Historia Yangu yenye kujaa ukakasi na uhusiano wangu na Member huyu wa JF

Nimezaliwa mwaka 1970, na kupata Elimu yangu ya Msingi hapa hapa Dar Es Salaam na Sekondary Nje ya Dar Es Salaam katika shule zinazomilikiwa na Makafir. Kiukweli ilikuwa changamoto kidogo kutokana na Mzee wangu kuwa ni mtu anayeshika sana Dini.

Kwa wale watu walioishi Kimanga, Mji Mpya watakuwa wanaufahamu Msikiti wa Ngunde. Mzee wangu alikuwa hakosi kuswali pale swala zote tano. Nakumbuka hata kipindi kile Sheikh Shariff Majini amekuja Kimanga mmoja ya watu ambao walisupport sana ile mihadhara alikuwa mzee wangu.

Mimi nmecheza mpira Uwanja wa Twiga nikichezea Twiga na akina Omary, Mluguru, Galabu n.k kwa wenyeji wa maeneo hayo watakuwa wanakumbuka.

Sheikh Shariff alifanya sana mihadhara ule Uwanja wa Twiga. Nilikuwepo kipindi hicho sehemu za mbele kabisa. Akina Mazinge watakuwa wananikumbuka pia sababu nlikuwa mtu wa imani sana. Mwaipopo na Abubakar. Hawa hawawezi nikumbuka.

Mzee wangu alikuwa ni mmoja ya wazee wenye kauwezo flani yale maeneo tukiwa na nyumba nzuri miaka hiyo yenye fensi. Na tulifanikiwa kwenda shule tofauti na wenyeji wengi ambao waliishia darasa la 7 au hawakumaliza shule. Sekondary O Level nlisoma ya Serikali na A level nikaenda ya Makafir.

Mimi nlikaa na wahuni... Ile mitaa ilikuwa na wahuni sana. Tukicheza mnanda, mchiriku n.k mpaka kipindi imekuja anzishwa team ya Begeju baada ya Twiga kuvunjika. Begeju ikawa ina wahuni wavuta bhangi na Twiga ya wastaarabu. Ilikuwa hizi teams zikikutana moto lazima uwake.

Leo hii nimefikaje hapa JF? Na wengi wananiona kama si Muislamu (nakubaliana nao) na huwa natamani sana niweze kuwa Mkristo ingawa bado sijaweza kuwa sababu ya aina ya maisha ambayo nimezoa na imani iliyonikuza. Huwa nawaambia watu mimi Role Model wangu kwa tabia zangu zote ni Muhamad. Huwa sitanii.

Lakini Elimu ilinisaidia sana kufunguka na kusoma kwa kureason hivi vitabu. Nlianza kusoma Biblia kwa lengo la kupata mistari ya kupotoshea Wakristo na kuwananga. Badala yake ikaanza kunifundisha vitu ambavyo vilianza kunifanya nione kuna maeneo mengi sikuwa sawa katika imani yangu ya awali.

Mzee wangu alikuwa anajua kuyaita majini na kuongea nayo. Alikuwa analetewa hata watu awapige kisomo na alikuwa na mambo mengi sana ambayo mimi yalikuwa yananitatiza. Lakini all in all alikuwa swala 5 na muislamu kweli kweli. Aliwachukia sana Wakristo na mara nyingi alikuwa akisema alitamani waondolewe wote Duniani. Hii ilikuwa inanishangaza. Nlisoma shule ya Wakristo. Tena RC. Nakumbuka ambavyo waliheshimu sana imani za sisi waislamu wachache.

Hatukuzidi 13 pale shuleni. Lakini walihakikisha hatulishwi nguruwe na vyombo ambavyo vinatumika kupikia Nguruwe havichanganywi na vya ujumla. Walitupa darasa la kuswalia. Walituheshimu sana. Mimi hili lilinipa shida. Sababu nlitamani tuchukiane wao hawakutuchukia wala kututenga. Walikuwa nasi vizuri tu. Ilinifanya nitake kujifunza Biblia. Sikujua ambayo ngekutana nayo huko mbele. Huwa najuta sana kwa uamuzi huo wa kusoma Biblia mpaka leo

Nitaendelea...
Ulikuwa unasoma bure hiyo shule ya makafiri,?(acha kutumia jina hilo,Kuwait wengine makafiri)
 
Huyo sio muislamu ila anapenda kuzusha chuki za udini
Huu ni ukweli,ikiwa kazaliwa 1970,mpaka anafika secondary,itakuwa ni miaka ya 1980,wakati huyo,shule zote zilikuwa ni za serekali,Mwalimu Nyerere,hakuruhusu shule za dini wala za binafsi,na zilizokuwepo,ni chache na zilipewa masharti maalumu kwa uwepo wao.aitaje hiyo shule jina lake.
 
Huyo jamaa ni mdogo sana ,hana cha maana ameshanifuata sana inbox na ile ID yake lya komeo la chuma ..Ningeshare hapa ,simuelewi kama ni gay ila kunifuata inbox kama mara mbili ili kuleta shari ila kadunda mpaka kaniblock.
 
Huyo ni dogo tu kama anabisha aprove hapa ...Hakuna mtu ana miaka 50 na kuendelea akawa analeta content za kukejeli dini isiyokuwa yake..Anajifanya muislamu wa mchongo.

Huyo ni wale vijana waozurura huko ughaibuni kama chimakeke🤣🤣hawana impact kazi kushangaa.
Nampenda sana chimakeke😆😆
 
Huyu ni muongo,ikiwa kazaliwa 1970,itakuwa secondary kasoma miaka ya 1980,miaka hii,ya utawala wa Mwalimu Nyerere,shule za kidini,zilitaifishwa na kuwa za serekali.halafu pia hao kina Sharifu Majini,hawajakuwa watu wazima,na hao kina Mazinge na Sharif Majini,hawako kitu kimoja.
 
