Extremes are dangerous!!!!!!! MS angetanabaisha wazi kuwa angle anayotumia ni ya KIDINI, ila si kupotosha historia nzima ya UHURU wa nchi yetu. Nomba kuuliza neno HISANI katika dini yetu ina maana gani? Maake naona Nyerere alisahau hisani, sijui inasemekana nini............ Neno hili HISANI lina maana au umuhimu gani? Hadithi za MS are the same as carrying coas to Newcastle.
Naona umekuja na hadithi ndeefu na takwimu nyingi lakini hoja dhaifu sana. Mohamed Said anasema hao wazee wa hicho "kitongoji" ndio waliosahauliwa katika historia na ndio yeye ameamuwa kushika kalamu na kuandika historia yao na vipi walishiriki kikamilifu katika harakati za kujitwalia madaraka na hizo harakati walizianza kabla ya Nyerere kukaribishwa kuungana nao.
Kumbuka kuwa hicho "kitongoji" ndio kilikuwa mstari wa mbele katika harakati, hicho "kitongoji" ndio kilikuwa mwanzo wa vyama kama TAA kilicho zaa TANU, hicho "kitongoji" (Ashaakum si matusi) ndicho kilichomvalisha suruali Nyerere, nasikia alikuja na kaptura, na picha zake za zamani kweli zinaonesha akivaa kaptura ya Khaki na soksi ndefu mpaka karibu ya magoti na viatu vyeusi (kama wale wanaocheza ngoma za Kinyasa kama umebahatika kuwaona).
Kinachowekwa sawa ni kuwa siasa za harakati za kudai madaraka hazikuanzia kwa Nyerere na wala Nyerere sio muasisi wa hizo harakati, hao wazee wa hicho kitongoji ndio waasisi wa harakati zote zilizotufikisha kupewa madaraka na Umoja wa Mataifa. Ni matusi makubwa zaidi kuwaacha hao wazee katika historia hususan kwa mtoto wao Mohamed Said, msomi na mtunzi wa historia anaetambulika vyuo vingi vikuu duniani na ambae ameshaandika vitabu na "papers" nyingi zinazotumika katika vyuo vikuu. MashAllah.
Muwie radhi nduguyo huyo maana wakati mwingine nawe waweza kujikuta umesema kitu cha kumkwaza mtu na ikawa kumbe ni kughafirika tu kwa ubinadamu. Vizuri ni kufuata maxim yangu ya muda "hoja hujibiwa kwa hoja si viroja"
Asante Mungu JF inaelekea kurudi kwenye hadhi yake mijadala ya aina hii ndiyo ilinifanya nikajiunga na hili jamvi lakini kuanzia mwaka 2010 tulivamiwa na kundi la wahuni wasiopenda mijadala yenye afya bali matusi na kejeli.
Mzee Mohamed Said,Fundi Mchundo,Jasusi,FaidaFoxy,WildCard,Mzee Mwanakijiji,Mwita Maranya,Nguruvi3,Mag3 na wengine wote niliowasahau kwa bahati mbaya tafadhali sana tujiepushe na lugha za kuudhi,kejeli au matusi kwa faida ya mjadala.Niseme kweli nimejifunza mambo mengi kupitia kwenu na nina hakika wako wengi pia kupitia michango yenu wamefaidika sana.
Sawa Mama!! Endeleeni ku-flog a dead horse...........Hilo neno linamaanisha "Punda wangu", kama hujapenda uliza ajuae kiarabu.
wana JF tusimsakame sana uyu mohamedi, unajua kila nchi kunakua na jamii ya mlengo wa kushoto, mlengo wa kulia na wa kati,
ANACHOANDIKA MOHAMEDI KINAWEZA KUWA NI UCHOCHEZI KWA UPANDE MMOJA LAKINI KWA UPANDE MWINGINI ANAWAJULISHA WALE AMBAO WALIKUWA WANELEWA HISTORIA KWA UCHACHE WAKE.
