Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Fundi,
Mohamed anaamini TAA/TANU ilikuwa na WENYEWE. Sio hawa uloowataja hapa. Kigezo kikubwa kwake kilikuwa UISLAMU au hata jina tu la KIISLAMU. Naamini haya ni mawazo ya Mohamed na sio wazee wake hawa ambao walimkaribisha Mwalimu kwa moyo mkunjufu kama MTANGANYIKA mwenzao na sio MKATOLIKI wao WAISLAMU. Mwalimu asingeingia TAA na hatimaye kuwa Rais wa kwanza wa TANU ambayo inaangalia DINI ya mtu.
 
............Dini nikiwa na maana Uislam siku zote ilikuwa ndiyo nembo ya TANU penda usipende.

Mohamed

I feel the pain ya wazee wako...kwa hiyo wazee wako walitaka/tegemea TANU iwe na Mfumo-Islam? au?...ilikuwaje wakamkaribisha JKN Mkatoliki?...Je, walitegemea kumsilimisha au?...sasa napata picha kwa nini Sheikh Takadir alisema vile..., maana alikaribishwa mvaa kaptura na yeye akawakaribisha wenzake...ikawa songombingo...sawasawa?...nisahihishe pale nilipohisi sivyo...tupe darsa Brother MS
 
ngawetu.... Fundi mchundo. Tatizo ni kuwa simulizi hizi zimethrithishWa katika misingi ya chuki. Mfano Mohamed anAsema marhum mama yake alikuwa analia kwasababu mwanae ameonewa shule hakupewa nafasi. Juzi Mohamed kaja na habari kuwa mwanae kaonewa shuleni kwa sababu anauwezo. Na huyu mtoto naye atakua akiwa na concept hiyo hiyo.

Chuki tu hata akiona mpita njia. Mohamed anatueleza kuhusu mtoto wake alivyo kipanga huko shuleni na anavyofuatilia maendeleo yake. Hawaelezi watu wa Kilwa kuhusu sekondari iliyofungwa kutokana na wanafunzi kukimbia na madhara ya jambo hilo siku za usoni. Anachowasaidia nacho ni kuwachochea kuwa wanaonewa.

Cha kushangaza wale wanaodhaniwa wangeonelewa sana wanafanya vizuri tu na mfano ni familia ya Sykes.
Masimulizi yame base katika chuki ya mtu mmoja anayetaka kufanya chuki hiyo kama 'standard kwa taifa zima'. Kwamba Mohamed kaonewa shule basi hiyo ni 'symbol' ya dhulma dhidi ya Uislam. Haoni yule profesa aliyekwenda shule bila viatu kwasababu tu alifaulu tena jina lake ni Ramzani Mohamed. Kwamba huyu hawezi kuwa symbol ya mfanikio.

Chuki kwasababu tunaambiwa kamati kuu ya TANU ndiyo iliyovunja kamati ya watu 11 ya baraza la wazee ambalo lilikuwa na wajumbe 170. Wakati huo huo tunaambiwa Mwaikela peke yake alizuia jaribio la kuua EAMWS. Sasa hapa tujiulize kwanini mtu mmoja afanikiwe kumzuia Nyerere na watu 170+ washindwe!

Kwa mtafiti wa kweli angeanzia hapo kutafuta chanzo na si Nyerere.

Ukisoma makala za Mohamed kuna mahali ukristo upo kwa ujumla na pengine kuna ukatoliki. Vyote hivyo vinachomekwa kwa makusudi ili kuleta hisia za udini. Ni hisia hizo ndizo zilizofanya hao wazee uliowataja wasitajwe kama wapigania uhuru. Sio kuwa Mohamed hajui, la hasha lakini ni katika jitihada za kupotosha umma kwa kivuli cha dini.

Mohamed anasema wazee wake waliochangia UDSM hawaku enziwa, tukamuuliza je Bhoke alikusanya na kuhifadhi hizo pesa ameenziwa vipi? hana jibu. Fundi mchundo, tumeshaonyesha hadi wakina mama wa Kipare walivyopinga ukoloni achilia mbali huko Nyanza federation n.k. Lakini mtu akiwa umefundishwa chuki hawezi kuhubiri upendo, atatafuta njia za kweli na uongo ili mradi chuki itawale.

Ndiyo maana kuna wenzetu jamvini wanaimba nyimbo za Mohamed, lakini waulize yatokanayo na nyimbo utashangaa. Hawana majibu ila wameshashiba chuki.

