Habari ya muda huu wakuu na ndugu zangu JF.
Mwezi mmoja na Nusu uliopita (about 45 days) nilileta hapa moja ya mtiririko wa jambo langu lililokua linaniandama kama ambavyo nilieleza hapa kwenye uzi huu 👇👇
Wakuu heshma kwenu. Habari za jioni. Nimeona ni vyema kuwa update kuhusu mwenendo wa suala ambalo nilileta hapa jukwaani siku ya jumatatu katika uzi huu...
www.jamiiforums.com
Leo tena naomba kutimiza ahadi yangu kama nilivyoahidi kuwa nitafanya.
PART-1 : KUITIKA WITO
Siku ya jana, nilifanikiwa kufika mahakamani kama ambavyo tuliambiwa baada ya session ya shauri letu la Ndoa na Talaka kuisha mwezi wa pili katikati. Uzuri tuliambiwa kuwa kila mtu anaweza kufika kwa wakat wake mwenyewe ili kuweza kufuata na kukabidhiwa hukumu ya kesi. Sina uzoefu sana na masuala haya ya mahakami hivyo kwa manufaa ya wengi ningependa wajuzi watie neno , maana binafsi kitu nilikua natarajia kukabidhiwa kama hukumu ya kesi hii ni PAMOJA NA HATI YA TALAKA (sijui hata inafananaje).
Hivyo bila hiyana, nikafika jana baada ya kusafiri toka mkoa(maana nilihamisha makazi kwasasa) na mategemeo yangu jana hiyo hiyo niweze kugeuza kurudi nilikotoka. Hizi ndio zilikua hesabu zangu ila ndio hivyo mipango sio matumizi maana nilipofika nikakutana na habar ambayo sikua naitegemea.
Baada ya ku report ofisi ya karani wa mahakama, na kujitambulisha na kisha kueleza detail za kesi yangu na kusudio la uwepo wangu pale, nikaambiwa "karibu, unaweza kukaa chini, naomba Samansi ya kesi" na mi nikaikabidhi. Nafikiri alikua anatazama namba rejea ya shauri letu na baada ya hapo akaanza kufungua yale makabati yao ya chuma. Moyo wangu ukafarijika nikiona kama hesabu za ratiba zangu zitakwenda kama nilivyopanga.
Ila sasa tofauti na matarajio yangu, nikaona muda unakwenda karani kazamia kwenye ma "locker" na baada kama ya 30 minutes akanambia "aisee, hii kesi yenu si ni ya juzi tu mwezi uliopita?".
Nikamjibu "Naam, mid of February".
Akasema "Sioni rekodi yake na pia Hukumu yake haionekani, naomba ukasubiri ukumbini (court hall ambako watu wanasubiria kesi zao kuitwa)"
Nikaona hapa tayari vipengele vishaanza.
Kabla sijatoka akaniuliza "hakimu wako (aliesikiliza kesi) unamjua?"
Nikasema "simjui ila namfahamu kwa sifa 1,2,3(nikazitaja)"
Akasema okay, huyo ni fulani. Akauliza tena "karani wake unamkumbuka aliyekuwepo wakati wa session?" Napo nikajibu kama awali, kuwa simjui ila namfahamu. Akasema "huyo ni fulani"
Akasema "hapa acha nimpate kwanza karani wa kesi yako, maana hakimu yuko busy, japo nae yuko kwenye maongezi na Mfawidhi".
Nikaelekea ukumbuni kusubiri. Nikaona 1 hour imepita siitwi. Nikarud tena ofisi ya karani, sikumkuta badala yake nikakuta "samansi" yangu imebwagwa pale na mtu hayupo. Nikaona hapa nitakesha, nikaanza kuzunguka mle ndani ,kuuliza uliza mpaka nikambahatisha yule karani wa kesi yangu. Nikamueleza kisha akaniambia nimfuate ofisini (kule kule nilikoanzia). Naye akaanza zoezi lile lile ambalo mwenzake alishafanya, mwisho wa siku akaambulia matokeo yale yale na mimi nikapewa majibu yale yale japo ya kwake yalikuja na nyongeza kidogo.