NADHANI KAMA UYU MWANDISHI ANACHOKIANDIKA NI CHA UONGO NA HANA UHAKIKA NACHO BASI TUNAAMINI ANAKIUKA MAADILI YA KAZI YAKE NA KAMA NI IVO SERIKALI IPO BASI ICHUKUE HATUA DHIDI YAKE KWA KULETA UCHOCHEZI WA KIDINI.
HAYA ANAYOANDIKA UYU MWANDISHI NI BAADHI TU YA HISTORIA AMBAYO JAMII FULANI YA WA TANZANIA WANAAMINI IPO ILA KWA SABABU FULANI FULANI NA KWA MASLAHI YA WATU AU JAMII FULANI TULIKUWA ATUFUNDISHWI MASHULENI KWETU KUHUSU HISTORIA KAMILI YA NCHI YETU.
MUACHANI AENDELEE KUIJUZA JAMII NAAMINI ANAVYO VYANZO NA USHAIDI WA KUTOSHA, TUSIMUHUKUMU KWA JAZBA ZETU
Hapa nanusa kaarufu ka chuki binafsi Kwa Mwalimu Nyerere, anyway kama historia" imewasahau" hawa wazee wa gerezani nina uhakika wako wengi "waliosahauliwa" sehemu nyingine pia katika ukombozi wa nchi yetu hii. Mohamed Said anafanya kila anachoweza kumulika hilo lakini tatizo lake ni kuweka udini kidogo kwenye hili na ndiyo hapo utafiti" objective" unarushwa nje na hisia binafsi kutawala zaidi. Ningependa kuongea mawili matatu kumjibu Mr Said kama ifuatavyo;
Vita ya ukombozi Afrika yetu hii mara nyingi ilianzishwa na wakazi wa mijini kama wafanya kazi wa serikali, madereva, makuli, wafanya biashara ndogo ndogo, waandishi n.k kwa hapa kwetu walikua wapwani, watu wa DSM, na haswa pale gerezani, sawa sawa, lakini hawa wote iwe Tanganyika, Nigeria, au Ghana ilibidi wapate nguvu za mikoa ya ndani yenye wananchi wengi ili kukamilisha kile walichokianza na hapa sasa ndiyo akina Bomani na Nyerere na wasukuma, wanyamwezi, wahaya,wapare, na wanyakyusa wanapokuja. Sijui Mo Said alitaka historia iwaadikaje hao lakini kila mwenye mchango muhimu kwenye ukombozi wa nchi hii ameguswa na wengine wengi wameachwa siyo hawa tu wa gerezani
Kingine pamoja na yote kuanzisha kitu na kumalizia kitu ni vitu viwili tofauti sana katika maisha haya ya mwana adam na wote nafikiri tunajua hili. Napenda kuungana na mag3 kuhusu mchango wa Watanganyika wa sehemu zingine zisizokua Pwani, huu mchango ulikua mkubwa na wenye chachu kubwa katika kuleta uhuru, pwani pekee yao wasingeweza, ila hawa wa maeneo mengine wangeweza bila ya Pwani, hilo Mo Said inabidi kulijua na hapa siongelei udini ila ukanda kama naweza kuuita hivyo. Na hili linaondoa umuhimu wa kipekee au kama Mo said angependa kuiweka umuhimu wa uanzishaji wa kitu na nafasi ya muanzishaji kwenye historia, hivi tunajua nani alianzisha motor engine? hapana Kila mtu anasema ni huyu au Yule, na je ina maana yeyote au umuhimu gani kumjua katika jamii? Nafikiri hapana labda tu kama wewe ni mwanahistoria na unataka kuandika kuhusu hilo la mashine. Mchango wa Syskes, Bomani, wasukuma, Abushiri Salum, Nyerere, wanyakyusa, wapare, wachaga na wengine uko wazi na kwa hili sisi siyo wana historia na waanzilishi wa TAA tusiowajua hawatunufaishi kama jamii kwa lolote, bwana Said angalia hili kwa mawazo mapana.
