Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Mzee, katika orodha uliyoweka hapo ya mawaziri umewataja sita, kama nimekuelewa vizuri, baraza lilikuwa na mawaziri 15. Sasa hapo ungependa iweje?! Wangekuwa wangapi ndo iwe sawa? Unaweza kutuwekea hapa mawaziri 9 waliobaki?
 


Kasema, hajasema, alisikika, hajasikika. Hapo mwenyewe unajiona ndio unachambuwa kweli kweli. Tewa alikuwepo? Tewa alishika hizo nyadhifa?

Hilo moja linakutosha maana zingine umemwaga pumba, hivi wewe umewahi kuandika hata insha?
 
Kasema, hajasema, alisikika, hajasikika. Hapo mwenyewe unajiona ndio unachambuwa kweli kweli. Tewa alikuwepo? Tewa alishika hizo nyadhifa?

Hilo moja linakutosha maana zingine umemwaga pumba, hivi wewe umewahi kuandika hata insha?
Haya ndiyo mambo tunayokataa humu ndani...! Nguruvi kamjibu MS kwa hoja. Sasa tabu iko wapi kwako wewe FaizaFoxy kupita hoja za Nguruvi na kuonyesha jinsi kila hoja yake ilivyojaa pumba? Ukifanya hivyo utakuwa umemsaidia Nguruvi , MS na sisi sote humu ndani.
 

Nguruvi3,

Inasemekana jamaa keshawasili.

Na hapo nishazungumzanae na kaniambia keshafika.
Nitakapomueleza mtu kuwa jamaa amewasili nitasema, "Inasemakana jamaa keshakuja."

Hivi ndivyo tunavyozungumza watu wa pwani.
Hii ndiyo nama yetu ya kuongea.

Ziangalie hizo "inasemekana" ziko nyingi.

Makala za Mwananchi zimekuumeni sana.
Taarifa zimenifikia.

Makala zile zimeninyanyua hata sikutegemea na zote walichapa.

Nimepewa mradi mzito wa "documentary."
Mengine sina haja ya kujibu.

Mohamed
 
kwenye bold ...hayo ni mambo 'mepesi'.

Google inaleta video nyingi sana za mohamed said lakini siyo huyu...! labda ustaadhi mwenyewe atusaidie nadhani anaweza aka nazo kwenye hazina yake.

Sweke34,

Kama uko Dar es Salaam pita msikiti wowote Kariakoo wanakuwa na sehemu wanauza vitabu na DVD utapata DVD zangu hii ndiyo njia nyepesi maana ya "google" inakuwia tabu kidogo.

Nikipata link nitakurushia Insha Allah.

Mohamed
 
Bwana Mohamed ni jinsi kichwa cha habari chenyewe kilivyo ndiyo maana hali kwenye mjadala huu iko hivi. huwezi amini mimi kwenye zile makala zako kwenye ile thread yako nimechangia mara moja tuu, kwani kama siziamini makala zile sina budi kuandika za kwangu. Lakini Hapa umekosolewa kwa makala zile ndiyo maana kuna wanaomuunga mkono aliyekukosoa na wapo wanaompinga. Wakosoaji (Critics) hawana ulazima wa kuandika vitabu ili wafikie viwango vya kuitwa wakosoaji. Wakosoaji ni wakosoaji na si waandikaji, kwani waandikaji nao ni waandikaji na si wakosoaji.

Wewe kwa majisifu yako kwamba unaingiliana sana na watu wa Magharibi bila shaka unaelewa kwamba si kila anayekaribishwa ulaya ni mtu anayefaa. Mashoga wa Uganda walikaribishwa kwa mbwembwe, vifijo na nderemo walipokwenda Marikani kuelezea jinsi wanavyo "kandamizwa" nchini kwao. Vipi mashoga hao wakikwambia "kama huamini sisi tuna haki nenda kaullize ulaya ambako tumeshatoa mihadhara zaidi ya 50 kwenye vyuo vikuu mbali mbali vya huko". Kwa mtazamo wako Ushoga ni kitu halali kwa sababu tu mashoga hao wa Uganda walikwenda ulaya na marikani kutoa mihadhara kwenye vyuo vikuu vya nchi hizo?

Mimi sikosoi bali namuunga mkono aliyekukosoa wewe na ukosoaji wake ni kitu kipya wala haigi maandishi yako bali ameandika ya kwake kwa tafakuri inayotokana na udhaifu wa kwenye maandishi yako. Mag3 ni Critic.
 


Tena kuna kijana wetu wa Lumumba pale ni mkali kweli wa "ma video" na ametoka Canada baada ya kwenda kuchukuwa ujuzi zaidi, atakuwa msaada mkubwa sana wa kutayarisha "documentary" ntakupa namba zake kwa pm. Unamjuwa sana tu.
 
Kumbuka kuwa hilo ni vazi pia la mapadri na hizo hijab pia huvaa ma nun. Zisikustuwe sana.