Baba mtoto ameyakanyaga hata mama mtoto wake ameniita kafiri jamani 🤣🤣🤣🤣🤣

Paulo aliwashangaa hao wasioamini katika Kristo na kuwaita Wagalatia waliorogwa...

Wagalatia 3: 1
Enyi Wagalatia, mmekuwa wajinga kweli! Ni nani aliyewaroga? Habari juu ya kusulubiwa kwake Yesu Kristo ilielezwa waziwazi mbele ya macho yenu.

Lakini hata leo hii hawaamini juu ya habari za msalaba, hata jina la Yesu Kristo likabadilishwa na kuitwa wanavyoliita
 
Huyo jamaa ni mdogo sana ,hana cha maana ameshanifuata sana inbox na ile ID yake lya komeo la chuma ..Ningeshare hapa ,simuelewi kama ni gay ila kunifuata inbox kama mara mbili ili kuleta shari ila kadunda mpaka kaniblock.
Mtu alie jiunga jf 2013 sio mdogo kiumri , labda useme mdogo kibusara
 
Nimepata hasira sana kuona neno
makafiri
yani akili za dini nyingine bwana
Kafiri mwenyewe...😏😏😏😏
Kafiri wala sio neno baya kwnye biblia yako pia limeandika zaidi ya mara 15
 
Nimezaliwa mwaka 1970, na kupata Elimu yangu ya Msingi hapa hapa Dar Es Salaam na Sekondary Nje ya Dar Es Salaam katika shule zinazomilikiwa na Makafir. Kiukweli ilikuwa changamoto kidogo kutokana na Mzee wangu kuwa ni mtu anayeshika sana Dini.

Kwa wale watu walioishi Kimanga, Mji Mpya watakuwa wanaufahamu Msikiti wa Ngunde. Mzee wangu alikuwa hakosi kuswali pale swala zote tano. Nakumbuka hata kipindi kile Sheikh Shariff Majini amekuja Kimanga mmoja ya watu ambao walisupport sana ile mihadhara alikuwa mzee wangu.

Mimi nmecheza mpira Uwanja wa Twiga nikichezea Twiga na akina Omary, Mluguru, Galabu n.k kwa wenyeji wa maeneo hayo watakuwa wanakumbuka.

Sheikh Shariff alifanya sana mihadhara ule Uwanja wa Twiga. Nilikuwepo kipindi hicho sehemu za mbele kabisa. Akina Mazinge watakuwa wananikumbuka pia sababu nlikuwa mtu wa imani sana. Mwaipopo na Abubakar. Hawa hawawezi nikumbuka.

Mzee wangu alikuwa ni mmoja ya wazee wenye kauwezo flani yale maeneo tukiwa na nyumba nzuri miaka hiyo yenye fensi. Na tulifanikiwa kwenda shule tofauti na wenyeji wengi ambao waliishia darasa la 7 au hawakumaliza shule. Sekondary O Level nlisoma ya Serikali na A level nikaenda ya Makafir.

Mimi nlikaa na wahuni... Ile mitaa ilikuwa na wahuni sana. Tukicheza mnanda, mchiriku n.k mpaka kipindi imekuja anzishwa team ya Begeju baada ya Twiga kuvunjika. Begeju ikawa ina wahuni wavuta bhangi na Twiga ya wastaarabu. Ilikuwa hizi teams zikikutana moto lazima uwake.

Leo hii nimefikaje hapa JF? Na wengi wananiona kama si Muislamu (nakubaliana nao) na huwa natamani sana niweze kuwa Mkristo ingawa bado sijaweza kuwa sababu ya aina ya maisha ambayo nimezoa na imani iliyonikuza. Huwa nawaambia watu mimi Role Model wangu kwa tabia zangu zote ni Muhamad. Huwa sitanii.

Lakini Elimu ilinisaidia sana kufunguka na kusoma kwa kureason hivi vitabu. Nlianza kusoma Biblia kwa lengo la kupata mistari ya kupotoshea Wakristo na kuwananga. Badala yake ikaanza kunifundisha vitu ambavyo vilianza kunifanya nione kuna maeneo mengi sikuwa sawa katika imani yangu ya awali.

Mzee wangu alikuwa anajua kuyaita majini na kuongea nayo. Alikuwa analetewa hata watu awapige kisomo na alikuwa na mambo mengi sana ambayo mimi yalikuwa yananitatiza. Lakini all in all alikuwa swala 5 na muislamu kweli kweli. Aliwachukia sana Wakristo na mara nyingi alikuwa akisema alitamani waondolewe wote Duniani. Hii ilikuwa inanishangaza. Nlisoma shule ya Wakristo. Tena RC. Nakumbuka ambavyo waliheshimu sana imani za sisi waislamu wachache.

Hatukuzidi 13 pale shuleni. Lakini walihakikisha hatulishwi nguruwe na vyombo ambavyo vinatumika kupikia Nguruwe havichanganywi na vya ujumla. Walitupa darasa la kuswalia. Walituheshimu sana. Mimi hili lilinipa shida. Sababu nlitamani tuchukiane wao hawakutuchukia wala kututenga. Walikuwa nasi vizuri tu. Ilinifanya nitake kujifunza Biblia. Sikujua ambayo ngekutana nayo huko mbele. Huwa najuta sana kwa uamuzi huo wa kusoma Biblia mpaka leo

Nitaendelea...
Ulijuta nini sasa kwa kuisoma biblia
 
Back
Top Bottom