Na napenda kuongeza hata kama hawa wa gerezani wangekua wanashirika katika ukoloni kama tabaka la pili la kinyonyaji bado mapambano yangeanzishwa tu na wengine wasomi wa mikoa ya ndani kwani si wangeona ndugu zao wengine wa Afrika wanafanya nini kwa hiyo hapa hii "indignation" yako haina maana ya hawa kupewa nafasi kubwa na muhimu katika historia ya ukombozi wetu wakati wako wengi tu waliosahaulika kama unavyodai wao.
Shukhran,
Sawa Mama!! Endeleeni ku-flog a dead horse...........
Jee, na hao waandishi wengine waliowasahau wazee wa Dar. waliwasahau kwa ajili walikuwa ni Waislaam?
Sasa hili la Bi Titi la hadithi chanya kwa sababu kaelezea kwa kutumia nasaba yake yaani Titi Mohamed, sasa kama tunataka kuelezea hao wagerezani basi watajwe majini, yao na mchango wao na kusauliwa kwao, lakini bahati Mbaya Abdulwahid alifariki mapema sijui leo hii angekuwa nani, Abas alikuwa Balozi wetu huko Italia nk, Ali akaamua kuwa mfanya Biashara mkubwa wa Insurance na Travel Agent na Uzalisha wa Soda Tanga, baadae Magodown yake yaka kituo cha kuhifadhia Bia za East Africa Breweries, na kuna wengi walio amua kufanya Biashara wengine walifanya kaziSerikalini, sasa Uislamu unapowekwa mbele ndipo hapo maudhuwi yana potoshwa, kwa sababu kuna wengine hawataweka dini yao mbele bali Kabila au makabila yao, mwisho wa siku tutakua hatujengi taifa, bali nafsi zetu, kwa mfano wakati wa akina Isike, Bushiri, Mkwawa , Milambo nk nk tuliwajua kwa nafsi zao, na leo hii subjects wao hawasemi kwamba bila wao taifa hili lisinge kuwa huru? na mind you wakati huo mawasiliano hayakuwa mazuri hivyo unapochukulia historia/hadithi ya gerezani kuwa ndio chanzo cha harakati za ukombozi au ndio walio leta uhuru ni kujidanganya au kujaribu kupotosha ukweli? maana kama niliposema mwanzo mawasiliano yalikuwa duni, hivyo dunia yao iliishia gerezani kwa kuwaona hao akina sykes baada ya kutoka vitani burma. lakini kuna wazee wetu wengi tu walikuwa si watu wa kupiga kelele (wastaarabu) kama Rashid Mfaume Mungu amlaze pema peponi kuna wazee wa bagamoyo, magomeni .mtoni kwa azizi Ali, kilwa kivinje nk nkJamani kuna tatizo hapa, ishu sio kuyakataa anayosema Mohamed, ishu ni kuwa yapo mengi kuhusu taifa hili ambayo hatuyajui na yanajulikana na wachache miongoni mwetu. Basi kila mmoja aliandike lake analolifahamu ile wengine nao pia wapate kufahamu na pengine kujua Nyerere aliyakuasanyaje yote hayo pamoja akayazika na kujenga taifa lisilo na historia ndogondogo labda ambazo zisingetuwezesha kuwa wamoja kama tulivyo leo. Kama yapo yasemwe, yaandikwe tuyafahamu na eti si kumwambia mwingine asiseme kwa kuwa wewe hujayasema unayoyafahamu. Ajabu na kweli hata Bibi Titi Mohamed nae ametoa malalamiko ya kusahauliwa waliopigania uhuru kikwelikweli. Malalamiko yake yapo katika kitabu chake kiitwacho WANAWAKE WA TANU, kilichochapishwa na E&D VISION PUBLISHER kikiwa kimedhamioniwa na TGNP. Ukiemda E&D pale Afrika Sana Sinza utakipata au ukienda TGNP utakipata. Kama hata BIBI TITI alilalamika ni wazi kuna tatizo hapa. Kuna Tatizo kama lile alilolizungumza Jaramongi Odinga katika Not Yet Uhuru na kuna Tatizo kama lile alilochagiza Ngugi katika vitabu vyake A grain of Wheat na MATIGARI. Tufungue macho tuone ni jinsi gani tutaweza kuliingiza hili ndani yetu na kusema hili ni tatizo kisha tulitafutie tiba. Hatuwezi kulitibu kama hatujajua hili ni tatizo