"Sio tu kwamba hati ya hukumu haionekani, bali hata JARADA la kesi yako silioni" nikasema enheehhh!!! But really i was not caring ila kilichokua kinaniuma ni muda wangu niliopoteza na matarajio yangu naona waz hayaendi kufikiwa..
Akasema "kuna mawili, aidha hii hukumu HAIJACHAPWA BADO na Hakimu, yaani hajaindaa au jarada liko mezani kwake"
Nikamuuliza "hii inawezekanaje na hali ni nyie ndio mlinipangia tarehe ya leo kurudi,nikiwa nafikiri kila kitu mnafahamu?"
Akajibu "kuna ambazo nazichapa mimi na kuna zingine anaziandaa hakimu" Nikachoka.
Nikamwambia "kwahiyo way forward ni nini na mimi natakiwa kufanya nini sasa? Maana kama huyo hakimu ana deal na court hearing, mimi siwez kusubiri hapa nina ratiba zingine?"
Akasema "chukua namba yangu, uwe unankikumbusha".
Nikaona hapa hamna kitu. Au ndio masuala ya kutengenezwa mazingira ya kuanza kutumia pesa ili upate kilicho chako. Nikawaza hili suala kwangu wala haliwez nitoa shilingi 10 yangu. Nikachukua namba nikasepa.
HAPO NIKAINGIA KWENYE RATIBA NYINGINE.
PART-2: "kuwaona watoto wangu".
Fasta, nikashuka pale Day Care ambapo mtoto wetu wa mwisho, 3 yrs huwa anashinda hapo. Nikajitambulisha (kwakua mimi sifahamiki sana hapo). Na kabla sijaruhusiwa kumuona mtoto, nikamuomba yule msimamizi pale "naomba umpigie simu (official) mama yake huyu umpe taarifa kuwa mtu flan kafika hapa ili kumuona mtoto isije ikaleta shida, kwenu na kwangu pia"
(Hii ni kwasababu sinaga mawasiliano na ex-yf) toka mwaka jana November.
Sijawah ongea nae kwa simu wala live. Na baada ya kesi nilibadili namba zangu zote hivyo it has been silence for amost 5 months.
Basi wakampigia naye nikamsikia akisema "Haina shida, ni kweli huyo ni baba yake, mpe tu".
nikapewa mtoto ila hakua mchangamfu sana licha ya kuwa alinikumbuka. Nikaona hapa sitamu enjoy nikapata wazo. Nikamwambia yule msimamizi naomba tena umpigie mama yake niongee nae mambo flani
Akapiga kisha akanipa :
Mimi: inakuaje?
Yeye: poa tu za siku?
Mimi: nzuri tu, huyu mbona mmemvalisha rozali?(sis sio wa Rc)
Yeye: aah kuna rafiki yake mtoto mmoja hapo huwa anampenda sana ndio akampa hiyo leo ni siku ya 3 anavaa.
Mimi: naomba ujitahid umtoe na uirudishe rozali ya watu. Akasema sawa.
Mimi: sasa nataka nitoke na huyu mtoto hapa, niwafuate dada na kaka yake ili niwe nao wote pamoja nafikiri atachangamka, amepoa sana.
YEye: poa haina shida mchukue. Ila kabla hujawafuata B na C shulen kwao, njoo hapa kwanza umfuate A, ni breaktime nitamuombea kibali cha kutoka (anakosoma dogo ndio anakofanya kazi ex-yf)
Nikasema poa.
Nikamchukua mwanangu nikawasha gari mpaka kazini kwake mategemeo yangu nitamkuta dogo nje ya geti kama alivyosema. Hivyo sikua nawaza lolote.
Sasa hapa kumbuka mimi niliacha kila kitu (mali),ikiwemo gari yangu amabyo wakati naondoka nilimuachia mshkaji wangu awe anaitumia ili kui keep up isilale tu na ni muda sasa toka nimeondoka.
Sasa yeye akafikiria probably nitakua nimeifuata gari yetu na ndio nitakuja kumchukua nayo hapo shule firstborn wangu/wetu.
