Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Hapo umekosea. Nyerere hawezi kuwa Baba wa Taifa kwa Waislamu. Waislamu hatumwiti mtu "Baba" kwa "utakatifu" wake anaopewa na Kanisa.

Waislamu hatuna cheo cha "Baba" unless ni baba yako mzazi. Kwa watu wa Pwani ni TUSI kumwambia mtu amwite mtu fulani "Baba" yake wakati si " Baba" yake mzazi. Kwa hiyo rekebisha hiyo lugha.
Kwenu tafsiri ya neno baba imeishia hapo kweli? Halafu ni ulimbukeni kudhani wote tuliomo humu si watu wa pwani. Mimi nimemwambia MS kwamba kama wao walikuwa wanazaliwa majumbani siye wengine tumezaliwa Ocean Road Hospital.kwa sababu nampinga MS miye si mtu wa Pwani?
 
-------
Hoja ilikuwa ni kama Mkwawa alikuwa ni Muislam au la, na wala hoja haikuwa mkwawa alipataje utawala wa Wahehe. Kuna wengi sikuwataja kama kina Mayagila, mdegela, Mdemu na wengineo. Inshaalah watakuwemo kwenye Historia fupi ya Mkwawa.

Kigarama,

Mwananchi la 24 Novemba kuna makala ya Charles Kayoka anasema Mkwawa hakuwa Muislam lakini akiandika kwa irabu za Kiarabu uk. 4 na ameweka na picha ya moja ya barua hizo.

Hebu gonga kichwa kidogo hapo.

Mohamed
 
Na mpaka leo umeshindwa kuonesha kuwa alikuwa sio Muislaam.
 
-------

Kigarama,

Mwananchi la 24 Novemba kuna makala ya Charles Kayoka anasema Mkwawa hakuwa Muislam lakini akiandika kwa irabu za Kiarabu uk. 4 na ameweka na picha ya moja ya barua hizo.

Hebu gonga kichwa kidogo hapo.

Mohamed

Baba yangu mzazi alikuwa akiandika kwa irabu za kiarabu, alivaa kanzu na kofia, na pia aliweza kuongea kiasi (fairly) kiarabu na bado alikuwa mpagani mpaka kifo chake.........watoto wake tumegawanyika wengine bado wapagani, wengine Waislam na wengine ni Wakristo
 
Ogah,

Utafiti kwa kawaida unaongozwa na "general rule" siyo "exceptions."

Ndiyo mara kwa mara nasisitiza watu kusoma hivi vitu na kujua sheria zake.

Kuhusu mzee wetu kwa kweli kuna mengi ya kujiuliza kwani mtu hajinasibu kwa upagani.
Si sifa.

Upagani ni ujinga "jahilia."
Sasa mtu aliyesoma kwa kiwango hicho na kuonekana muungwana vipi atakuwa jahil?
Panatakikana maelezo ya kina.

Mohamed
 
Sheikh Mohamed, sidhani kama Ogah anaijuwa hata maana ya ujahilia.
 
Mohamed Said,

..hapo ulipoita "wapagani" wajinga ni kutokana na mafundisho na malezi yako.

.."wapagani" nao kwa upande wao wanawaona Waislamu,Wakristo,etc etc watu wasiokuwa na maana.

..sasa who is right, and who is wrong kuhusu hizi imani[dini], uwepo au kutokuwepo kwa MUNGU, hakuna kati yetu mwenye majibu ya kuweza kumtosheleza mwenzake.

..sidhani kama inapendeza ku-label watu wa imani fulani wajinga.

..tujitahidi kuheshimu imani za wenzetu.
 
Ogah,

Utafiti kwa kawaida unaongozwa na "general rule" siyo "exceptions."

Ndiyo mara kwa mara nasisitiza watu kusoma hivi vitu na kujua sheria zake.

Kuhusu mzee wetu kwa kweli kuna mengi ya kujiuliza kwani mtu hajinasibu kwa upagani.
Si sifa.

Upagani ni ujinga "jahilia."
Sasa mtu aliyesoma kwa kiwango hicho na kuonekana muungwana vipi atakuwa jahil?
Panatakikana maelezo ya kina.