Yaani kwa ukigeugeu wewe ni balaa!! Yaani leo Kanzu na Hijabu unayaona ni mavazi tu ya kawaida, wakati huko nyuma mavazi hayo hayo uliyahusisha na Uislamu!!??i

Pia unapenda sana kurekebisha mabandiko ya wenzio lakini na wewe hujanusurika kukosea. Ukisema "hizo hijab pia huvaa ma nun" unamaanisha kwamba ma nun (watawa?) ndiyo huvaliwa na Hijab. Ungeaandika "hizo hijab pia huvaliwa na ma nun" ni ushauri tu ndugu yangu kwamba ukirusha mawe kwenye nyumba ya mwenzio wakati ya kwako ni ya kioo, JIANDAE!!
 
Heshima kwako Nguruvi3.

Mkuu wangu haya maswali sitegemei kama Sheikh Mohamed Said atayajibu kwasababu ajenda yake ya kutugawa waTanzania kwa misingi ya Imani itakufa kifo cha mende.Ni vyema mjadala ukafungwa kwakuwa MS hana majibu ingawa anajisifia maandiko yake yapo Marekani na ulaya ajabu anashindwa kujibu nondo za uhakika hapa JF.Kwa maneno rahisi JF ni kiboko wapo magreat thinker uwezi leta upupu ukashangiliwa kama bi harusi.



 
kwenye bold ...hayo ni mambo 'mepesi'.

Google inaleta video nyingi sana za mohamed said lakini siyo huyu...! labda ustaadhi mwenyewe atusaidie nadhani anaweza aka nazo kwenye hazina yake.

Sweke34 unamtoa rangi mwalimu wa spelling hahahah aibu!
 
Sweke3,

Ni "publish" siyo "public."

Maana ya usemi huu ni kuwa kama hutoandika hutokuwepo.

Katika minakasha hiyo wote hapo wajuzi wana vitabu na "papers" lukuki.
Maswali wanayouliza si kama haya yenu.

Mohamed

hili laweza kuwak kweli kabisa kwa sababu wanakuuliza the wrong questions..!
 

Unakosea tena. Zuberi Mtemvu alikuja baadae, Katibu wa kwanza alikuwa Denis Phombeah ambae alikuwa Meneja wa ukumbi wa Arnatoglou. Zuberi alikuja baadae kama alivyokuja Oscar. Oscar Kambona alikuwa wa kwanza aliyekuwa mwajiriwa full-time. Denis Phombeah alikuwa mnyasa na mkristu kama alivyokuwa Oscar, ndiyo maana unapata ugumu kutambua nafasi yake.


Baraza la TANU halikutawaliwa na waislamu. Waislamu walikuwa wengi, ndio, lakini haina maana kuwa waliwatawala wasio waislamu. Kama uliwajua wakina Julius Nyerere, Oscar Kambona, John Rupia, Denis Phombea, bila shaka utakiri kuwa hawa hawakuwa watu wa kuburuzwa. Vile vile tofauti na unavyotaka kutupotosha, hao waislamu hawakuwa bloc bali waligawanyika katika makundi. Wako pengine ambao walitanguliza uislamu wao lakini wengi zaidi walitanguliza utanganyika na ndio maana hoja za wakina Nyerere ziliweza kukubaliwa na kufanyiwa kazi.

Ukweli ni kuwa pamoja na wakina Barubaru kutaka kupunguza sumu ya hoja yako bado ukweli unabaki kuwa unaongozwa na chuki dhidi ya wakristu, haswa wakatoliki na ajenda yako ni kuamsha simanzi ya waislamu wawachukie. Kwako wewe haijalishi mchango wa mtu, cha muhimu ni dini yake. Hakuna mtu anayepinga mchango wa hao unaowaenzi katika taifa letu lakini tunaachpinga ni kuwafanya kuwa walikuwa peke yao na wengine wasio wa dini yako walikuwa wapambe tu! Hauwezi leo kuandika historia ya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini bila kuwataja wakina Ruth First, Nadine Gordimer na wengine wengi ambao walikuwa weupe walikuwa tayari kuweka maisha yao rehani kudai haki kwa ajili ya mtu mweusi. Kwa vile tu muingereza aliyetutawala alikuwa dini moja na Oscar haiondoi na haibadilishi mchango wake katika mapambano dhidi ya utawala ule.

Unakotaka kutupeleka ni kubaya na ndio maana hatutakukubalia utuburuze huko maana hatuna ankal Doha wa kukimbilia mambo yakiharibika.

Amandla.......
 

Ngongo,

Huwezi kuwa "great" kwa kutamani.
Huwezi kuwa "great" kwa kuuliza maswali ya vichekesho.

Unakuwa "great" kwa kuonyesha uwezo wako katika hicho unachokisemea.
Na hakuna njia ya mkato.

Lazima kuuendea u "great" uandike kwa uchache "paper" moja mbili watu wakusome.
Ikiwa uloandika yana maana utaona unaalikwa katika makongamano na mikutano...

Hatua inayofuatia unaandika kitabu...