Sasa hili la Bi Titi la hadithi chanya kwa sababu kaelezea kwa kutumia nasaba yake yaani Titi Mohamed, sasa kama tunataka kuelezea hao wagerezani basi watajwe majini, yao na mchango wao na kusauliwa kwao, lakini bahati Mbaya Abdulwahid alifariki mapema sijui leo hii angekuwa nani, Abas alikuwa Balozi wetu huko Italia nk, Ali akaamua kuwa mfanya Biashara mkubwa wa Insurance na Travel Agent na Uzalisha wa Soda Tanga, baadae Magodown yake yaka kituo cha kuhifadhia Bia za East Africa Breweries, na kuna wengi walio amua kufanya Biashara wengine walifanya kaziSerikalini, sasa Uislamu unapowekwa mbele ndipo hapo maudhuwi yana potoshwa, kwa sababu kuna wengine hawataweka dini yao mbele bali Kabila au makabila yao, mwisho wa siku tutakua hatujengi taifa, bali nafsi zetu, kwa mfano wakati wa akina Isike, Bushiri, Mkwawa , Milambo nk nk tuliwajua kwa nafsi zao, na leo hii subjects wao hawasemi kwamba bila wao taifa hili lisinge kuwa huru? na mind you wakati huo mawasiliano hayakuwa mazuri hivyo unapochukulia historia/hadithi ya gerezani kuwa ndio chanzo cha harakati za ukombozi au ndio walio leta uhuru ni kujidanganya au kujaribu kupotosha ukweli? maana kama niliposema mwanzo mawasiliano yalikuwa duni, hivyo dunia yao iliishia gerezani kwa kuwaona hao akina sykes baada ya kutoka vitani burma. lakini kuna wazee wetu wengi tu walikuwa si watu wa kupiga kelele (wastaarabu) kama Rashid Mfaume Mungu amlaze pema peponi kuna wazee wa bagamoyo, magomeni .mtoni kwa azizi Ali, kilwa kivinje nk nk
Sasa hili la Bi Titi la hadithi chanya kwa sababu kaelezea kwa kutumia nasaba yake yaani Titi Mohamed, sasa kama tunataka kuelezea hao wagerezani basi watajwe majini, yao na mchango wao na kusauliwa kwao, lakini bahati Mbaya Abdulwahid alifariki mapema sijui leo hii angekuwa nani, Abas alikuwa Balozi wetu huko Italia nk, Ali akaamua kuwa mfanya Biashara mkubwa wa Insurance na Travel Agent na Uzalisha wa Soda Tanga, baadae Magodown yake yaka kituo cha kuhifadhia Bia za East Africa Breweries, na kuna wengi walio amua kufanya Biashara wengine walifanya kaziSerikalini, sasa Uislamu unapowekwa mbele ndipo hapo maudhuwi yana potoshwa, kwa sababu kuna wengine hawataweka dini yao mbele bali Kabila au makabila yao, mwisho wa siku tutakua hatujengi taifa, bali nafsi zetu, kwa mfano wakati wa akina Isike, Bushiri, Mkwawa , Milambo nk nk tuliwajua kwa nafsi zao, na leo hii subjects wao hawasemi kwamba bila wao taifa hili lisinge kuwa huru? na mind you wakati huo mawasiliano hayakuwa mazuri hivyo unapochukulia historia/hadithi ya gerezani kuwa ndio chanzo cha harakati za ukombozi au ndio walio leta uhuru ni kujidanganya au kujaribu kupotosha ukweli? maana kama niliposema mwanzo mawasiliano yalikuwa duni, hivyo dunia yao iliishia gerezani kwa kuwaona hao akina sykes baada ya kutoka vitani burma. lakini kuna wazee wetu wengi tu walikuwa si watu wa kupiga kelele (wastaarabu) kama Rashid Mfaume Mungu amlaze pema peponi kuna wazee wa bagamoyo, magomeni .mtoni kwa azizi Ali, kilwa kivinje nk nk
August,
Sijapatapo kusema kuwa bila ya watu wa Gerezani uhuru usingepatikana.