Mohamed
Mohamed,
Unakosea unaposema kuwa upagani ni ujinga. Hawa pia wana taratibu zao za kuabudu na miiko yao kama walivyo wakristo na waislamu. Wanaamini Mungu au miungu wao. Bahati mbaya ni kwamba hizi imani hazijawekwa kwenye maandishi kama walivyo wakristo na waislamu lakini laiti yangekuwepo maandishi yanayosimulia imani na kanuni za upagani usingewabeza hata kidogo. Hizi ni imani za asili kama walivyo wa Budha wa India na Shinto wa Japan. Kulikuwepo mzee mmoja, mdogo wa babu yangu akija pale kwetu nyumbani kunapokucha anasali aki adress jua. Jioni kunapokuchwa anatoa sala nyingine akilishukuru jua kwa mwanga na uhai. Nilikuwa namwangalia kwa kustaajabu lakini nilikuwa mdogo. Ningekuwa na uelewa nilio nao hivi sasa ningekaa naye kitako nijue ni kitu gani anachoamini. Alikataa kata kata kubadilishwa kuwa Mkristo licha ya kwamba baba yangu alikuwa kasisi.
 
Kwa hiyo "wazee wetu" waliopigana na walioogoza vita ya maji maji na falsafa yake ya kipagani tuwaite "wajinga". Kama sio wajinga hii falsafaya maji maji ni ya dini gani ?

kama ni wajinga unaonaje kwenye hsitoria yako mpya aliyoficha nyerere tukifunua na kifuchua ujinga wao wazee wetu hawa wa kipagani waiopigana vita kwa misingi ya kipagani.
 
Fahari,

Mimi sina taarifa kuwa falsafa ya majimaji ilikuwa ya kipagani.
Tafadhali nielimishe.

Mohamed
 
Mohamed,
Unakosea unaposema kuwa upagani ni ujinga. Hawa pia wana taratibu zao za kuabudu na miiko yao kama walivyo wakristo na waislamu. Wanaamini Mungu au miungu wao. Bahati mbaya ni kwamba hizi imani hazijawekwa kwenye maandishi kama walivyo wakristo na waislamu lakini laiti yangekuwepo maandishi yanayosimulia imani na kanuni za upagani usingewabeza hata kidogo. Hizi ni imani za asili kama walivyo wa Budha wa India na Shinto wa Japan. Kulikuwepo mzee mmoja, mdogo wa babu yangu akija pale kwetu nyumbani kunapokucha anasali aki adress jua. Jioni kunapokuchwa anatoa sala nyingine akilishukuru jua kwa mwanga na uhai. Nilikuwa namwangalia kwa kustaajabu lakini nilikuwa mdogo. Ningekuwa na uelewa nilio nao hivi sasa ningekaa naye kitako nijue ni kitu gani anachoamini. Alikataa kata kata kubadilishwa kuwa Mkristo licha ya kwamba baba yangu alikuwa kasisi.

Jasusi,

Ahsante kwa mawazo yako.
Mimi naomba kujitoa katika huu mjadala wa upagani.

Waislamu tumeonywa na Allah kuwa tujiweke mbali pale Mungu atakapofanyiwa shere.
Sasa hii ni post yangu ya mwisho kuhusu somo hili.

Tuendelee na historia ya uhuru.

Mohamed
 
Mohamed Said,

..hapo ulipoita "wapagani" wajinga ni kutokana na mafundisho na malezi yako.

.."wapagani" nao kwa upande wao wanawaona Waislamu,Wakristo,etc etc watu wasiokuwa na maana.

..sasa who is right, and who is wrong kuhusu hizi imani[dini], uwepo au kutokuwepo kwa MUNGU, hakuna kati yetu mwenye majibu ya kuweza kumtosheleza mwenzake.

..sidhani kama inapendeza ku-label watu wa imani fulani wajinga.

..tujitahidi kuheshimu imani za wenzetu.

JK,

Basi naomba radhi.
Nishajitoa katika mjadala wa "upagani."

Tuendelee na historia ya uhuru.

Mohamed
 
JK,

Basi naomba radhi.
Nishajitoa katika mjadala wa "upagani."

