Hivi hakuna kabisa uwezekano wa kuzungumza kuhusu Mungu nje ya msamiati wa kiyahudi?

Ujue kila kitu kina mungu wake. Mimea,wanyama, wadudu nk. Labda miungu hiyo ikae pamoja na kumchagua bisi wa wote . Swala la binadamu huenda kila rangi ina mungu wake ndio maana IQ zinatofautiana. Na huenda kila mtu ana chanzo chake , basi heshimu hicho chanzo ndio ngao yako. Hizi dini ni kanyaga boya .
 
Hivi kaka tutumie nyenzo gani au tupite njia gani ili tuupate huo ukweli ?
Uchunguzi uliojikita katika uthabiti wa kimantiki usiotetereshwa na mahamaniko ya kihisia yanayotokana na upotofu wa kifikra unaoogopa kuhoji kila kitu.

Hoji kila kitu. Hoji dini. Hoji historia. Hoji utamaduni. Hoji mpaka kuhoji kwako.
 
Naomba unipe faida hapo kidogo. Hivi wayahudi wanamuelezea vipi Mungu mpaka wewe ukawaona ni bora katika jambo hilo. Ukinipa na mifano utakuwa umenisadia sana mimi na wale mfano wangu.
Kutoa faida ya maelezo na mifano kwa watu ambao hawaamini hivyo vitabu

Ni sawa na Bure
 
Uchunguzi uliojikita katika uthabiti wa kimantiki usiotetereshwa na mahamaniko ya kihisia yanayotokana na upotofu wa kifikra unaoogopa kuhoji kila kitu.

Hoji kila kitu. Hoji dini. Hoji historia. Hoji utamaduni. Hoji mpaka kuhoji kwako.
Kwanza kabisa naomba unipe maana ya tamko "mahamaniko".

Vipi naweza kuhoji kuhusu dini,kuhoji kuhusu historia,kuhoji kuhusu dini,na kuhoji kuhusu kuhoji kwangu... ?

Kadhalika naomba unipe ukweli wa jambo lolote ulioupata kutokana na maelezo yako.

Au unaweza kuniambia ukweli juu ya kwanini binadamu hatuijui kesho yetu ?

Msaada tafadhali.
 
Kutoa faida ya maelezo na mifano kwa watu ambao hawaamini hivyo vitabu

Ni sawa na Bure
Kaka swali langu liko wazi sana na ni swali la jumla. Sasa unafikiri kama sisi tusiojua yaliyopo katika vitabu vya mayahudi na wewe unajua,ni wajibu wako utupe maelezo ili tupate kujua.
 
Mkanganyiko, ni kweli
 
Kuhamanika ni kuwa na wasiwasi mkubwa juu ya jambo au kitu fulani, kuhangaika, kuhaha, kupatwa na mshawasha kwa kuona jambo ambalo hukutarajia au likuvutialo sana moyoni, kuhaha kutokana na kuzingwa na kazi nyingi.

Neno lina mzizi wa kiarabu.

Maana hiyo ya juu imetolewa katika Kamusi Kuu ya Kiswahili. Baraza la Kiswahili la Taifa iliyochapwa na Longhorn chapa ya mwaka 2015. Ukurasa wa 280.

Unaweza kuhoji kwa kuuliza maswali yanayotafuta uthabiti wa kimantiki.

Kwa kujielimisha kwa njia ya uthabiti wa kimantiki nimepata kujua kwamba huyu Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote tuliyepewa kumuamini, hayupi, ana mikanganyiko ya kidhana ambayo inamfanya asiwezekane kuwepo.

Unaposema hatujui kesho yetu unamaanisha nini? Mbina watu wanapanga miadi ya kesho kama hawajui kesho? Mbina kuna utabiri wa hali ya hewa? Mbina watu wanatabiri kupatwa kwa jua kutakakotokea mamia ya miaka ijayo, siyo kesho tu?

Be specific in your questions please.
 
Asa
Asante kwa kunipa maana ya tamko nililo kuuliza.

Nikisema siku ujue nazungumzia massa 24 kama ilivyo ada.

Je unaijua kasho yako ya masaa 24 ?

Halafu suala la kupanga miadi si kujua bali ni matarajio yaweza yakawa au yasiwe,halikadhalika ni hivyovyo hata katika upande wa tabiri na mfano wake.

Nikisema kuijua kesho yake simaanishi kubahatisha wala kudhania bali namaanisha hakika isiyo na shaka ndani yake.
 
Hiyo midoli yenu itawaueni nyie wenyewe, mizimu yote pumbavu zenu. Tena kuna matusi mengine nimeitukana hiyo mizimu yenu hayaandikiki hapa JF.
Mizimu yote ni mafala
Bujibuji punguza jaziba
 
Hii course ukisoma kubishana na watu wengi hapa kwa usomi ni kazi sana.

Watu wanaandika kwa hisia za kutetea dini zao, zaidi ya kuandika kisomi.
Huwezi kuhoji mambo kwa uhalisia wake kama ukijifunza falsafa na ukaifanya kuwa nyenzo yako ya kupata ukweli.

Ndio maana wanafalsafa wote huwa ni wajinga na hawajui kuitumia akili yao vizuri.
 
Kwa iyo mungu Wa wazungu ananguvu sana.
Kuliko akina sisi Wa Africa
 
Huwezi kuhoji mambo kwa uhalisia wake kama ukijifunza falsafa na ukaifanya kuwa nyenzo yako ya kupata ukweli.

Ndio maana wanafalsafa wote huwa ni wajinga na hawajui kuitumia akili yao vizuri.
Nani kataja falsafa? Falsafa ni nini?
 
Uchunguzi uliojikita katika uthabiti wa kimantiki usiotetereshwa na mahamaniko ya kihisia yanayotokana na upotofu wa kifikra unaoogopa kuhoji kila kitu.

Hoji kila kitu. Hoji dini. Hoji historia. Hoji utamaduni. Hoji mpaka kuhoji kwako.
Wewe ndiyo kinara wa kuona watu hawana elimu kisa wanahoji,kwa maana kuhoji hayo mambo kwako wewe huona ni upungufu wa elimu.
 
Watu hawaijui kesho kwa sababu ya entropy.

The second law of thermodynamics, in context, dictates that entropy tends to increase with time. In closed systems, with the passage of time, we are always moving from a lower entropy state to a higher entropy state.

A higher entropy state is more unpredictable.

Ni kama kuwa na computation ambayo ina trillions of possible different outcomes, halafu unaambiwa uchague moja ambayo itakuja kutokea.

Obviously complexity ya wingi wa outcomes itakufanya uone ugumu kujua litakalotokea.

Kwa hiyo, hatujui kesho kwa sababu ya entropy kuongezeka na muda kama ilivyoelezewa katika Second Law of Thermodynamics.

Kama ulitafuta jibu la Mungu, halipo.

In fact, kutokujua kesho kunaonesha Mungu hayupo kuliko kunavyoonesha Mungu yupo.

Kwa sababu, Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote, asingetujuza kama kuna kesho na hapo hapo kuwa mchoyo wa kutunyima kujua kesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…