Kama chuki zingekuwa zinafanyika vyumbani ahalan wahsalan, lakini zinapandwa katika jamii. Tukikaa kimya nasi tutakuwa chuki kwa jamii. Tukemee!!
 

kwa jinsi unavyosimuliwa...MATENDO ya wazee wako then ni questionable, si ya KIZALENDO na hayana mapenzi na Tanganyika...kama nia yao ilikuwa ndio kama unavyosimulia basi binafsi nina mashaka na uzalendo wao (hasa ukizingatia baadhi yao ni mamluki), pili walitegemea wapewe special attention na sasa wana wao wanatumia mgongo wa dini kuhalalisha matakwa waliyokusudia wazee wao...
 

Ogah,

Kwa kawaida mimi huwa sipendi kufanya mnakasha na mtu anaeonyesha lugha ya kijuvi.
Napenda mtu analeta hoja kiungwana kwa kutaka kujua au ananipinga...lakini kwa lugha hii huwa inanitoa raha ya kuhangaisha akili yangu kufanya majadiliano.

Jitulize halafu liulize swali hilo hilo kwa adabu Insha Allah nitakupa majibu.

Unajua haya maswali niulizwayo humu nishaulizwa mara nyingi sana tena na wajuzi wa siasa za Afrika na historia yake.

Na siku zote siku naondoka hunambia, "Unajua Mohamed umetufungulia mengi ambayo hatukuwa tunayajua."

Mohamed

 

Atawaambia "na nyie kaandikeni ya wazee wenu". Mohammed Said kashikilia kipande cha ardhi ambacho hayuko tayari kukubali hata nchi moja aachie. Katika kushikilia kipande hicho yeye hajali ukweli - kwani ukweli ni ule aliosimuliwa na wazee 'wake'. Hayuko tayari kuutafuta ukweli - isipokuwa ule unakubaliana na aliyoambiwa na wazee 'wake'. Hayuko tayari kuhoji kile alichokisia kwani kufanya hivyo ni kuwashuku wazee 'wake'. Hakubali kukiachilia kipande cha ardhi na hawezi kukiachilia kwa sababu kuachilia nchi hata moja itaondoa ile dhana aliyojijengea kuwa kazi yake ni ya kisomi.

Jambo pekee ambalo nimelipenda katika mjadala huu ni kuwa sasa anakubali kuwa histohisia aliyoandika:

a. Haijali hasa historia ilivyokuwa
b. Inategemea masimulizi yenye mrengo wa kidini
c. Haijali kama kuna hoja za kupinga kwani yeye hakuwa anazijali kwani hoja za kukubaliana naye tu ndio ameziingiza
d. Anakubali kuwa chuki ya kikundi cha Waislamu dhidi ya Nyerere haijaanza 1962/1963 bali ilianza siku ile Nyerere alipotambulishwa kwa wazee na wakajua ni Mkristu
e. Amekubali kuwa dhulma ambazo anazingumzia siyo matokeo ya Nyerere bali Ukoloni na Nyerere alijitahidi kuziondoa.
f. Amekubali kuwa sera za wakati wa Nyerere zilifungua mlango usiowakawaida ambapo vijana wa Kiislamu ambao wakati wa ukoloni wasingeweza kupata mafanikio ya kielemu. Kina Kapuya na wengine. Aliwahi kusema kuwa "Waislamu hawakunufaika na chochote" lakini sasa msimamo huo umebadilika kwani hawezi kusema hivyo bila kuulizwa kuhusu kina Shimbo na wengine ambao wengi walisoma bure chini ya sera za Nyerere.


Sasa japo haya ni kweli hawezi kuyakubali kwani kuyakubali ni kuachilia kipande cha ardhi. Sasa njia pekee ya kiufundi (technical strategy) ambayo amekuja nayo ni kudai kuwa "na nyie andikeni vya kwenu". Hataki kujibu hoja ambazo yeye kazitoa kwenye kitabu chake, hataki kujibu mambo ambayo yeye ameyadai wala kujaribu kuyatetea. Anatuzungusha tu akiulizwa ananukuu alichonukuu wiki iliyopita na ambacho alinukuu wiki moja kabla! Anatuzungusha kwenye nukuu zile zile bila kufafanua lolote japo anajua nukuu zenyewe ndio zinauliziwa! Mkimuuliza kuhusu Nyerere atawaletakwenye hotuba ya 1985; mkiuliza kuhusu ugomvi wa Nyerere na Waislamu atarudi kwenye 'kongamano la waislamu' la 1962! Mkiulize vipi kina Kambona na Rupia atarudi kwa Shehe Amri au Takadir. Mkiuliza kuhusu Kirilo Japhet atawaambia Tewa Said Tewa.

