Hivi Dodoma ndio hakuna maji namna hii?

Hivi Dodoma ndio hakuna maji namna hii?

Shukrani kwa clarifications Mr. Emmanuel,

Me naomba tu kufahamu maeneo ya Ilazo huku mnaturudishia maji lini, Nina miezi sasa at least tulikuwa tunapata maji vyema tu, hata yakikata ilikuwa ni siku chache zinazovumilika..!!

Lakini haikuwahi kuwa mbaya hivi kama ya hii week yaani hamna kitu, tupo kama tunaishi jangwani..!!
Jirani angu kumbe jna usiku yalitoka uku ilazo baada ya kma wiki kuwa kukavu
 
Makao makuu yanajengwa tangu 1973, lakini suala la maji halikupewa kipaumbele. Ikulu inazinduliwa, lakini tatizo la maji halijatatuliwa. Hii ndio Tanzania ya minazi mirefu.
Hiyo hali ni mikoa yote
Hata dar kwenyewe maji ni changamoto
 
Suluhisho lakudumu Ni kutoka Maji ziwa Victoria mpaka Dodoma wangeomba hata itumike force Account kufanikisha hilo jambo.
 
Katika bara la Africa ni 2% ya watu hupata maji safi na salama,Refer to Contemporary Geography for Africa
 
Itawafaidishaa eeh sie tunaliona ziwaa kila siku lkn majumban hakuna maji
Itakua hao wanaopelekewa maji
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Kuna mambo yanafikirisha sana🤔🤔
 
Mdau pole kwa changamoto hiyo

Mimi ni Mkurugenzi wa Usambazaji maji na Usafi wa Mazingira hapa DUWASA.
Kwanza ningependa kufahamu eneo uliloishi kwa muda huo wote ukakosa maji, pili nielewe kwa kifupi kuhusu hali ya maji jijini Dodoma.

Pamoja na kuhudumia Dodoma Mjini, DUWASA pia inahudumia miji ya Chamwino, Kongwa, Bahi na hivi karibuni tumeongezewa kibaigwa.

Ukiongelea Dodoma mjini, utakumbuka kuwa kati ya mwaka 2017/18 yalifanyika mabadiliko ya Serikali kuhamia Dodoma ambapo immediately kama taasisi tulitarajia ongezeko kubwa la mahitaji ya maji. Wakati huo tulikuwa tumekamilisha mradi wa maji hapa mjini ambao uliongeza uwezo wa uzalishaji na usambazaji maji kutoka lita 30 milioni hadi kufikia lita 61.5 milioni kwa siku. Mradi huu ulikamilika 2015, na miradi ya maji husanifiwa kwa kipindi cha kati ya miaka 20 mpaka 30.

Kutokana na hali hii ya ongezeko la mahitaji ukilinganisha na uwezo uliopo, hatua kadhaa zimechukuliwa na zinatekelezwa na DUWASA chini ya Wizara ya maji kutatua changamoto hii.

Mahitaji kwa sasa ni lita 133 milioni kwa siku wakati uwezo ni wastani wa lita 68 milioni kwa siku. Hii inatulazimu kutoa maji kwa mgao. Ndiyo maana nimeuliza eneo uliopo ili kujua nini kilitokea.

Tunaendelea na utatuzi wa changamoto hii katika hatua za Muda Mfupi (uchimbaji wa visima pembezoni Mfano Nzuguni), Muda wa kati (Ujenzi wa bwawa pa Farkwa), Muda Mrefu ( Kutoa maji ziwa Victoria)na Mpango wa Dharula (kutoa maji bwawa la mtera)

Yote hii ni kuhakikisha Dodoma inakuwa na huduma toshelevu ya majisafi.
Dodoma Ilazo extension hadi Swaswa hakuna maji wiki ya pili sasa. karibu na kule anakokaa mke mmojawapo wa waziri wako JUma aweso. kooote hakuna maji. jana nimepita swaswa mnarani watu wanauza maji ya kisima. na pamoja na kwamba maji hayatoki, bili bado huwa mnaleta.
 
Huu mkoa kweli hapana nimekaa miezi yote shida ya maji nilikuwa naisikia tu sahii naona ndiyo tunaishi nayo, inakera mno..
Mpaka hapa tulipofika kama nchi bado tuna struggle na vitu kama Maji kweli..?
yaani kama Makao makuu ya nchi kuna shida ya maji, vipi mikoani?
 
Unaweza kukuta huyo unayebishana naye, yuko Kakonko kwa shemeji yake. Hivyo jitahidi tu kumpuuza.

Huo mji una changamoto kubwa ya maji kitambo tu. Na sababu kubwa ni uwepo wa miundombinu ya maji isiyo endana na ongezeko kubwa la watu.
basi wawe wanatoa mgao walau siku tatu tatu au wiki wiki. kuna maeneo DODOMA wanaweza wasipate maji wiki hata tatu.
 
Back
Top Bottom