kijana mwenye ukakasi kama @ukwaju, Tatizo lako wewe na huyo mwenzako @kiranga ni Elimu ndogo! na bahati mbaya mnajifanya MNAJUA!
Na hili ndio tatizo linalowakuta wengi mno wa namna yenu!
Nadhani nimeshatoa darasa huko nyuma kuhusu KUWEPO KWA MUNGU! Na nikarudia mara kwa mara kuwafahamisha kanuni za kujua Mambo kama hayo. na hapa NTARUDIA TENA, manake mwalimu hachoki kufundisha.!
Mantiki ya dhana ya Mungu
Swali langu la kwanza kwenu nyie litakuwa: "Ni nini maana ya Mungu ?" Kwa mtu kusema hakuna Mungu, Unapaswa kujua nini maana ya Mungu.
Kama mimi nikishikilia kitabu na kusema kwamba 'hii ni kalamu', kwa mtu Mwingine kusema, 'Hio si kalamu', anapaswa kujua ufafanuzi wa kalamu ni KITU GANI, hata kama yeye hajui wala uwezo WA kutambua kitu hicho kilichoko katika mkono mwangu hana! Kwa yeye kusema hii si kalamu, anapaswa angalau kujua japo MAANA YA kalamu.
Vile vile kwa WEWE au hao wasio na elimu kina @kiranga kusema 'hakuna Mungu', mnapaswa angalau kujua JAPO MAANA ya Mungu. NA Dhana ya kuwepo Mungu itakuwa inatokana na mazingira mnayoishi nyie wenye kupinga kuwepo kwake.
Kila kitu ktk Huu ulimwengu ili wewe na mimi tupate kukijua au kukielewa au kukitekeleza basi lazima tufuate KANUNI YAKE.MAALUM !
na KILLA KITU KINA KANUNI.
Ntakupa mifano hapa!
1. UKITAKA UGALI lzm upate UNGA NA ukitaka unga sharti utwange au usage nafaka, na ili upate nafaka sharti upande mbegu kwenye ARDHI YENYE RUTUBA.
2 UKITAKA KUFAHAMU jumla ya namba, mfano 2 na 2 zinakuwa ngapi! basi sharti UTUMIE HESABU, LA SI HIVYO HUWEZI KUPATA JIBU.
3. Na ili wewe @ukwaju na huyo @kiranga mpate nguvu ya kuja hapa jukwaani kutumwagia mapovu, basi LAZIMA MLE CHAKULA! na msipokula HAMTOPATA NGUVU, na matokeao yake mtapoteza maisha!
SASA Kutokana na mifano hio michache hapo juu, ntajaribu kuwafundisha KANUNI IPI IFUATWE ILI MUWEZE KUMFAHAMU MUNGU NI NANI!
Naomba nikufahamishe kitu kimoja. kama mjuavyo kuwa MIMI NI MUISLAMU. Na ntajaribu kukuelimisheni kupitia ISLAMIC CONCEPT OF WHO GOD.
Kabla ya Kukimbilia kujiuliza MUNGU NI NANI, AU YUKO WAPI n.k Sharti tujiulize JE! NI NANI ALIYENIAMBIA MIMI KUWA KUNA MUNGU??
Manake kila mwenye imani ya KUWEPO KITU CHOCHOTE, Basi kuna chanzo ambacho Kimelezea kuwa Kile kitu au sehemu kuwa ipo, au kipo!
Tulipoambiwa kuwa ULIMWENGU WETU NI MDUARA WA umbo la yai! Cha kwanza tulichofanya ni kujiuliza je! nani kayasema haya?? na je! wana credibility gani hao waliosema hayo?? na baada ya kuwasoma hao wanasayansi na kuangalia ni namna gani wameelezea huo ugunduzi wao, Basi kwa kutumia AKILI ZETU pamoja na utafiti wa namna tofauti Tukaja kwenye HITIMISHO KUWA KWELI DUNIA YETU INA UMBO KAMA YAI!