Kilichofanya mimi niandike historia ya wazee wangu ni kuona kuwa wameondolewa
kwa makusudi katika historia hiyo na sababu ya kuondolewa kwao ilikuwahistoria
nzima ya kudai uhuru wa Tanganyika imesheheni Waislam.
Lakini huwezi kuyajua haya hadi ufahamu ugomvi uliozuka kati ya Nyererena Waislam
mara tu baada ya uhuru kupatikana.
Ikiwa hamtoona vibaya niko tayari kuweka hapa ukumbini chanzo cha ugomvi ule na
vipi historia iliyoandikwa ya uhuru ilivyohujumiwa nk. nk.
Ninaloomba kwa ndugu zangu punguzeni hamaki. Someni hizi nyuzi kwa utaratibu na
tuhojiane kiungwana.
Huu ni mnakasha tu.
Mwisho na kama nanyi mnazo historia kutoka kwenu kuhusu harakati za kudai uhuru
ziwekeni hapa jamvini tunogeshe baraza.
Mohamed
Son of Alaska,Hapa chini nakuwekea jinsi chokochoko zilivyoanza:"Jaribio la mwanzo la Nyerere kutaka kuivunja EAMWS lilikuwa mwaka 1963. Lakini jaribio hilo halikufanikiwa kwa sababu ya mpango uliopangwa na Mufti Sheikh Hassan bin Amir na kutekelezwa na Bilali Rehani Waikela, katibu wa EAMWS Tabora. Mwaka huu wa 1963 EAMWS ilifanya mkutano wake katika ukumbi wa Shule ya wasichana ya Aga Khan. Wajumbe wa mkutano huo walipowasili mjini Dar es Salaam walikuta uvumi kuwa wajumbe wa mkutano wa EAMWS watakamatwa na kuwekwa kizuizini. Chanzo cha uvumi huu hakikufahamika lakini haikuwa vigumu kuhisi. Baada ya kuvunjwa kwa Baraza la Wazee wa TANU mwaka ule ilikuwa wazi kuwa Nyerere alikuwa amewatupa mkono washirika wake wa zamani na sasa alikuwa akitafuta wapya ili kujenga upya msingi wake wa siasa. Kutokana na mambo yalivyokuwa yakienda ilikuwa ni dhahiri washirika wake wapya hawatakuwa Waislam.Katibu wa EAMWS Tabora, Waikela alipowasili Dar es Salaam kuhudhuria mkutano aliitwa na Sheikh Hassan bin Amir. Mufti Sheikh Hassan bin Amir mbele ya Mzee Ali Comorian, alimfahamisha Waikela kuwa kulikuwa na njama zilizokuwa zikipikwa na Nyerere kumuungamiza yeye na Tewa Said Tewa ili kuvunja EAMWS ipatikane nafasi ya kuanzishwa jumuiya ya Kiislam ya Watanganyika itakayokuwa chini ya wanafiki. Sheikh Hassan bin Amir alimwambia Waikela kuwa harakati za uhuru zilikuwa zinatekwa nyara na Wakristo kwa manufaa ya makanisa yao. Sheikh Hassan alimfahamisha Waikela kuwa ni lazima yeye afanye kila linalowezekana ili njama za Nyerere zishindwe. Waikela alimuuliza Sheikh Hassan bin Amir kwa nini amechaguliwa yeye kufanya kazi ile. Sheikh Hassan bin Amir alimuambia kuwa yeye ana imani na uwezo wake. Baada ya maneno hayo Sheikh Hassan bin Amir alinyanyua mikono yake juu na kumuombea dua Waikela. Nyerere alikuwa anamfahamu Waikela kwa kuwa alikuwa muasisi wa TANU na alikuwa ametoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru.Nchi nzima hasa sehemu za Waislam kulikuwa mpango wa serikali wa kuwavunja Waislam nguvu