History inapingana na wanaosema ''HAKUNA MUNGU'': The simple research you can do to prove it.

Kwanini umeshindwa kuthibitisha Roho? Of course God is Spirit. Kama kuna Mbishi aje hapa anipe ushaidi kwanini Mungu sio Roho. That is how it works.
Zaidi ya hapo, hivi unaposema thibitisha kama Mungu yupo huwa unatumia formula gani?
Hii Para ya kwanza umenimaliza ila nasisitiza mmea hauna Roho (animals. Plants zote zina Cells) na MUNGU ni ROHO uatakapofika kwenye UTATU MTAKATIFU tutaongea sitaki kwenda huko kuamini ila hii yako
Mungu sio Roho.Of course God is Spirit.

para ya pili ya kuthibitisha MUNGU yupo imeshaelezwa na jamaa yetu humuhumu kuwa akili tuliyonayo ni vigumu kutambua UWEPO wake kwani hakuna aliyekutana naye au kuongea naye ila ni Hadithi ambazo tanazukubali au kuzikataa ni mpaka hapo tutakapokufa.
(mfano mimi sijawahi kumuona hata katika Ndoto, au kumhisi uwepowake majini au katika hewa il napambana na vinyamkkera na majini ambavyo UKIVIKEMEA KWA KUTUMIA JINA vinakimbia
kwa hiyo formula rahisi ya kuthibitisha ni pale utakapotoa USHUHUDA
la sivyo ni URONGO Utapeli kwa jina la Mungu - YouTube kwa hisani na Kahtaan
 

nishakwambia hiyo hoja ya matter and energy itoe umeendelea kuishikilia tu on top of that usiseme niliyemcopy hajielewi hizo arguments sijachukua toka kwa mtu mmoja nimechukua more than five sources baada ya kuchambua na nyingine nimeziacha na nyingine nimeongezea mimi.


Kuhusu kukataa hoja ya complexity inathibitishaje uwepo wa mungu hilo ni tatizo lako i cant help you with that,

narudia tena huwezi kuonyesha uwepo wa mungu bila ya kuonyesha effect zake hapa ulimwenguni ambazo ww unaendelea kuzikata sijui uelezewe vipi ili uelewe ni sawasawa na mwanafunzi kapata mwl mzuri kafundishwa kaelewa akafaulu alafu ukatae kwamba ile effect ya kufaulu kwa mwanafuzi haijatokana na mwl.


Tukirudi katika roho-kwa lugha ya kimombo wanaita soul by defn means the non physical part of a person that is seat of emotion

or spititual part of a human body that is believed to give life
ndo maana mwanzo nikakuuliza unaelewa nini kuhusu roho ili tuanzie hapo unapoelewa wewe nisije nikatoa defn ambayo hutoikubali tukarudishana nyuma....

So umesema huamini roho wala maisha baada ya kufa wala super natural yoyote.
sasa jiulize maswali haya wale watu wanaokuwa na mapepo,or mashetani
?? Nini kinakuwa kinawaingia mwilini mwao what made them to behave strange??? Maana unaweza kumkuta mwanamke ana pepo la simba basi unaanza kumkuta ananguruma kama simba anatoa sauti nzito na ajabu zaidi anakuwa hana fahamu na wala haelewi nini kilikuwa kinaendelea,(so nipe maelezo hapa mwanamke mwenye sauti nyembamba na laini sauti nzito kama ya simba anaipata wapi?? Hilo moja pili anavyokuwa hajitambui nini kinaendelea katika mwili wake yeye huwa hasa anakuwepo wapi??? Na who is taking controll of her body???

Tuje katika maisha baada ya kufa,simple logic kama kuna maisha kabla ya kuzaliwa kwa nini kusiwe na maisha baada ya kufa? hilo mosi,pili tujiulize kwa nini mtu anakufa??? Na mtu akifa nini hasa kinakuwa kinaondoka katika huo mwili wake??? Na kwa nini tunaita mwili wa marehemu... That means owner wa ule mwili hayupo pale yupo somewhere else very posible kuna maisha mengine huko yanaendelea,roho na mwili wa binaadamu unaweza kuifanaisha na comp na operating system,os unaweza ukaichukua ukaiingiza kwenye comp(physicl part) yoyote ile unayoitaka ndo maana unaona majini mapepo wanaingia katika miili ya binaadamu na kutake controll ya miili yao.
 

Kama hizo mada umechukua kwa zaidi ya mtu mmoja, then wewe ndiye uliyejikombea tu vitu vinavyoji contradict bila kujua.

Hoja ya complexity , inalazimisha kila kilicho complex kiwe kimeumbwa, hivyo inalazimisha hata mungu unayesema katuumba awe kaumbwa, na aliyemuumba awe kaumbwa, hivyo hivyo bila mwisho. Mtu yeyote anayefikiri ataona huu ni upuuzi.

Huwezi kusema tu kwamba hii ni effect ya kuwepo kwa mungu bila kuthibitisha.

Pia, hujajibu swali. Kama mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote yupo na ndiye aliyeumba ulimwengu huu, imekuwaje aumbe ulimwengu ambao mabaya, maovu na maumivu yanawezekana? Does that make sense to you?

Kuhusu roho/ soul, mtu akikwambia there is no proof of soul, only a brain and mind and we do not understand how consciousness works, utasemaje?