Sasa kwa mimi Muislamu, Sehemu ilionifahamisha kuwa MUNGU YUPO NI QURAAN. Kitabu ambacho kwa mujibu wa HISTORIA kinadaiwa kuwa ni maneno ya MUNGU yaliopitia kwa Mtu mmoja aitwae MOHAMMAD IBN ABDILLAHI{s.a.w} aliyezaliwa huko bara ARAB miaka 1500 na kidogo iliyopita!ambae alidai kuwa yeye ni MTUME WA MUNGU!
Sasa kwa kufuata ile KANUNI ya UHAKIKI jambo la kwanza ni KUFANYA UPEKUZI WA KINA KUHUSU HIO QURAAN,!JE!HIO QURAAN KWELI NI MANENO YA MUNGU??
Tukisharidhika na hilo, Then SIDHANI KAMA TUTAKUWA NA HAJA YA KUCHUNGUZA MENGINE ZAIDI, manake kama tukiridhika na hilo, moja kwa moja tutakubali kuwa KILA LISEMWALO HUMO LITAKUWA LIMETOKA KWA HUYO AMBAE tunajiuliza kama yupo, au hayupo.
LKN kama pia hukuridhika sana unaweza pia Kumchunguza huyo MUHAMMAD! JE ni kweli anachodai KUWA YEYE NI MTUME??
Sisi binaadamu wa sasa ambao Tumebahatika kuishi ktk karne ya sayansi na teknologia mambo yetu mengi tumekuwa tukitumia KANUNI za kisayansi ktk KUYAHAKIKI.
imefikia kipindi sasa hata ile nyanya pia tunatumia kanuni za sayansi ili tujue faida zake na hasara zake.
SASA BASI, Hebu tujaribu KUTUMIA KANUNI HIZO HIZO kutazama UWEZEKANO WA HIO QURAAN KUWA NI KITABU AU MANENO YA MUNGU.
Nadharia{kanuni} ya uwezekano au THEORY OF PROBABILITY.
Katika hisabati kuna nadharia inayojulikana kama ' nadharia ya uwezekano .Ambayo inakwenda kama hivi.
Kama una chaguzi mbili, ambayo moja ya SAHIHI, na moja ni SI sahihi, nafasi ya kuwa wewe utachagua moja sahihi ni nusu , yaani mmoja kati ya wawili watakuwa sahihi . Una 50 % nafasi ya kuwa sahihi.
Vile vile kama wewe utarusha sarafu juu, na ukaamua kuchagua upande wowote, nafasi ya wewe kuwa sahihi ni 50% (1 nje ya 2 ), yaani 1/2.
Kama utarusha sarafu mara ya pili, nafasi ya wewe kuwa utakuwa sahihi mara zote mbili INAPUNGUA KWA NUSU TENA yaani (1/ 2 x 1/2) ambayo ni sawa na 1/4 yaani 50% ya 50% ambayo ni sawa na 25%.
Kama utarusha sarafu mara ya tatu, nafasi ya wewe kuwa utakuwa ni sahihi mara zote tatu inapungua tena na inakuwa ni (1/2 x 1/ 2 x 1/2) kwamba ni 1/8 au 50% ya 50% ya 50% kwamba ni 12 ½% .
mfano wa pili wa nadharia ya UWEZEKANO.
Ukichukua kete yenye pande sita . Kama ukitupa kete na ukadhani idadi yoyote kati ya 1 hadi 6, nafasi ya kuwa dhana yako itakuwa sahihi ni 1/6 . Kama utatupa kete mara ya pili, nafasi ya wewe kuwa sahihi katika mara zote mbili ni (1/6 x 1/ 6) ambayo ni sawa na 1/36 .
Kama utatupa kete mara ya tatu, nafasi ya wewe kubahatisha mara zote tatu na ukawa sahihi ni (1/6 x 1/ 6 x 1/6) ni sawa na 1/216 ambayo ni chini ya 0.5%.
Hebu sasa TUIINGIZE HII nadharia hii ya uwezekano KTK Qur'an , na tudhani tu kuwa MOHAMMAD ALIBAHATISHA taarifa zote zilizotajwa katika Qur'an ambayo ilikuwa haijulikani wakati huo.