na kuwakatisha tamaa. Waikela, kama ilivyokuwa kwa viongozi wengine wa EAMWS alikuwa anasuguana na Mkuu wa Mkoa wa Jimbo la Magharibi, Richard Wambura. Kulikuwa na ujeuri kwa upande wa serikali walipokuwa wanashugulikia matatizo ya Waislam, mbali na mategemeo ya Waislam waliyokuwanayo kabla ya uhuru. Subira ya Waikela ilifikia kikomo pale Wambura alipowatukana Waislam katika mkutano wa hadhara. Baada ya kuhutubia Wambura, Waikela alipanda jukwaani na akaikumbusha serikali isiwe mwizi wa fadhila kwa kusahau jinsi Waislam walivyojitolea muhanga katika kudai uhuru. Serikali ikachukulia hotuba ya Waikela kama usaliti na yenye kuwashawishi Waislam wasiitii serikali. Ilikuwa katika hali hii Waikela mwanachama shupavu wa TANU alijitoa kwenye chama na akaamua kutumia nguvu zake kuwatumikia Waislam kupitia EAMWS. Ilikuwa wazi kuwa Nyerere alikuwa na habari za msuguano kati ya serikali na Waislam kule Tabora na mtu ambae alikuwa akihusika na msuguano huo. Siku kabla ya mkutano wa EAMWS, Nyerere aliwaalika wajumbe wa mkutano Government House kwa chakula cha usiku. Hao waalikwa walikuwa wajumbe waliochaguliwa mahsusi. Waikela hakuwa mmoja wa hao waalikwa. Nyerere alichukua nafasi ile kuwashauri wajumbe wale waanzishe jumuiya ya Waislam wa Tanganyika ichukue nafasi ya EAMWS. Wajumbe hawa walipoleta katika mkutano hoja ya kuanzisha jumuiya ya Waislam wa Tanganyika, Waikela alisimama na kuipinga hoja ile. Alizungumza vilevile kuhusu uadui wa serikali kwa Waislam na Uislam. Waikela alimaliza hotuba yake kwa kutoa changamoto kwa wajumbe wamuite Nyerere kwenye ufunguzi wa mkutano ili aje awaeleze wajumbe msimamo wake kuhusu kadhia hii ya chinichini baina ya serikali na Waislam. Baada ya kushindwa kwa hoja ya kuivunja EAMWS wajumbe wa mkutano ikaonekana kuwa ingekuwa vyema Nyerere aitwe kufunga mkutano ule na asomewe makubaliano yaliyofikiwa. Nyerere alifika kufunga ule mkutano na akakutana uso kwa uso na Waikela, ambae alimsomea maazimio ya mkutano. Waikela alimfahamisha Nyerere kuwa umoja kwa Waislam ni fardh ñ wajibu wa lazima. Ni kwenda kinyume na maamrisho ya Allah kuwagawa watu. Baada ya utangulizi huu Waikela huku akimnyooshea Nyerere kidole alieleza uadui unaoonyeshwa na serikali dhidi ya Waislam. Waikela alimaliza hotuba yake kwa kitisho. Alimwambia Nyerere ikiwa Waislam watamgeuka kupambanana yeye hatakuwa na uwezo wa kuwashinda. Nyerere alitulia tuli pembeni mwa Rais wa Baraza la Tanganyika la EAMWS Tewa Said Tewa akimsikiliza Waikela. Aliposimama kujibu hotuba ya Waikela Nyerere kwa upole alisisitiza msimamo wa serikali wa kutoa haki na usawa kwa raia wake wote. Kwa kiasi fulani Nyerere alikuwa amefanikiwa kupunguza joto kati ya Waislam na serikali. Hotuba ya Waikela na ya Nyerere zikapewa umuhimu