Hivi ATCL kufanya safari za ndege Chato, hakutaliletea hasara kibiashara Shirika hilo?

Mkoa wa Geita unatembelewa na mabillionare kadhaa kutoka nje kwa sababu ya kununua dhahabu. Vile vile Geita ni mkoa ambao unatakiwa kuwa na uwanja wa ndege. Watanzania mnakwama wapi kuwa na wasi wasi wa ndege zetu kwenda Geita? Mbona mikoa mingine hamuhoji? Kwa mfano Kilimanjaro, Dodoma, Dar Es Salaam, Zanzibar, Unguja nk. Wacheni wivu Geita ni sehemu ya Tanzania na lazima ivune kinachotokana na Tanzania.
 
Wacha1
Wivu gani tunaionea Chato?

Tunaongelea hali halisi ya kibiashara, kuwa ni lazima ufanye tathmini, kabla ya kujitumbukiza kwenye mradi wako, kujua kama utaleta faida au laa
 
Wacha1
Wivu gani tunaionea Chato?

Tunaongelea hali halisi ya kibiashara, kuwa ni lazima ufanye tathmini, kabla ya kujitumbukiza kwenye mradi wako, kujua kama utaleta faida au laa
Mkuu tuwekee ushahidi kwamba hawakufanya tathmini?
 
Mimie nashindwa kuelewa kwa nini Tunawaombea mabaya ATCL. Kwanza chato ni miongoni mwa sehemu za tanzania. Na nyegine ni sehemu alietoka mh rais wetu wa tanzania. Kwahiyo kwanini tunaadama ATCL? Kama hamna abiria basi watasitisha. Zote tunajifanya wajuaji.
 
Baada ya muda kidogo utatuletea mrejesho mwenyewe tunakusubiri kwa hamu kubwa.
 
Hii ya ndege kujaa kwenye booking nayo ni kichekesho kingine , Kama sio hujuma

Nimesafiri Mara kadhaa na Atcl , kwenye booking naona ni last seats ,ila Siku ya safari mnasafiri na dege halijajaa hata nusu yake
Haa ha ha, si unajua sie ni mabingwa wa kutengeneza movies; sina hakika kama hua mnaruhusiwa kupiga picha humo ndani
 
Lakini usiwazuie wanahabari kuleta mrejesho wa usemalo.
Mimi tena kaka? Mi niliangalia tu ile booking nikakuta Ndege is almost full, hiyo ya kuzuia wana habari kuleta mrejesho, jeuri hiyo naitoa wapi?
 
Ukisoma koments za JF siku hizi unatambua tunaelea kuwashinda wachangiaji wa Facebook na Instagram muda mfupi sana ujao.

Unapozungumzia uwanja wa Chato unazungumza uwanja wa Geita na Kahama.

Watanzania eneo lenye uchumi wa zaidi ya Dollar million 830 kwa Mwaka ukose kiwanja cha ndege hapa tunazumzia Uchumi au Matope?

Uwanja wa Ndege uwepo Kia Hai, na Geita ukosekane wakati Geita wa Uchimi mkubwa kuliko uchumi wa Utalii tulionao Tanzania.

Labda tatizo ni Chato, na kama Geita isingekuwa ni milima ya mawe basi hizi kelele zisinge kuwepo kwa kuwa Uwanja ungejengwa Geita district na sio Chato District Geita.

Mkoa wa Geita una uchumu mkubwa kuliko Mikoa yote Tanzania kasoro Dar es salaam na Mwanza tu.

Kimapato kuna Mikoa minane kwa pamoja haifikii mkoa wa Geita Pekee yake. ( Singida, Mara, Tanga, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Rukwa, Songwe na Njombe) au Mikoa mitano Manyara, Arusha Kilimanjaro, Tanga na Pwani.


Tujaribu kuweka ukweli kutuongoza katika michango yetu hapa JF.
 
Nafikili hupajui CHATO,huwa unasoma kwenye mitandao,
Chato ni kijijini ,huwezi kupalinganisha hata na chalinze,
Mabasi ya kutoka Bukoba kwenda Dsm hayapitii Chato kwa Sasa baada ya kukosa abiria,badala yake yanapitia Biharamulo,
Hakuna anayekataa uwanja kujengwa Chato,shida ni kwamba umejengwa kwa faida gani?
ungejengwa hata Katoro/Buseresele ,
Katoro ni mji wa kibiashara hata Geita mjini haifikii,
Pia Geita ni jirani hata wafanyakazi wa migodi na wafanyabiashara wangeutumia,
Hifadhi ya Rubondo ipo jirani sana na Geita,

Tuache siasa kwenye Mambo ya msingi hata Kama kunakitu kinakufaidisha.
 
Ndege imejaa ya kwenda wapi? Yaani Mataga mnakazi kweli,
Ungekuwa unapajua CHATO usingesema kitu,
Chalinze ni mji mkubwa Sana kuliko Chato.
Mkuu,usinichanganye na wana magamba tafadhari, please dont do it again, nakuomba. Mi nimeona kwenye system kwamba trend ya wateja ni kubwa, sasa kama system imenidanganya hilo si suala langu mkuu, hata wewe unweza tu ku apply uone simple as that.
 
Kutoka Geita mpaka chato kuna miji midogo midogo inazidi ukubwa Chato. Kwa kweli kule wamebugi. Walishindwa nini kuweka Geita mjini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…