa ambako makanisa yalichelewa kufika. Halafu mbona wenzetu WAHINDI na WAARABU hawaonekani kwenye ajira hizi?
Siku zote Data zinajieleza pasi na shaka yoyote.
Hebu rekebisha miwani yako upitie tena jedwali kwa nia ya kuelewa na sio kwa nia ya kupinga kisha lete hoja.
Wakuu wa Shule za Umma Kanda ya Dar es Salaam
[TABLE="class: cms_table_MsoTableGrid"]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]Aina ya Shule[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Wakristo[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Waislamu[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Jumla[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]Serikali[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]11[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]0[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]11[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]Kata [/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]200[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]15[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]215[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Serikali inakataa kutunga sera za kuondoa upendeleo wa
Wakristo katika elimu na kuendeleza ulaghai dhidi ya
Waislam
Mimi nilitegemea ulete argument ya kuwa data zimechakachuliwa na hivyo kutupa data sahihi au hata kuleta data za Tanzania nzima tokea kuasisiwa kwake 1964.
Vitu kama hivi ndivyo ambavyo vinanifanya kuone kuwa wewe ni mchochezi zaidi ya mtafuta haki! Umetuwekea statistics ambazo zitawafurahisha wakina Barubaru na wenzake bila kueleza lolote la maana. Haujatuambia hizo shule ni za awali, msingi, sekondari au nini? Haujutuambia msingi wa wewe kuamini kuwa hao uliowabandika hapa ni wenye dini hizo. Kumbuka kuna wakina Moses wengi tu ambao ni waislamu na wakina Ali ambao ni wakristu. Kutumia majina si ushahidi tosha. Haujatuambia ni mwaka gani hizi statistics zilichukuliwa. Mbaya katika yote ni kama kweli wewe ni mtafiti mahiri ni lazima utajua kuwa data za mwaka mmoja hazionyeshi dalili ya systematic ubaguzi. Tutajuaje kama kuna mwaka ambapo wamisheni walimu wakuu walikuwa wachache kuliko waislamu? Tutajuaje kama kuibuka kwa shule nyingi za kiislamu kunapunguza idadi ya waislamu wenye sifa za uongozi katika shule hizi? Ili kuonyesha bias, angalau ungefanya yafuatayo:Na haya ni mapungufu machache tu ya data zako unazotumia kujenga hoja yako ya unachoita mfumokristo.
- Ungetumia takwimu za muda mrefu. Kwa vile Nyerere yupo sana katika darubini lako basi takwimu hizo zingeanza wakati wake.
- Ungetuwekea uzoefu na qualifications za walimu waliokuwa wakifundisha kwa wakati huo pamoja na dini zao.
- Ungetueleza basis yako ya kujua dini ya mtu.
- Ungetuelezea matokeo ya mitihani ya wanafunzi wakati wa uongozi wa watu wa dini tofauti.
- Umetuambia shule za kata ziko 200 na wakuu wa shule waislamu 15. Namba hizi zinatia shaka kwa jinsi tu zilivyo! Angalia hapa takwimu wanazotoa wenzako halafu utueleze zako ulitolea wapi? SEKTA YA ELIMU MKOA WA DAR ES SALAAM
Amandla.......
Mkuu Barubaru, ebu nipe darsa maana inaelekea unafahamu sana historia ya kwenu Zanzibar ambako wote walioongoza mapinduzi walienziwa! kwani shujaa wa mapinduzi Kasim Hanga alienziwaje?Je hizo ni sababu tosha za mtu kupewa title ya Ubaba wa Taifa.
Kumbuka kuwa kuna waasisi wengi sana wa Uhuru wenu ambao walihamasisha kupatikana kwa uhuru huo. Na kumbuka kila penye watu zaidi ya wawili lazima pawe na kiongozi. Nyerere alipewa uongozi huo na kuwa rais wa kwanza wa Tanganyika huru. Je hao washirika wake na waliomfadhili wataitwaje? Kule kwetu Zanzibar wote walio ongoza mapinduzi walipewa hadhi ya kuwa MBM ( member wa baraza la mapinduzi) na mwenyekiti wao ni Rais wa Znz. Vipi huko Bara wanapewa hadhi gani? Kwanini apewe Nyerere pekee kuwa baba wa Taifa. Kwanini nao wasiwe wajomba au mababu au ammi wa Taifa lenu.
Nafikiri sababu hii haitoshi kabisa kupewa U Baba wa Taifa.
Nikija kwenye Sera Nzuri. Nafikiri utakumbuka farsafa yake ya maendeleo ya Tanganyika. Alikuwa anasema ili Tanganyika iendelee inahitaji vitu vinne. Watu, Ardhwi, Siasa safi na uongozi bora.. Sasa nikuulize je Tanganyika imekosa nini hapo mpaka jinsi siku zinavyokwenda inazidi kuwa masikini zaidi? Je wajua chanzo cha umasikini wa tanganyika ni yeye Nyerere na sera zake? Ni kipi nyerere alifanikiwa kiuchumi huko Tanganyika?
Kuhusu Elimu. Kumbuka hakuna elimu ya bure. Mimi baba yangu alikuwa mfanya biashara na alilipa kodi kubwa sana Serikalini. Hivyo najinasibu nimesoma kwa kodi za baba yangu na sio bure. Kama mzee wako alikuwa alipi kodi basi ndio ulisoma bure na kama alilipa kodi basi ni matunda ya kodi yake ndio nawe ukasoma.