But ,kutokana na hali ya mvua jana jijini nikachukua gari ya mshkaji wangu tu, Nissan Navara haina muda toka amei ship toka nje.
Nilipofika nikapaki gari nje ya geti nikawa nawasubiri.
Nikaona mwanangu yuleee anatokea getini. Ghafla nikaona na mama yake huyo naye anafuata. Wakawa wanashangaa pale wakinisubiri. Nikamtumia text kwa namba yangu "mwambie mtoto aje gari hii ilio mbele yenu".
Hakuja mtoto pekee. Nikaona na yeye kasogea.
Nikashusha kioo. Nikawasalimia , yeye akasema "shuka basi tusalimiane vizuri jamani, kwanza ndio nini kutubadilishia magari bila taarifa?" (huku anacheka-not in such, ni kama smile lililozidi).akaendelea "mi nikawa nategema kukutana na DNK yetu (namba za gari yetu).
Nikamwambia "si unafahamu hiyo gari niliiacha kwa flan"? Akasema "yeah i know, huwa napishana nayo sana barabarani, anaitumia"
Nikasema "daah bas viZuri, nilikua na was was kama ameipaki tu, bora kama anaitumia."
Huyu bwana nilie muacha gar naye niliamua tu kutomtafuta baada ya kubadili namba licha ya kuwa ni mshkaji kwa kipindi hiki ambacho nimekua natafuta utulivu ku recover mindset yangu.
Ni hivi, Mimi nina washkaji wangu ambao wife anawajua, na kuna circle nyingine ambayo hata hawajui japo yeye wanamjua. Hii gari nilichukua huko sasa so she had no idea about nahusiana vipi na hii gari mpya. Na kwa upande anaonijua, hajawahi kuniona maishani mwetu natumia gari ya mtu mwingine yeyote. Nikajua tu hii lazima itamfikirisha kidogo
Basi nikashuka,na ile bila kutegemea, ex-yf akanisogelea akani kumbatia kama sekunde 30 hivi kisha akasema "aisee nimeku miss sana".
Nika smile tu friendly huku namtazama but sikusema neno lolote (ofcourse nilim hug pia, sikuona ni vyema kuwa rude na ukizingatia mwanetu mkubwa yuko hapo na ni wa kike) baada ya hapo, akafuata mwanangu akanisalimia kwa kusita sita huku anafurahi (amebadilika sana sasa nimemuona nafikiri kashavuka hatua za ukuaji baada ya kumchunguza overall, hata aibu niliona zimeongezeka.
Mama yake akamwambia "we A, si ulikua unasema siku ukimuona baba utamkumbatia maana umemkumbuka?" Tukacheka pale wote na nikamwambia dogo "come and hug me" and she did.
Basi nikamwambia mama yake "nataka nitoke nae huyu (firstborn) japo kwa saa 1 nitamrudisha"
Akasema "usiwaze nimeshashughulikia kibali chake , hata hivyo na mimi hamniachi hapa, tunakwenda pamoja"😀😀.
Nikasema "haina shida, ni wewe tu,usijefikiri nitawaiba bure, ingieni". Haoooo. Mpaka shuleni kwingine ambapo madogo wawil wanasoma . Hawa wako primary.
Nikafika pale. Nikaomba ruhusa nikawachukua. Walifurahi mnoooooo kuniona. Bas kama ujuavyo watoto, huyu mmoja wa kiume anamuuliza mama yake " mama hii nayo gari ya baba?" Akawajibu "jamani baba yenu huyo hapo, mumuulize, yeye ana majibu yooote ya maswali yoote mlionayo mimi leo mnipumzishe".😅
Basi nami nikawajibu "ndio, ni gari yangu nyingine hii"🤣🤣. Hata sikutaka kumtazama mama yao reaction yake 😆.
Basi tuka spend time hotel ya karibu pale, tukala lunch, nikawapa zaid nilizokuja nazo, kavulana ketu nilikanunulia baiskel. Bas tukaongea mengi sana na watoto pia na sis kama wazazi.
Akaniuliza "umekuja kufuata hukumu?"