Hivyo mnabakia kuzunguka tu. Rudieni muone nukuu ngapi anazirudia rudia. Ni kuwa anawapeni uchaguzi mkubali bila kuuliza na muitikie kwa kumshangalia au mkibisha muende mkaandike vya kwenu. Yeye hataki kujibu hoja za kisomi ambazo anazitoa. Ni kwamba hana majibu lakini hataki kukubali kuwa hana majibu. Akikubali kuwa hana majibu kwenye maswali mengi (karibu 40) ina maana anakubali kuwa kitabu chake hakina hoja za ukweli na ile sifa yote ambayo amepewa na vyuo mbalimbali na majarida mbalimbali kumbe haina ukweli. Ameweza kuwashawishi hao watu wa nje kwa sababu wengi wao hawajui siasa zetu za ndani lakini hapa amekwama.

Amekwama si kwa sababu amekusudia kutuposha bali ni kwa sababu alipoandika alikuwa anaandika kutoka katika hisia zake zilizojengwa katika simulizi la historia ya wazee wake. Kama nilivyosema huko nyuma kwamba Bw. Said alienda kuandika kitu ambacho kilikuwa kinathibitisha hisia zake za kudhulumiwa Waislamu na Nyerere (japo wakati mwingine anajisahau na kutuambia ni dhulma za wakoloni) na kuthibitisha masimulizi ya wazee wake - ambao ni kundi la wale wazee wa 1958 waliomkataa Nyerere kwa sababu ya dini yake.

Sasa hawezi kuwapa kipande cha ardhi ambacho amesimamia kwa sababu akitoa kidogo tu mnaweza kukidai chote.
 

Brother MS,
Samahani kama nimekukwaza...nilikuwa naomba ufafanuzi... kama nimeelewa sivyo...nambie tu sivyo hivyo halafu uendelee kutoa darsa...
 

Nguruvi3,

Wewe si mgeni kwangu hata kidogo. Kwani kuna mjadala (faida za mungano kwa Zanzibar) tulichuana sana na kwa mantiki hiyo nakufahamu ujuzi wako na udhaifu wako. Pamoja na kuwa na lugha nzuri lakini una mapunguvu makubwa sana ya data na kusema mambo pasipo na uhakika na kutumia lugha za kubuni na visa visivyo na mashiko.

Nafikiri darsa nililokupiga kule la kiuchumi na sheria lilikuingia sana ingawa mara zote unakuwa sintofahamu.

Nikirudi kwenye mada hii. Wewe kama ulivyojinasibu tokea awali kuwa umemfahamu Mohamed said more than 20 yrs ago na umepitia vitabu vitabu vyake na kufanya nae majadiliano kwa kipindi kilefu tu. Lakini kwa mtu makini unaona wazi kuwa si mwelewa ima kwa kukataa kuelewa au unasumbuliwa na uhaba na ufinyu wa elimu hususan hii ya kiuandishi wa kiutafiti. Kwani ungekuwa makini na una mapenzi mema kabisa na nchi yako Tanganyika na kuipenda jamii yako ya wa Tanganyika najuwa kabisa ungekuwa nawe umetoa kitabu chako ambacho kitaeleza yale yaliyo bayana. Kwani siku zote kazi za kisomi kama ya Mohamed said haiwezi kupingwa ma mistari mia ya maandishi yako pasi na kufanya utafiti.

Kwa hili nakuhurumia sana kuona kuwa ulitendei haki taifa na wananchi wa Tanganyika katika kutaka kuandika historia ya kweli na kubainisha yale yaliyofichwa na kujificha katika historia hiyo. Kwa msomi kama wewe naomba uone aibu sana kusema kuwa unamfahamu mtu aliyeandika historia ya tanganyika kwa zaidi ya miaka ishirini na wewe unapingana nae ukiwa umejificha chooni pasi na kutoka barazani kupingana nae kimandishi kama alivyofanya yeye.