mkubwa katika radio. Waislam wengi wakajitokeza stesheni ya gari moshi Tabora kuja kumpokea shujaa Waikela. Alipewa heshima ile kwa kuwa na ujasiri wa kuweza kusimama kidete dhidi ya wale waliodhani kuwa wanaweza kuwakalia Waislam vichwani. Nyerere alihisi ameumbuka na hili lilimchoma moyo sana. Kuanzia hapa Nyerere hakumtazama Sheikh Hassan bin Amir kwa jicho jema. Alingoja nafasi yake ili alipize kisasi. Mwaka ukiofuata, tarehe 20 Januari, 1964 jeshi liliasi. Nyerere alichukua fursa ile kuwatia kizuizini masheikh walioonekana wanapinga serikali na viongozi wa vyama vya wafanyakazi. Waikela alikuwa mmoja wa wale waliokamatwa na kuwekwa kizuizini. Nyerere kwa wakati ule hakuwa na nguvu ya kumgusa Mufti Sheikh Hassan bin Amir.Wakati ule mwaka wa 1963 shughuli za kueneza dini za EAMWS zilikuwa zikienda vizuri sana. Tabligh ilikuwa chini ya Sheikh Amir bin Juma kutoka Tanga na Wakristo wengi walikuwa wakirudi katika Uislam. Tabligh ilikuwa ikiongozwa kutoka kwa masheikh wa mikoa na wilaya. Fedha za kufanyia shughuli hizi zilikuwa zikichangwa na Waislam wenyewe. Mufti Sheikh Hassan Bin Amir yeye alikuwa akisomesha fikh, mantik, tauhid, na tafsir ya Qurían katika misikiti mbalimbali ya Dar es Salaam Wakati ule Katibu Mkuu wa EAMWS kwa Afrika ya Mashariki alikuwa V.M. Nazarali. Mwezi Aprili 1964 ujumbe wa hali ya juu wa EAMWS ndani yake wakiwemo Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Said Omari Abdallah, Tewa Said Tewa, Katibu wa EAMWS Abdul-Aziz Khaki na mzee wa TANU Mzee Mwinjuma Mwinyikambi; Makisi Mbwana, Issa Mtambo, Omari Muhaji na Saleh Masasi waliondoka kwenda ziara ya nchi za Kiislam kutafuta msaada wa kujenga Chuo Kikuu cha Kiislam na kuanzisha uhusiano na nchi za Kiislam. Gamal Abdel Nasser alifurahishwa sana na ujumbe wa Tanganyika kiasi kwamba ingawa alikuwa katika matayarisho ya mapokezi ya Waziri Mkuu wa Urusi Kruschev, na ingawa ujumbe wa EAMWS ulikuwa wa kidini zaidi kuliko wa kiserikali, alikutana na ujumbe ule akaupatia ofisi, huduma za simu, na makatibu muhtasi ili waweze kutayarisha mipango yao kwa serikali ya Misri bila shida. Halikadhalika alimuagiza makamu wake Sharbasy afanye makubaliano na EAMWS kwa niaba yake. Serikali ya Misri ilikubali kugharamia ujenzi wa chuo hicho. Mkataba wa makubaliano ukatiwa sahihi mjini Cairo kati ya Tewa Said Tewa kwa niaba ya EAMWS na Makamu wa Rais wa Misri, Sharbasy kwa niaba ya serikali yake. Serikali ya Misri iliahidi kujenga Chuo Kikuu cha Kiislam ambacho kitamilikiwa na kuendeshwa na EAMWS. Gharama ya mradi mzima uliuwa pauni milioni hamsini na tano za Ki-Misri. Baada ya kukamilisha kazi ile ujumbe ule uliondoka Cairo kuelekea Makka kufanya ibada ya hija. Baada ya kumaliza hija wajumbe wanne walirudi nyumbani na Tewa, Aziz