Nikasema ndio. Akasema "bas tutakwenda pamoja ". Nikamwambia "sio lazima pamoja kama una ratiba za kazi wewe endelea tu maana hii kila mtu yuko huru kuifuata kwa muda wake. Na hata hivyo mimi nimeshatoka huko, ndiko nilianzia na SIJAFANIKIWA" Akauliza sababu na mi nikampa maelezo. Akauliza kwahiyo nini kinafuata , nikasema ni kufuatilia tu "nitakupa mamba ya karani, baada ya kutoka hukumu, wewe mdai uliefungua kesi, unatakiwa kuiandikia mahakama barua ya kukazia hukumu ili hatua za utathimin mali zianze na kisha mnada"
OFcourse hakua anajua mambo haya hivyo nikatumia muda kumuelisha namna hatua anazotakiwa kuzifuata ili tumalizane kwenye hili. Hata mimi sikua najua ila soon baada ya kesi niliwaona wana sheria na wakanielekeza juu ya haya masuala.
Basi baada ya lunch , nikalipa na tukaingia wote kwenye gari(kumbuka hapo tuko familia nzima) , kisha tukaelekea kwa mshkaji ambapo niliacha gari. Akafurah kutuona. Huyu anajua kila kimachoendelea baina yetu na i guese nikamuacha na maswali sana. Na kwakua ex-yf alikua pale, hatukupata fursa ya kuongea mengi. Tukaondoka.
Hapo ni baada ya ex ku take snap na clip za kutosha..kuanzia chini, kwenye gari, cafteria ,everywhere yani. 😀.
Mimi sikupiga picha hata moja kwa simu yangu. Na aliponiambia, nikurushie kwa bluetoosh nilipotezea tu kidizaini flan. Na sijamuomba picha hizo
Nikawarudisha watoto wawil shule, kisha tukamrudisha huyu mdogo day care na kisha nikamliza na hawa wawil, mtu na mama yake maana wao wako pamoja. Tukaagana, ila ex-yf alijichelewesha kushuka kwenye gari (nilisoma mchezo juwa alitaka kwanza dogo atangulie). Alipobaki yeye na mimi (alikua sit ya mbele all the the time), akanisogelea ,akani hug, akanipa light kiss shavuni mara 2. Akaniaga baada ya kushuka na percel zao.
Sikubeba zawadi yoyote special kwaajili ya mama yao, but ni zawadi za watoto tu pamoja na kuwapa cash.
Basi akashuka akaingia kazini , nami nikawasha chuma nika geuza mjini, maana makaz yako pembezoni mwa jiji.
HITIMISHO
Ni kwamba mpaka sasa bado sina mkononi official statement ya kuthibitisha kuwa ndoa imevunjika. Naendelea kusubiri.
Kuna mambo kadhaa najiuliza japo naona may ne nina complicate tu mambo huenda ,hivyo si muhumi sana but mambo hayo ni
1. Je inawezekana hakimu akawa ndio anachapa hukumu (secretarial work) kias kwamba yangu bado hajaifanyia kazi kutokana na kuzidiwa na kazi over 45 day ?
2. Je kuna namna ipo mechanism ya mtu /watu behind kuchelewa huku kwa hukum na jalada kutoonekana? Na kama wapo ni nani? Maana nachojua, hata kama hukum haijatoka (sawa), jalada la kesi linapaswa kuwepo toka siku mdai (ex-wife) alipofungua kesi, hivyo mambo yoote kuhusiana na shauri letu mfamo mwenendo wa kasi mpaka hukum vinatakiwa kuwa humo??? (Wanasheria wanisaidoe kuelewa).
3. Siku baada ya kesi kuisha na mimi kusimama, nilimuacha ex-yf amekaa na hakuonekana kunyanyuka ,kitu ambacho nilikitafsi kama alichoshwa na suprise ya kesi jinsi ilivyokwemda na kuisha siku hiyo hiyo, JE, kuna namna hili linahusiana na kuchelewa kwa hukumu? How??
Mwisho kabisa, naamini ni mambo ya kwaida tu hasa kwa mahakama za kibongo kuchukulia mambo poa poa tu so hata hili laweza kuwa ni moja kati ya zile kazi za "businesa as usual".
Wasalaam
Ahsanten.