Tuendelee na historia ya uhuru.

Mohamed
Pamoja na kujitoa. Ukristo na Uislamu ni ujinga zaidi. Hizi tamaduni na mila za watu wengine kabisa. Tumezipokea, tumezikumbatia kichwakichwa. Zinatugawa. Zinatutenga. Zimetuweka mbali na mila na desturi zetu. Sasa tunataka ziingie hata kwenye siasa na uendeshaji wa nchi yetu. Wapagani tupo. Hatutakubali.
 
Jasusi,

Ahsante kwa mawazo yako.
Mimi naomba kujitoa katika huu mjadala wa upagani.

Waislamu tumeonywa na Allah kuwa tujiweke mbali pale Mungu atakapofanyiwa shere.
Sasa hii ni post yangu ya mwisho kuhusu somo hili.

Tuendelee na historia ya uhuru.

Mohamed
Duh...naona promotion ya vitabu bado inaendelea. Nataraji na mauzo yatakuwa si haba vilevile! Sasa mkuu inabidi uanzishe na ka Foundation/Asasi hivi... Mohamed Said Foundation for Muslims______.
 
Fahari,

Mimi sina taarifa kuwa falsafa ya majimaji ilikuwa ya kipagani.
Tafadhali nielimishe.

Mohamed

Falsafa ya majimaji haikuwa ni ya kipagani. Yale yalikuwa ni maji ya ZAMZAM yaliyopatikana kwa waliokuwa wamekwenda Makka kuhiji. Kwa vile ni maji ya baraka yalitumika kuwapa ujasiri wapambanaji.Lakini historia ilioptoshwa ilipoandikwa kuwa eti yalikuwa ni maji ya kichawi.
 
Pamoja na kujitoa. Ukristo na Uislamu ni ujinga zaidi. Hizi tamaduni na mila za watu wengine kabisa. Tumezipokea, tumezikumbatia kichwakichwa. Zinatugawa. Zinatutenga. Zimetuweka mbali na mila na desturi zetu. Sasa tunataka ziingie hata kwenye siasa na uendeshaji wa nchi yetu. Wapagani tupo. Hatutakubali.

Kwa Ukristu sijui, lakini Uislam sio utamaduni wa waarabu kwa sababu Mtume Muahammad (SAW) alipoanza kutangaza Uislam karne kadhaa zilizopita aliwakuta waarabu wakiwa ni wapagani kama walivyo wapagani hapa Tz,wakiabudu masanamu na mizimu,hawakuwa na sheria,mwenye nguvu ndo alikuwa na haki.Walimpinga sana kwa kuingilia utamaduni wao.kwa ufupi ni kwamba ulikuwa ni utamaduni wa kijinga.Kwa maana hiyo basi unapo husisha Uislam na utamaduni wa waarabu nitakupinga mpaka kesho
 
Dah!....Brother MS umeita utamaduni ulionikuza mimi ujinga? Sheikh nitake radhi tafadhali.....
 
Kwa Ukristu sijui, lakini Uislam sio utamaduni wa waarabu kwa sababu Mtume Muahammad (SAW) alipoanza kutangaza Uislam karne kadhaa zilizopita aliwakuta waarabu wakiwa ni wapagani kama walivyo wapagani hapa Tz,wakiabudu masanamu na mizimu,hawakuwa na sheria,mwenye nguvu ndo alikuwa na haki.Walimpinga sana kwa kuingilia utamaduni wao.kwa ufupi ni kwamba ulikuwa ni utamaduni wa kijinga.Kwa maana hiyo basi unapo husisha Uislam na utamaduni wa waarabu nitakupinga mpaka kesho
Kwani huyo Mtume Mohamad( SAW) alikuwa Mzaramo, Mkurya? Hiyo mizimu na sanamu ndizo zilikuwa DINI zenyewe Mohamad( SAW) na Yesu Kristo walifanya maboresho tu kama ambavyo akina Mzee wa Upako, Kakobe, Mwingira,..., wanaboresha Ukristo sasa.
Msitusumbue na DINI zenu hizi za kuletewa. Fanyeni haya kama mambo binafsi na Mungu wenu.
 
Back
Top Bottom