Hebu tujadili uwezekano wa kubahatisha kwoote huko KULIKO TAJWA ndani ya QURAAN kulikuwaje wakati huo huo kuwa sahihi mara ZOTE?? .
1.Wakati Qur'an ilinafunuliwa , watu walidhani dunia ilikuwa TAMBALALE, kuna chaguzi nyingine kadhaa kwa ajili ya kuitafakari sura ya dunia. wengine walisema Inaweza kuwa pembe tatu, inaweza kuwa quadrangular , pentagonal , hexagonal, heptagonal , octagonal , spherical, nk na kule kudhani kwao kuhusu sura na umbo la dunia kulikuwa na chaguzi mbalimbali 30.
Qur'an imeeleza Sawa sawa 100% kuwa Dunia ni spherical, ikiwa ni dhana peke yake basi nafasi ya dhana hii kuwa sahihi ni 1/30 .
2. Mwanga wa mwezi unaweza kuwa mwanga wake mwenyewe au mwanga unao akisi .
Qur'an imesema Sawa Sawa kuwa ni mwanga ulio akisiwa. Kama ni dhana peke yake , basi nafasi ya kuwa itakuwa ni sahihi ni 1/2.
na uwezekano kwamba quraan imeweza KUBAHATISHA vyote hivyo, yaani nchi ni spherical na mwanga wa mwezi ni mwanga yULIOAKISIWA ni 1/30 x 1/ 2 = 1/60 .
3. Zaidi ya hayo, Qur'an pia anataja kila kilicho hai chanzo chake ni MAJI. . Kila kilicho hai Kinawezakana kuwa na vyanzo vingi kama miti, mawe, shaba, aluminiam, chuma, fedha , dhahabu , oksijeni, nitrojeni, hidrojeni, mafuta , maji, saruji, , nk chaguzi hizi tumejifunza ktk HISTORI zimetajwa chaguzi zaidi ya 10,000.! ambazo watu walidhani ni nini chanzo cha UHAI.
Qur'an Sawa Sawa inasema kwamba kila kitu kilicho hai Basi CHANZO CHAKE NI maji. Kama ni DHANA nafasi ya kuwa itakuwa ni sahihi ni 1/10, 000.
na uwezekano wa Quraan KUBAHATISHA VYOTE VITATU yaani nchi ni spherical, mwanga wa mwezi ni mwanga ULIOAKISIWA na kila kitu KILICHO HAI Kitokana na maji kuwa sahihi ni 1/30 x 1/2 x 1/ 10, 000 = 1/ 60, 000 ambayo ni sawa na kusema 0.0017 %.
Qur'an inazungumzia kuhusu mamia ya mambo ambayo hayakujulikana kwa Mtu yoyote wakati wa ufunuo wake na tunashuku MUNGU leo sayansi imetusaidia kuyaona yale YALIOTAJWA KTK QURAAN MIAKA ZAIDI YA 1500 ILIOPITA!!.
The quraan speaks about hundreds of things that were not known to men at the time of its revelation. Only in three options the result is 0.0017!
i leave it up to you @ukwaju along with your partner @kiranga to work out the probability if all THE HUNDREDS OF UNKNOWN FACTS WERE GUESSES, The chances of all of them being guesses simultaneously and there being NOT A SINGLE ONE HAPPEN TO BE A WRONG GUESS.
It is beyond HUMAN CAPACITY to make all correct guesses without a single mistakes.
which itself is SUFFICIENT TO PROVE TO A LOGICAL PERSON THAT THE ORIGIN OF QURAAN IS DEVINE.
SASA bwana @ukwaju na huyu anaepinga MUNGU bila elimu @kiranga.
KAMA MMELEWA HILO SOMO HAPO JUU.
Tutaendelea na darasa la pili. na kama unaswali unakaribishwa kuuliza.
cc @polite @mipangomingi @wabara @khawarizm @ngongoseke @ritz @the big show @mdau35