Mapepo yanaweza kuelezeka kwa namna nyingi, kwanza kuna mental conditions, pili kuna fraud ( kasome historia ya Jim Jones wa Guyana alivyowatapeli wafuasi wake kwamba anatoa mapepo na kisha kuwaua Kibwetere style). Ukisoma psychology na brain science utaona kuna ma hypnosis na mambo kibao ya brain science amvayo hayajaeleweka vizuri bado, kwa nini tunakimbilia kukubali mapepo bila uchunguzi?

Kuhusu maisha baada ya kifo/ kabla ya kuzaliwa, thibitisha kwamba either exists.

Usiseme "very possible kuna maisha mengine huko" that's guesswork, huna hakika, unabahatisha.
 

Kama mmea una uhai lakini hauna roho, uhai hauthibitishi kuwapo kwa roho.

Kwa nini unafikiri kila mtu anaogopa kupoteza uhai?

Kuna watu wanajitoa uhai wao wenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Labda ameshindikana kwako....

kwahiyo unakubali mungu hayupo kwa mtazamo hafifu na dhaifu wa Kiranga?

umechemsha

Hujajibu maswali, thibitisha bila mgongano wa hoja zako mwenyewe na kwa kutumia logical, consistent and comprehensive arguments kwamba mungu yupo.

Pia, hujajibu swali la, kama mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote, uzuri wote yupo, basi angeweza kuumba ulimwengu bora zaidi ya huu, ulimwengu ambao hauna shida, majanga, ubaya, magonjwa etc.

Kwa nini hatuoni ulimwengu huo? kwa nini mungu huyu kama yupo hakuumba ulimwengu huu?

Kabla ya kujibu maswali haya, huwezi kusema mtazamo wa Kiranga ni hafifu na dhaifu.

Kwa maana wako ni hafifu na dhaifu zaidi.

Hujaweza kujibu maswali ya mtu mwenye mtazamo hafifu na dhaifu kama Kiranga.
 


Hiyo logic si umeikataa?

Nilikuhakikishia uwepo wa Mungu maneromango ulibisha bila kusema kwa nini unabisha...

Mfano Mimi nikisema mama yako ni huyu ukakataa itabidi uelezee why unakataa kwa kutoa features za huyo unaemhisi..

hiyo logic unayoiimba ndio hiyo inayotuambia huwezi kataa uwepp wa kitu wakati hukijui..


Huna jipya... hujui ufanyalo ..
 

You have it backwards.

Ukisema mungu yupo Maneromango itabidi wewe unayesema mungu yupo Maneromango unieleze kwa nini unasema hivyo. Kusema tu hakutoshi, si uthibitisho. Inabidi utoe sababu, kwa nini mungu yupo Maneromango, na sio Cholesamvula wala Masaki (ya Kisarawe si ya Dar).

Nimekuuliza kwa nini umesema mungu yupo Maneromango, na si Kazimzumbwi wala Minaki.

Hujanijibu.

Halafu unaita maneno yako mbofumbofu "logic".
 

Si dhani kama ulikuwa unazungumzia Mmea. Jaribu kubakia katika swali lako la mwanzo. Usiwe kama yule GOD HATER anaye ruka huku na kule na kukimbia madai yake mwenyewe.
 
 


huna jipya..

unajisikia aibu kukubali ukweli
 

By Kiranga

Hujaelewa/ unakwepa swali, siulizi mungu wangu, nauliza mungu wako.











Hayo maneno kwenye Quote hapo juu ni yako.

Narudia swali lile lile:

HUYO ALIYE ANDIKA POST YENYE WORDS IN RED. ANAJUA ALICHO ANDIKA AU ANAAMINI ALICHO ANDIKA?
 

We kiranga huna lolote, subir tu mauti ya kukute ndipo utakapomjua mungu!. Jamani Hamna namna yoyote ́mtakayomwambia juu ya mungu akakakubali huyu kiumbe. Labda amuone! Yeye anamsimamo wake tayar .Nadhani huwa anakuchekeni tu mnapomuelimisha.
 
We kiranga huna lolote, subir tu mauti ya kukute ndipo utakapomjua mungu!. Jamani Hamna namna yoyote ́mtakayomwambia juu ya mungu akakakubali huyu kiumbe. Labda amuone! Yeye anamsimamo wake tayar .Nadhani huwa anakuchekeni tu mnapomuelimisha.

Si kweli kwamba sina lolote.

Nina maswali ambayo hujayajibu.

Kwanza, thibitisha kwamba mungu yupo. In a logically consistent way.

Pili, nieleze imekuwaje mpaka mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao maovu na mabaya mengi tunayoyaona yanawezekana kufanyika?

Kabla ya kujibu maswali haya, huwezi kusema sina lolote.

At the very least nitakuwa na maswali ambayo hujaweza kuyajibu.
 

By Kiranga

Hujaelewa/ unakwepa swali, siulizi mungu wangu, nauliza mungu wako.













Hayo maneno kwenye Quote hapo juu ni yako.

Narudia swali lile lile:

HUYO ALIYE ANDIKA POST YENYE WORDS IN RED. ANAJUA ALICHO ANDIKA AU ANAAMINI ALICHO ANDIKA?
 

huna lolote wala chochote

si lolote si chochote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…