Lakini pia umejihidhirisha kuwa una uwezo mdogo sana au huna kabisa uwezo wa kufanya tafiti. Hilo umejipambanua pale uliposema kuwa hata baada ya kifi cha JKN akina Kambona, Fundikira na wengine walisema memngi sana magazetini. Ukiwa unafananisha mahojiano na utafiti pasi na kujua kuwa hivyo ni vitu viwili tofauti saaana.

nakushauri sikiliza au soma darsa la Mohamed said pasi na kusukumwa na hisia za udini wala kupinga bali soma kwa nia ya kutaka kuelewa. Hilo litakusaidia kujua wapi amekosea na wapi amepatia. Lakini kikubwa sana jua kipi kilikuwa mazingatio yake katika kuandika historia hiyo ambayo amejipambanua wazi na kutaka kuandika mchango wa wazee wake wa Kariakoo katika uhuru wa Tanganyika. Kama utaelewa hilo sidhani kama utamtaja hapo Bhoke Munanka, Abdallaha Fundikira na hata Rashid kawawa na wengine. Angalia yeye amejipambanua sana na asipomtaja mzee Rupia hapo uliza kwani huyo ni mmoja wa wakazi wa kariakoo.
narudia tena soma kwa nia ya kuelewa na si kwa nia ya kupinga na siku zote anaepinga basi anaonyesha ukweli upo wapi.Hilo litakuweka pazuri sana.

Huo ni ushauri wangu kwako.
 

"Hear much and put aside the points of which you stand in doubt, while you speak cautiously at the same time of the others:-then you will afford few occasions for blame. See much and put aside the things which seem perilous, while you are cautious at the same time in carrying the others into practice: then you will have few occasions for repentance. When one gives few occasions for blame in his words, and few occasions for repentance in his conduct, he is in the way to get emolument."
Confucian analect.
 

Ni vizuri kujua taratibu za kuandika historia hususan za kitaffiti. Historia yoyote inaongozwa na kipaumbele na motion. Unaweza ukaamua kuandika historia ya wahaya katika mchango wao wa uhuru wenu. hapa utazungumzia wahaya tu na kutaja wachache wasio wahaya atika kujenga hoja zako. Na vile vile kama alivyoamua kuandika Mohamed said kuhusu mchango wa wazee wake wa kariakoo katika Uhuru wa Tanganyika. Hicho kichwa cha habari au motion yake inajipambanua kuwa anaongelea watu wa Kariakoo ambao kwa wakti huo walikuwa mora than 95% walikuwa waislam. Nitashangaa sana hapa kama atamtaja Bhoke Munanka au Kiriro Japhet ambo si wakaazi wa Kariakoo.

Kutokana na motion yake utaona wazi ni lazima uguse uislam katika Historia hiyo kwani hata vikao vyao walikuwa wanafanyika kwenye madrasa n.k. Na kama kuna mtu ana motion nyingine labda mchango wa kanisa katika uhuru wa tanganyika (kama alivyoandika Padre Silvalon na kitabu chake '' Kanisa Katoliki na siasa za Tanzania bara 1953-1985) na kujikita zaidi katika hiyo motion yake.

Narudi pale kwanza ni vizuri watu wasome kwanza kichwa cha habari cha mwandishi wa mada na baadae kumsoma nini kusudio lake katika mada yake kabla kuanza kuchangia.
 

Fundi mchundo,

Nilitaka nikuulize je hao nirio RED walikuwa wakaazi wa Kariakoo au gerezani Dar es salaam?

Kwani Mohamed Said motion yake kuandika Histiria iliyosahaulika ya Mchango wa wazee wake wa Kariakoo na gerezani katikaUhuru wa Tanganyika.

Kwa maniti wa hicho kichwa cha habari cha utafiti wake asingeweza kabisa kuwagusa watu waliotoka nje ya dar labda kuwe kuna kitu kimefanyika au mkutano na kunasibishwa na motion yake katika kuweka huo utafiti.

Nawashauri msme vichwa vya habari kwanza kabla kuanza kuchangia.
 
Labda niwaulize swali kidogo. Hivi biography ni historia ya mtu/watu au historia ya NCHI? Kitabu kile cha Mzee Mohamed kina stahili kuwa historia ya wazee wake au ya nchi hii?
 
Kwa hiyo alichoandika Mohamed ni memoirs za wazee wake sio historia ya kudai uhuru wa Tanganyika ambayo ni pana zaidi na inawahusisha wengi zaidi na kiongozi wao tangu mwaka 1953 akiwa ni Mwalimu?
 