Moja ya Kudidimiza uchumi wa Tanganyika ni pale Nyerere alipojitolea kusaidia nchi nyingine wakati nchi yake inadidimia. Tukuulize je umenufaika nini na kusaidia nchi nyingine kupata uhuru. Je Tanganyika ilinufaika na nini zaidi ya swifa binafsi kwa Nyerere.
Nakuomba utupe sababu makini sana zinazoweza kutuingia akilini na kujua kwanini awe Baba wa taifa lenu.
Tudadavuie je amesaidia nini katika uhuru wenu? je amesaidia nini katika kukuza uchumi wenu? etc
Mkuu Barubaru, ebu nipe darsa maana inaelekea unafahamu sana historia ya kwenu Zanzibar ambako wote walioongoza mapinduzi walienziwa! kwani shujaa wa mapinduzi Kasim Hanga alienziwaje?
Mzee Mohamed, mwambie Barubaru asikimbilie kusifia kila kitu cha Zanzibar, kwani kunawalioongoza mapinduzi ya Zanzibar ambao hawakuenziwa hata kidogo na badala yake walichinjwa kwakuhofiwa tu!Gwalihenzi pokea kijidarsa lakini ukitaka darsa kamili sema tu Insha Allah nitakupa.
Hivi ndivyo Nyerere alivyomtunuku Abdullah Kassim Hanga:
"Hakika ni wazi Hanga hakutegemea mapinduzi aliyoyaasisiyangemgeukia na kuwa sababu ya yeye kutolewa roho kwa kuuliwa kishenzi. Jambola kusikitisha ni kuwa hadi pale alipokamatwa na kuwekwa jela Ukonga nakufikishwa mbele ya mkutano wa hadhara na kuadhiriwa na Nyerere tayari alikuwakeshapoteza kila kitu achilia mbali dira ya mapinduzi aliyokusudia ingeongozaZanzibar. Hanga hakuwa kamwe na uwezo wa kumfanya Karume lolote kwani Karumetayari alikuwa chini ya mbawa za Nyerere, ngome ambayo Hanga asingewezakuitikisa achalia mbali kuisogelea na kuibomoa. Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa hirizi tosha ya kumkingaKarume.Katika mkasa wa kuuliwa kwaHanga ndipo msemaji mmoja akasema, "Maiti toka makaburini mwao walionyeshaujuzi wa kufanya miujiza na uchawi wao kwani laiti kifo cha Hangakingesababishwa na wale waliyopinduliwa kisasi chake kingekuwa cha kutisha.Ilibidi Hanga kwa miujiza ya maiti zile auliwe na wale wale aliowawekamadarakani watu ambao hapakuwepo na sababu ya wao kumuona adui." Halikudondokachozi kwa kifo cha Hanga. Kila aliyepata mnong'ono wa kuuliwa kwake alikuwakimya kama vile ile taarifa ya kifo haimuhusu." Hakika dunia inazunguka.
Mohamed
Mzee Mohamed, mwambie Barubaru asikimbilie kusifia kila kitu cha Zanzibar, kwani kunawalioongoza mapinduzi ya Zanzibar ambao hawakuenziwa hata kidogo na badala yake walichinjwa kwakuhofiwa tu!
Duh mkuu wangu bado unaliendeleza barza.... Heee ama kweli wajua kuuza kitabu... Kwa hili la Hanga nakuomba sana tena sana funga safari nenda Zanzibar mtafute Nassoro Moyo atakueleza kwa ufasaha kilichotokea (kama atapenda) maana yeye na marehemu H. Hanga walikuwa kundi moja..Gwalihenzi pokea kijidarsa lakini ukitaka darsa kamili sema tu Insha Allah nitakupa.
Hivi ndivyo Nyerere alivyomtunuku Abdullah Kassim Hanga:
"Hakika ni wazi Hanga hakutegemea mapinduzi aliyoyaasisiyangemgeukia na kuwa sababu ya yeye kutolewa roho kwa kuuliwa kishenzi. Jambola kusikitisha ni kuwa hadi pale alipokamatwa na kuwekwa jela Ukonga nakufikishwa mbele ya mkutano wa hadhara na kuadhiriwa na Nyerere tayari alikuwakeshapoteza kila kitu achilia mbali dira ya mapinduzi aliyokusudia ingeongozaZanzibar. Hanga hakuwa kamwe na uwezo wa kumfanya Karume lolote kwani Karumetayari alikuwa chini ya mbawa za Nyerere, ngome ambayo Hanga asingewezakuitikisa achalia mbali kuisogelea na kuibomoa. Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa hirizi tosha ya kumkingaKarume.Katika mkasa wa kuuliwa kwaHanga ndipo msemaji mmoja akasema, Maiti toka makaburini mwao walionyeshaujuzi wa kufanya miujiza na uchawi wao kwani laiti kifo cha Hangakingesababishwa na wale waliyopinduliwa kisasi chake kingekuwa cha kutisha.Ilibidi Hanga kwa miujiza ya maiti zile auliwe na wale wale aliowawekamadarakani watu ambao hapakuwepo na sababu ya wao kumuona adui. Halikudondokachozi kwa kifo cha Hanga. Kila aliyepata mnongono wa kuuliwa kwake alikuwakimya kama vile ile taarifa ya kifo haimuhusu. Hakika dunia inazunguka.
Mohamed