Tuishie hapa nadhani ushaipata picha...
Huwezi kuwa "great" JF.

Na kuwa "great" ni kitu kinaweza kikakuchukua umri wako wote.

Mohamed
 

Fundi Utumbo,

Ungeliandika kitabu ingelikuwa raha kweli kweli maana sasa mie na we sote tungekuwa tunasomwa pamoja.
Vinginevyo...

Mohamed
 
Mimi ni mtu wa pwani pia, usitake kuwadanganya watu. Baada ya kuona aibu sasa unalitafutia neno hilo maana ili likuondoe na aibu ya hisia ambayo imekuchafua. Neno hili halitumiki kama unavyosema na hapa manguli wa kiswahili wanabaki wakicheka sana jinsi mzee mwenzao ulivyopelekwa kona na unavyojiuma uma.

Lakini kama umeleitumia kwa maana unayosema bado linakuumbua sana. Linaonyesha kuwa kazi yako ya uandishi haizingatiii lugha. Mwandishi anatakiwa awasailiane na hadhira yake bila tatizo la mawasiliano. Njia mojawapo ni kutumia lugha inayoeleweka kwa wote, sio lugha ya mitaani. Sasa kama wewe umelitumia kwa ajili ya watu wa kisiju, Nanjilili, Mjasani , Maneromango hajui hadhira unayotaka kuifikia. Kosa la uandishi na ushahidi wa ubabaishaji.

Maswali wanayokuuliza ulaya hawana background. Hawajui kuwa Tewa alikuwa msaliti kwa waislam wao wanajua Tewa kakuachia makabrasha ya maana. Wanakuuliza kuhusu Nyerere na wewe unawamwagia chuki uliyo nayo dhidi yake kama ya babu yako aliyeendesha mgomo.
Maswali ya wana JF huyawezi kwasababu utatudanganya nini kuhusu mwembechai, kariakoo, Nyerere, Rupia, Kawawa, TANU, TAA n.k.

Kama alivyosema mmoja wetu ukitia mkuu JF usitegemee vigelegele na zumari kama kigoli anayechezwa ngoma mkamba kisiju.
Gogovivu mashalah watakubusu mkono uwanunulie gahwa, hawajui kinachoendelea masikini sio JF

Jibu hoja na maswali hatuhitaji bla blah.
 

Fundi Utumbo,

Ungeliandika kitabu ingelikuwa raha kweli kweli maana sasa mie na we sote tungekuwa tunasomwa pamoja.
Vinginevyo...

Mohamed

Hatuwezi wote kuwa waandishi. Na si maandishi yote yanastahili kuheshimiwa na/au kukubaliwa. Kitabu kimoja kinachofanana na chako ni Mein Kampf ambamo mwandishi alielezea historia yake na imani yake. Na kama ilivyo kwa kitabu chako, kilikataliwa na kupingwa na wale wanaoutakia mema ulimwengu wetu!

BTW, Salman Rushdie yuko katika maktaba zote ulaya na anaheshimiwa sana katika akademia. Kwa mtazamo wako basi huyu nae kwa vile amesomwa na wengi na ametoa mada katika majukwaa makubwa, anastahili kuenziwa na jamii yetu!

Amandla.....
 
MS

Endelea kutoa darsa, hawa jamaa wanaojiita critics hawana maswali ya maana zaidi ya kashfa.

Kuna watu wengi wanasoma hii historia. Tunaomba uendelee kutupa vitu.
 

Du!
Mbona umenzindua sikuwa na khabari kama JF ina hadhi kubwa kiasi hiki ingawa bado hatujatoa "paper" hata moja.

Mie hanitoi mtu humu.
Naiweka katika CV yangu.

Sasa jamaa watanikoma.

Mohamed
 
MS

Endelea kutoa darsa, hawa jamaa wanaojiita critics hawana maswali ya maana zaidi ya kashfa.

Kuna watu wengi wanasoma hii historia. Tunaomba uendelee kutupa vitu.

Mr Right,

Si utani historia hii niloandika imewavuruga sana jamaa zetu.

Mohamed
 

Fundi Utumbo,

Ungeliandika kitabu ingelikuwa raha kweli kweli maana sasa mie na we sote tungekuwa tunasomwa pamoja.
Vinginevyo...

Mohamed

MS,

Wasio upande wako au wasiokubaliana nawe ndio wanapaswa kuandika vitabu au "papers" ili ukubali hoja zao au iwe "raha kweli kweli" lakini wanaokubaliana na wewe au wanatetea hoja hizi za udini hao hilo la kuandika vitabu or papers haliwahusu. Double standards? Au ndio "mfumo mbadala"? Waulize pia hawa wanaotetea hoja zako za "mfumo kristo" "Uovu wa Nyerere" na Historia ya wazee wako, vitabu au "papers" zao ziko wapi?

Ikishindikana basi hii hoja yule anayehoji unachotaka kutuaminisha anaambiwa kuandika kitabu/vitabu/papers itakuwa haina maana na mjadala undelee na maswali yajibiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…