Hivi hawa DSTV wanatuchukuliaje Watanzania?

Hivi hawa DSTV wanatuchukuliaje Watanzania?

Terms and conditions zao zinasemaje? Kama ameona ameonewa apeleke complaints kwenye dawati lao.
Nauliza tu, regardless terms zinasemaje. Mfano nakupa menu ya ugali kuku na mchicha, nakupa na bei, kisha unalipa, halafu unaletewa ugali mchicha bila kuku. Halafu mtu akihoji umwambie ni terms and conditions, hiyo ni sawa?
 
Wakati unajiunga si kuna vigezo na masharti unapewa? Kama ukikubaliana na hivyo vigezo na masharti ndio unajiunga.
Ndio maana nasema kama umeona umeonewa mbona kuna sehemu ya kuwasilisha malalamiko ikiwemo ndani ya kampuni lakini pia hata kwa regulatory authority ambae ni TCRA.
 
Channels zipi za Compact zilizohamishiwa Compact+ ?
 
We mbona muongo sana?unahisi uongo utakusaidia nini?ch 223 ipo COMPACT
Channel zinabadilika kutokana na decoder ya mtu.Na hiyo hutokea kama wakiona unaipenda Sana channel flani kusudi uongeze PESA Ili Ile channel Yako pendwa uendelee kuiangalia.
 
Wakati unajiunga si kuna vigezo na masharti unapewa? Kama ukikubaliana na hivyo vigezo na masharti ndio unajiunga.
Ndio maana nasema kama umeona umeonewa mbona kuna sehemu ya kuwasilisha malalamiko ikiwemo ndani ya kampuni lakini pia hata kwa regulatory authority ambae ni TCRA.
Mimi sijabisha juu ya vigezo na masharti, nimeuliza tu, je, kitendo hicho ni sawa?
 
Dish wanauza elfu 59 halafu kifurushi elfu 90
Wakati azam ni laki 210 ila kifuruzhi elfu 20 unapata Chanel's za michezo na burudani zote yaani hapo ndo naona kabisa hawaeleweki DSTV.
 
Dish wanauza elfu 59 halafu kifurushi elfu 90
Wakati azam ni laki 210 ila kifuruzhi elfu 20 unapata Chanel's za michezo na burudani zote yaani hapo ndo naona kabisa hawaeleweki DSTV.
DStv ni ya matajiri... Kama uchumi wako WA kuunga unga DStv ni ya moto.

Unalipia elfu 90 Bado baadhi ya channel wanakubadilishia ,Wanataka ulipe zaidi Ili uweze kuziona hizo channel[emoji2]
 
Salaam WanaJF!

Hivi hawa jamaa wa DSTV (Multichoice) wanatuchukuliaje Watanzania!? Kwamba wanatuchukulia tupo vizuri sana kiuchumi, ama wanatuchukulia sisi washamba sana au inakuwaje!?

Kila siku wanafanya kuzichezesha chaneli zao ndani ya DSTV, sio kitu cha ajabu kukuta chaneli yako pendwa imehamishiwa katika kifurushi kingine ambacho ni cha gharama zaidi.

Yaani Kifurushi cha COMPACT ambacho tunalipia Tsh 50000+ kwa mwezi nacho kimeshakuwa useless, chaneli pendwa wamezisogeza kwenye kifurushi cha COMPACT plus ambacho unatakiwa kulipia Tsh 90000+ kwa mwezi.

Huu ni utapeli kwa Watanzania, sijui mnatuchukuliaje DSTV!!?
Nakazia!
Hata mimi nmeona hili pia.
 
Kuna wakati kujiona mjanja na mwerevu ndio huwa Ujinga wenyewe.
Mjomba, kwahiyo kama tangu zamani watu wanailalamikia DSTV kwa hili jambo, kwa wakati huu mimi natakiwa kukaa kimya!? Niaje aisee? Kwahiyo kwako wewe werevu na ujanja ni kukaa kimya!?
 
We mbona muongo sana?unahisi uongo utakusaidia nini?ch 223 ipo COMPACT
Tulia kwanza mkongwe, uliza vizuri kabla haujaanza kunishushia tuhuma za uongo.
Screenshot_20220415-080725.png

KWENYE PICHA UPANDE WA KUSHOTO NI PACKAGE YA COMPACT PLUS, UPANDE WA KULIA NI PACKAGE YA COMPACT

Kabla sijajiunga tena na package nina tabia ya kuingia web ya DSTV kucheck kama kifurushi nitakacholipia kitakuwa na channel yangu pendwa, kwenye picha hapo ndio hali niliyokutana nayo jana. Hapo kwenye picha Supersport PL (223) inaonekana kwasasa inapatikana katika package ya Compact plus, kwenye package ya Compact haipo, imewekewa x. Labda kama wewe ni staff wa Multichoice TZ uniambie hayo ni makosa tu yamefanyika kwahiyo nilipie tu package ya Compact nitaipata channel ya Supersport PL.
 
Mimi sijabisha juu ya vigezo na masharti, nimeuliza tu, je, kitendo hicho ni sawa?
Mkuu kama sio sawa wasilisha complaints zako kwenye dawati husika watakusaidia. Hawa DStv ukiwapigia simu wanaushirikiano watatatua changamoto yako.
 
Channel zinabadilika kutokana na decoder ya mtu.Na hiyo hutokea kama wakiona unaipenda Sana channel flani kusudi uongeze PESA Ili Ile channel Yako pendwa uendelee kuiangalia.
Tangu nimeanza kutumia Dstv, hii habari ndo naisikia kwako kwamba kila mtu ana access na channel zake kwenye decoder 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom