Prof Griff
JF-Expert Member
- Aug 29, 2008
- 6,772
- 5,258
Wewe unaweza kuuliza swali la maana linalohitaji kujibiwa na msomi? unafikiri tunaimba mapambio kanisani?
Uliza swali kwa taratibu za mjadala utajibiwa ki-academic..siyo kashfa na matusi..watu wengine wana heshima zao..na wamelelewa kidini ..
Nasema hivii, "Mwamedi Saidi ameshindwa na kujaribu kwa kila namna kukwepa kujibu maswsali na hoja husika kuhusu maandishi yake mwenyewe. Ushahidi usiopingika unaonyesha kuwa Mwamedi Saidi ni msomi feki kwa vigezo vyote vya viwango na usomi unaokubalika kimataifa isipokuwa labda vile vya madrassah."
Kama wewe ndio kipimo cha standard za upi kasoma na upi hajasoma ok
Lakini kama kipimo cha usomi kuna standard na namna zake kupima ikiwemo uwezo wa
Ku-publish kwenye peer reviewed journals then wewe utabaki kubwabwaji na hisia zako..
Zilizotokana na kuw "arrogant and Incompetent" leta paper moja uliyo publish hata journal CBE??
Turudishe mnakasha pahala pake...Brother MS endeleza darsa la simulizi...lakini pia ujibu maswali uliyoulizwa...
......Ogah, Sasa tuendelee tuko 1959 AMNUT ishaundwa ili kulinda maslahi ya Waislam katika Tangnayika huru...: "Lengo kuu la AMNUT lilikuwa ni kulindahaki na maslahi ya Waislam ambayo ilikuwa ikihisi yalikuwa hatarini katikaserikali iliyoshikiliwa na Wakristo... Mohamed
?Mohamed Said;2590418]AMNUT ilipokuja viongozi hawa wa Kiislam walikiona chama kile kama nuksi inayotaka kuwabagua watu
kwa misingi ya dini na hivyo kuleta vita na kuwapa Waingereza sababu ya kutotoa uhuru.AMNUT ikapigwa vita na haikuweza kufanikiwa.Mohamed
Ogah,
Insha Allah nitajitahidi kujibu pale nitakapoweza.
Sasa tuendelee tuko 1959 AMNUT ishaundwa ili kulinda maslahi ya Waislam katika Tangnayika huru...:
"Lengo kuu la AMNUT lilikuwa ni kulindahaki na maslahi ya Waislam ambayo ilikuwa ikihisi yalikuwa hatarini katikaserikali iliyoshikiliwa na Wakristo. Abdulkarim alikwenda Tabora kujaribukutafuta kuungwa mkono AMNUT lakini matokeo yalikuwa ya kukatisha tamaa.Abdulkarim alichagua Tabora kwa sababu ilikuwa mahali penye athari kubwa yaUislamu. Hata hivyo Abdulkarim alifanikiwa kupokea mwaliko kutoka kwa AliMuhsin Al Barwani kiongozi wa Zanzibar Nationality Party (ZNP) ahudhuriemkutano wa kamati kuu na awakilishe suala la AMNUT. Mkutano huu ulifanyikakatika ofisi ya ZNP Darajani huko Zanzibar. Ali Muhsin alimwambia Abdulkarimkwamba ZNP haiwezi kujifungamanisha na tatizo la Uislam kwa sababu ZNP haikuwainaamini kama Ukristo una uwezo wa kuhatarisha Uislam hasa ukichukulia kuwaWaislam ni wengi nchini Tanganyika. Waislam wa Tanganyika walikataa kuiungamkono AMNUT wakihisi sera zake zilikuwa za kuwagawa watu kwa misingi ya dini.Kwa ajili hii basi AMNUT haikuwa na maslahi ya wananchi. Lakini pigo kubwa kwa AMNUT lilikujakutoka kwa masheikh wa Tanga. Masheikh na waalimu wa Qurían mjini Tanga walitiasahihi azimio la pamoja kuipinga AMNUT. Azimio hilo lilisema kuwa AMNUT ingezuajanga.
Mohamed
Kwa maelezo ya Mohamed, baraza la wazee ndilo lilifanikisha safari ya kwanza ya mwalimu UN mwaka 1955.
Hadi mwaka 1963 baraza hilo lilikuwa la waislam tupu likiwa na idadi ya wajumbe 170.
Mwenyekiti wa baraza alikuwa sheikh Takadir, sina uhakika mwenyekiti wa chama cha TANU na rais hakuwa mjumbe!
Kwa vile lilikuwa na wajumbe 170 waislam watupu, na kamati kuu ilikuwa na asilimia 98 waislam watupu, ilikuwaje vyombo vyote viwili vyenye nguvu katika chama na serikali kuzidiwa nguvu na Nyerere peke yake kwa ushawishi wa kuvunja baraza. Je, ni Nyerere au ni waislam wakishirikiana na Nyerere waliovunja baraza la wazee la TANU. Ufafanuzi tafadhali
Namshukuru Mungu asiye na DINI. Kwenye sikukuu ya jana ujinga huu wa watu kubaguana, kuonewa, sikuuona wala kuusikia. Misikiti ilipambwa kwa kanzu na makoti ya bei mbaya. Mambo mengi alioyaandika Mohamed yalishapitwa na wakati. Yanapaswa kuwa historia kama yalikuwepo kweli.
hapa inabidi utupatie ufafanuzi. Katika maandishi yako mengine huko nyuma ulisema kuwa Waislamu hawakuwa na tatizo na Nyerere kabla ya 1963 na kuwa ilikuwa ni 1963 pale Kamati Kuu ya TANU ilipovunja baraza la ushauri la wazee wa TANU lililowahi kuongozwa na Shehe Takadir na ambalo lilikuwa na Waislamu watupu. Lakini unasema AMNUT mwaka 1959 iliundwa kwa ajili ya maslahi ya Waislamu. Ina maana kabla ya 1963 na kusema kweli 1959 tayari kulikuwa na kundi la Waislamu ambalo lilikuwa linaona linakandamizwa na Wakristu. Sivyo?
Hata hiyo DHULMA sijui ni kwa lipi! Hiyo 83% kwa 17% nayo ni utata mtupu. Fafanua Mohamed. Ni katika yapi hasa, haya:WC,
Hiyo ndiyo dua yetu sote.
Historia kwa hakika hii nielezayo ishapita linalotukabili ni hii dhulma dhidi ya Waislam ndiyo tunayoomba isifumbiwe macho.
83% kwa 17% si uadilifu hata kidogo.
Mohamed
Nasema hivii, "Mwamedi Saidi ameshindwa na kujaribu kwa kila namna kukwepa kujibu maswsali na hoja husika kuhusu maandishi yake mwenyewe. Ushahidi usiopingika unaonyesha kuwa Mwamedi Saidi ni msomi feki kwa vigezo vyote vya viwango na usomi unaokubalika kimataifa isipokuwa labda vile vya madrassah."
Hata hiyo DHULMA sijui ni kwa lipi! Hiyo 83% kwa 17% nayo ni utata mtupu. Fafanua Mohamed. Ni katika yapi hasa, haya:
-Vyeo, madaraka, ajira?
-Nafasi za masomo sekondari, vyuoni?
-Viwanja, ardhi?
- NGOs, vyama vya siasa?
-Magazeti, redio, Tv, globu?
-Idadi ya waumini?
- Uanzishwaji na uendeshaji wa shule, vyuo?
-Tufute BAKWATA, TEC, TCC?
Kakuchagua nani kupangia watu jinsi ya kuuliza maswali hapa JF? We kama huelewi kinachoulizwa tulia kaka zako wajibu.
Tunasubiri kwa hamu ili mradi zisiwe ni haki zinazofanana na hizi Cameron anazowaombea hawa jamaa. Zisiirudishe nchi yetu kwenye DINI na UDINI.
WC,
Kamati Maalum ya Maandalizi ya Makongamano ya Waislam Dhidi Mfumokristo Tanzania imetoa kitabu "Mfumokristo na Dhulma Dhidi ya Haki za Waislam Nchini" kitabu kimeweka yote hayo wazi.
Softcopy itawekwa humu ukumbini Insha Allah kwa manufaa ya wote.
Mohamed
MM,
Umeuliza swali la msingi kabisa.
Nakuomba ufanye subira usome darsa zima ndipo utakujakuelewa hali ya siasa ilikuwaje wakati ule.
Nimeanza na ugomvi kati ya Sheikh Suleiman Takadir na Nyerere mwaka 1958. Hiki kisa TANU wakikiogopa hata kukieleza halikadhalika Nyerere mwenyewe kikimtia hofu.
Baada ya kueleza sintofahamu ile nimekuja kueleza kuanzishwa kwa AMNUT 1959 na nimemalizia kwa kueleza jinsi Waislam walivyokabiliana na matatizo hayo yote.
Sasa nataka kuingia kwenye Muslim Congress 1962 uhuru ushapatikana 1961 na yaliyofuatia.
Nina hakika maswali mengi yatapata majibu ndani ya historia hii ambayo kwa hakika huijui.
Nakuomba vuta subira hadi tufike mwisho Insha Allah.
Mohamed
Wengine tumemsoma Mohamed miaka 20 iliyopita na tunamjua si kupitia mnakasha huu bali kwenye viwanja vingine.Ahali yangu,
Kwa mtu makini, Hata Nyerere mwenyewe alikipata kitabu chako (kwani kilitoka zaidi ya miaka miwili kabla kufariki kwake, na ninavyomjua Nyerere alivyokuwa msomi wa vitabu laazima atakuwa amekisoma) Lakini hakuthubutu kuandika kupinga maandiko hayo.Kwani aljua ni lazima atulie na kufanya utafiti kidogo kabla kujibu au alikubaliana na kilichomo ndanimwe.
Mimi nakushauri tuendelee na mnakasha huu kwani tuna kiu ya kutaka kujua mengi.
Watu wengi wanaokupinga mimi kwa masuala yao wanaouliza utaona ima hawajakusoma vizuri au kutaka kupinga sababu ya uchache wa elimu hususan hii ya utafiti lakini pia kuguswa na kusukumwa na udini. Kupenda dhulma iendelee huko Tanzania.
Challenge ambazo wote tumewapa nao basi wafanye utafiti na kuuweka hapa barzani lakini hawana jipya. Kwani kuna nyanja nyingi na motion nyingi wanazoweza kuandika utafiti wao. sasa zote kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza kile kilichosahaulika na kufichwa kwa nia ya kuandika historia iliyo sahihi.
WC,
Kamati Maalum ya Maandalizi ya Makongamano ya Waislam Dhidi Mfumokristo Tanzania imetoa kitabu "Mfumokristo na Dhulma Dhidi ya Haki za Waislam Nchini" kitabu kimeweka yote hayo wazi.
Softcopy itawekwa humu ukumbini Insha Allah kwa manufaa ya wote.
Mohamed
Wengine tumemsoma Mohamed miaka 20 iliyopita na tunamjua si kupitia mnakasha huu bali kwenye viwanja vingine.
Kama unakumbuka, Nyerere alipostaafu kila gazeti ndani na nje ya nchi, kila mwanasiasa kama Kambona, Fundikira, Katumbo Sanga n.k walitoa maneno makali sana ya kejeli dhidi yake. Hakuwahi kujibu tuhuma hizo kwasababu wakati mwingine ukibishana na Mjinga watu wanaweza wasielewe tofauti. Lakini pia Nyerere hana sababu ya kumjibu mtu kama Mohamed Said, dunia ndiyo inaweza kumjibia kama tuonavyo. Huyu ni moja ya wanasiasa maarufu wa karne wanaojulikana duniani, na ni haki kutojishughulisha na simulizi ziszo na majibu za Mohamed Said.
By the way, Nyerere ndiye mhusika alitakiwa afanye tafiti gani kumjibu Mohamed. Yeye amefanya kazi na Sykes hadi picha ya soksi ndeeeefu anayoongelea mtafiti Kiongozi Sheikh Mohamed kila siku ipo. Anayetakiwa kufanya utafiti ni yule aliyesimuliwa. Nyerere afanye ili iwe nini!!
Hivi inahitaji utafiti kumjibu Mohamed, tunahityaji taa ya kandili mchana maana mwanga uliopo hautoshi.
Ama kweli ukipenda chongo huita kengeza, licha ya wana jamvi kuonyesha udhaifu wa hali ya juu bado kuna watu wanaita masimulizi utafiti, sijui yale ya Dr Koch n.k tutaita nini.
Umeona jinsi tunavyovuta nyuzi zinazo contradict maneno ya mtafiti Sheikh Mohamed. Leo anaongea hili jioni neno lile lile analitolea maelezo tofauti. Mfano anasema AMNUT ilianzishwa kulinda masilahi ya waislam, halafu anasema waislam waliikataa kwasababu itakuwa udini.!!!????
Ahal wangu baru baru, rejea nyuzi uone jinsi Mzee wetu anavyojikanyaga. Hapa si pale gogo vivu, ni JF tunasoma maneno si mistari na tutakuwa naye samba samba ili kuhakikisha kuwa azma yake ya kuleta vurugu nchi haifanikiwi.
Endelea kukata kiu sisi tiulishakata kiu miaka 20 iliyopita kwa version ya english na kiswahili ,kwa makala Nasaha, Annur n.k. na wakti mwingine kumsikiliza mubashar, kama hatukumuelewa miaka 20 it is unlikely tutamwelewa leo.
Tunachojua, hakuna utafiti, ni hadithi za kusikia alizoshadidia na uongo uliopambwa kwa lugha nzuri mashallah. Tunachuja chuya na bahati mbaya mchele unaonekana kidogo sana.
Hatupingi simulizi zake na hutakatai anayosema, tunachokataa ni kile kisichokuwepo, au amekificha na uchochezi usio na shaka wa kutaka kulitumbukiza taifa katika matatizo kwa makusudi kabisa. Tupo naye ili historia isje muacha nje.