Yote hii ni kweli kabisa na umesema point nzuri. Lakini akijaribu kufanya hiyo ndio historia kamili ya kupigania uhuru wa Tanganyika tutamkatalia. Akidai kuwa yote ambayo anayesema yaliyotokea dar ni kweli 'tupu' tutamkatalia kama anapofanya hivyo anayaacha mengine yaliyotokea Dar au yaliyofanywa Dar. Akijaribu kuonesha - kama wengi mnavyojitahidi - kuwa Nyerere alikuwa na kitu kama 'supporting role' na siyo major and unique role tutawakatalia kwa sababu katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika nafasi ya Nyerere is unchallengable, unremovable, and absolutely unignorable! Andika historia ya Wahaya ukitaka au ya Watanga ukitaka au ya watu wa Gerezani au Songea. Thats alright usijaribu tu kuiandika bila kuonesha nafasi ya pekee ya Nyerere ambayo hao 'wazee wake' walilitambua na kuikubali. Nje ya hapo ni kujaribu kuwasimulia watu habari za Alfu Leila Uleila na kuwaaminisha kuwa ni simulizi la kihistoria kwa sababu tu miji ya Basra na Baghdad inatajwa au kwa vile Harun bin Rashid anatajwa!
 

La pili ambalo hutaki kuligusa ni jaribio la Mohammed Said - na unaweza kuliona kwenye kitabu chake - kuwa ni Waislamu ndio waliotaka Uhuru zaidi lakini Wakristu hawakutaka kwani walikuwa wananufaika na utawala wa mkoloni "Mkristu". Sasa hawezi kuonesha mchango wa Wakristu katika kugongana na Wakristu na akauelezea kwa sababu kwa kufanya hivyo hoja yake kuwa Waislamu ndio walipigania sana uhuru inavunjwa nguvu. Hivi umekisoma hiki kitabu cha Abdulwahid Sykes na "HISTORIA ILIYOFICHIKA"?
 
Labda niwaulize swali kidogo. Hivi biography ni historia ya mtu/watu au historia ya NCHI? Kitabu kile cha Mzee Mohamed kina stahili kuwa historia ya wazee wake au ya nchi hii?

Wewe soma ukisha soma kama kuna mapungfu uyaonayo, andika chako. Unaweza?
 

Nafikiri hili sio siri kuwa waislam walikuwa vinara wa kupigania uhuru wa Tanganyika ni ukweli usiopingika kabisa kwani ni moja ya kovu au athari ya ukoloni wa mwingereza huko Tanganyika.

Kumbuka kuwa Mwingereza alitumia divide and rule katika utawala wake. Kenya na Uganda kwa sababu kulikuwa na makabila machache alitumia kuwagawa kwa makabila. Na hicho mpaka leo kipo dhahiri shahir Kenya na Uganda ukabila umetawala. Kila kabila linajiona bora kuliko jingine.

Upande wa Tanganyika mbinu hiyo haikuwezekana kwa sababu kuna makabila mengi sana. Hapo ndipo alitumia mbinu ya UDINI. kwa kuifanya dini moja superior kuliko nyingine na hiyo kusababisha watu kuanza kudai uhuru wao. Angalia sehemu zote TANU ilizokuwa maarufu ni zile walizojikita waarabu na za waislam ndipo vuguvugu lilipoanza. Anzia morogoro, tabora, ujiji n.k.

Hilo ni kovu ambalo Tz inalificha na kusahau kulitafutia dawa tokea uhuru na sasa ndio limeshakomaa na linawatafuna kwa sana. Huwezi kusema hata siku moja tatizo la udini Tanganyika limeanza jana au leo bali ni la kihistoria na lipo kimaandishi.
 

MM,

Jitulize katika fikra na pitia upya kitabu changu.

"Leading role" ya Nyerere iko wazi sana na laiti nilngelikuwa mjinga kiasi cha kutaka kumshusha Nyerere ningelikiua kitabu na hakuna "scholar" yeyote angepoteza muda wake kukisoma na kukichukua kama ni kazi ya maana ya rejea katika historia ya Tanganyika.

Kilichowavuta wengi ni kwanza ile "role" ya wale ambao hawakutajwa katika vitabu vilivyokwishaandikwa na nafasi ya Uislam katika siasa za kikoloni.

Hivi vitu viwili ndivyo vilivyofanya kitabu kiwe cha maana.

Suala la mtu kukubali au kukataa ndiyo usomi wenyewe na ndiyo hilo lilonifikisha mimi hapa nilipo leo.