Khaki, Sayyid Omar Abdallah wakaendelea na safari kwenda Aman, Jordan ambako walifanya mazungumzo na Mufti na Waziri wa Aukaf. Kutokea hapo ujumbe ulikwenda Kuwait ambako walikutana na Sheikh wa Kuwait kisha wakaenda Bhaghdad, Iraq na kukutana na rais wake, Abdisalama Arifek. Kutoka hapo ujumbe ulielekea Beirut, Lebabon ambako ulifanya mazungumzo na viongozi wa harakati za Kiislam. Baada ya kutoka Beirut ujumbe ule ulirudi tena Cairo kwa ajili ya kukamilisha makubaliano ya kujenga Chuo Kikuu. Tarehe 20 Mei, 1964 ujumbe ulirejea Dar es Salaam na kupokelewa na viongozi wa EAMWS na Waislam kwa ujumla. Mkutano wa Halmashauri Kuu ya EAMWS ukaitishwa na Tewa Said Tewa akatoa taarifa yake kuhusu ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Kiislam. Siku ya pili Tewa akaitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutoa habari za kufurahisha za kujengwa kwa Chuo Kikuu Cha Kiislam kwa vyombo vya habari na kwa Waislam kwa ujumla. Kwa mafanikio haya Tewa akawa amejichimbia kaburi. Matokea haya yalijaza hofu kwa viongozi wa Kanisa. Kampeni za chinichini dhidi ya Tewa binafsi na uongozi mzima wa EAMWS zilianza.Mara baada ya ujumbe wa EAMWS kurudi kutoka ziara yake, Nyerere alifanya mabadiliko katika baraza la mawaziri na Tewa Said Tewa, Mwenyekiti wa EAMWS upande wa Tanzania akajikuta nje ya serikali. Nyerere akamteua Tewa balozi wa Tanzania katika Jamuhuri ya Watu wa China. Mwezi Januari, 1965 Tewa alikwenda China kuanza kazi yake mpya. Inasemekana uteuzi wa wa Tewa kwenda China ulisababishwa na juhudi zake za kutaka kuwaunganisha Waislam kuwa kitu kimoja chini ya jumuiya moja yenye nguvu. Wakati ule ile mipango iliyopitishwa na mkutano wa Waislam mwaka 1962 ilikuwa ikitekelezwa vyema, shule zilikuwa zimejengwa Ilala, Kigogo na Kurasini, Dar es Salaam; shule zilikuwa zimejengwa Ruvu na Maneromango. Shule hii ya Maneromango ilikuwa na umuhimu wa pekee kwa sababu hii ndiyo ilikuwa shule ya kwanza ya Waislam kujengwa Uzaramo. Shule za upili zilikuwa zikijengwa Dar es Salaam, Kinondoni na Moshi, Kibohehe. EAMWS ilikuwa vilevile imetiliana mkataba wa makubaliano na serikali ya Misri kuipa scholarship thelathini na tano kila mwaka kwa wanafunzi wa Kiislam kusoma Misri. EAMWS ilikuwa imejenga shule, misikiti, shule za ufundi na hosteli kwa ajili ya wanafunzi katika sehemu nyingi za Afrika ya Mashariki. Kwa hakika EAMWS ilikuwa ikifanya mambo ya maendeleo kwa Waislam."MohamedMohamed Said,tuwekee chanzo,kama ni kweli huo ugomvi wa Nyerere na waislam mara tu baada ya uhuru kupatikana
Mohamed Said,tuwekee chanzo,kama ni kweli huo ugomvi wa Nyerere na waislam mara tu baada ya uhuru kupatikana
Mohamed Said,tuwekee chanzo,kama ni kweli huo ugomvi wa Nyerere na waislam mara tu baada ya uhuru kupatikana