Nilikata historia rasmi na nikachagua kuandika historia ya wazee wangu na wala sijasema kuwa hiyo ndiyo "the history" hapana wengine wanaweza na wao kama nilivyofanya mimi wakaandika historia ya Tanganyika kwa mtazamo wao.

Hii itazidi kuimarisha rejea katika historia ya nchi yetu.

Soma hii hapa chini:

"Mwaka a 1986, miaka miwili kabla, baadaya takriban miaka ishirini na tano ya ukimya, Ally Sykes alikubali kufanyamajadiliano na mwandishi wa Kiingereza Paula Park. Park akachapisha majadilianoaliyofanya na Ally Sykes kuhusu ukoo wa Sykes na mchango wao katika historia ya uhuru wa Tanganyika.[1]Makala ile iliposomwa Ally Sykes akawa anapata simu kutoka kwa marafiki zake nakwa wafanyabiashara wenzake wakitaka uhakika kama yale yaliyoandikwa katikagazeti lile kweli yeye ameyasema. Haukupita muda mrefu, maofisa wa Idara yaUhamiaji walimtembelea Park na kumuomba aondoke nchini.Hivi ndivyo mambo yalivyo na mwandishiamekuwa akiulizwa maswali mengi na watu mbalimbali kuhusu ukweli ya yalealiyokuwa akiyaandika katika mchango wa Abdulwahid katika uhuru wa Tanganyika.Wasiwasi huu umekuwapo lau kama mwandishi amefanya rejea nyingi na za kutoshakutoka magazeti ya zamani, vitabu,majarida na kumbukumbu zingine za wakati waukoloni. Juu ya wasiwasi wote uliokuwapo hakuthubutu kujitokeza yeyote kupingayake mwandishi aliyoandika kuhusu historia ya Abdulwahid katika TANU na uhuruwa Tanganyika. Hata mwanahistoria wa CCM hakunyanyua kalamu yake. Hali hii yaCCM kuikataa historia yake na wakati huo huo ikidai kuwa haijaweza kuihifadhihistoria yake inatoa mvuto fulani kwa watafiti kutaka kujua kulikoni. Ukweli wakuwa CCM imeandika historia yake lakini hapo hapo imeonekana upo upungufumkubwa unaweka wazi suala la utafiti ufanywe na watafiti huru ili ukweli upatekujitokeza. Somo la historia ya uhuru wa Tanganyika bado lipo wazi kwa utafitizaidi."

Mohamed
 
Kwa hiyo alichoandika Mohamed ni memoirs za wazee wake sio historia ya kudai uhuru wa Tanganyika ambayo ni pana zaidi na inawahusisha wengi zaidi na kiongozi wao tangu mwaka 1953 akiwa ni Mwalimu?

WC,

Kabla kuandika kitu ni lazima utafute unataka kuandika nini? na baada ya kujua unataka kuandika nini ndipo unapo tafuta kichwa cha habari. Kisha maandiko yako yote yatajikita na kile kichwa chako cha habari.
Mfano Padre Silvalon aliandika kitabu chake cha siasa za tanzania bara na kanisa katoliki na akajikita zaidi kuanzia mwaka 1953-1985. Aliikiiita Kanisa Katoliki na siasa za Tanzania Bara 1953-1985. Sio kuwa kanisa hilo lilianza mahusiano ake na Tz Bara mwaka 1953 au lilivunja mahusiano yake 1985. Bali yeye alijikita katika kipindi hicho na kufanya utafiti wake na kuandika kitabu chake.

Vile vile Mohamed Said amejikita zaidi kuandika historia iliyofichika ya wazee wake wa Kariakoo katika uhuru wa tanganyika. Sasa si rahisi yeye azungumzie uhuru wote na wote walioshiriki hata wale kutoka bukoba, mara au hata mbeya na songea. yeye amejikita zaidi kwa watu wa kariakoo.

Huo ndio msingi mkuu wa uandishi ni lazima uwe na mada. na maandiko yatazunguka kutokana na mada yako.
 
Kwa hiyo alichoandika Mohamed ni memoirs za wazee wake sio historia ya kudai uhuru wa Tanganyika ambayo ni pana zaidi na inawahusisha wengi zaidi na kiongozi wao tangu mwaka 1953 akiwa ni Mwalimu?

WC,

Nimeandika "memoirs" (kumbukumbu) za wazee wangu kuhusu TANU na harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

"Style" niliyotumia ni "biographical approach."

Mohamed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…