Hivi haya mabanda ya Machinga kila kona Dar wameshindwa kuyadhibiti?

Chukueni Kama Sera ya Upinzani, kwamba uchaguzi wa 2025 mtawaondoa wote kuweka majiji/miji Safi. Ni kweli ni Uchafu na kiuchumi ni upotevu wa mapato ya kikodi,
 
Ukienda city centre maeneo ya kuanzia DIT mabanda kila kona hadi machizi wanalala humohumo.
Kwahiyo mkuu Machizi wamekukosea nini mpaka kuwahusisha hapo?

Unataka walale wapi haswa kipindi hiki cha mvua?

Umeshakua na ndugu umpendaye halafu ni chizi akatoroka nyumban ukawa na wasiwas anaishije?

Hujui uchizi ni ugonjwa? Kwamba unaweza kukupata hata wewe? Hata mimi ni chizi, sisi tunalala kwenye hayo mabanda ili kujihifadhi kwakua na sisi bado ni binadamu na tuna mahitaji Yale Yale mahitaji ya kibinadamu malazi,chakula, mavazi no

Bila haya mabanda ningekua kwako kukugongea kwamba nihifadhi ungekubali??

Ongelea Ishu ya machinga ambayo ni kero ya kila mtu. Ila machizi kulala kwenye banda analolikuta liko wazi kujihifadhi usituseme tafadhali
 
Hao ni wapiga kura wasibughudhiwe.
Hao ni zao la sera za ccm zilizofeli kwenye kuzalisha ajira. Hao ilitakiwa wawe kwenye uzalishaji na sio kwenye uchuuzi yaani kuwa madalali wa viwanda vya china
 
Serikali isiyotengeneza miradi mingi ya maendeleo lazima izalishe wachuuzi jamii ya machinga kwenye miji mikubwa.

Serikali ya sasa ya awamu ya tano imewekeza kwenye miradi mikubwa ya maendeleo hususani lwenyenkila mkoa ili kila mkoa wa nchi uweze kutoa mchango sawa kwenye kujenga uchumi wa nchi hivyo vijana ambao ndio nguvukazi ya Taifa watashiriki kwenye shughuli za kiuchumi huko huko walipo bila kuwa na mawazo ya kuja dar na kufanya biashara ya umachinga.

Ni kipindi ambacho watu wa mjini watapeleka mitaji vijijini kwenye umeme wa kutosha,miumdombinu ya usafirishaji iliyoimarika na kadharika.
 
Tatizo na siyo tatizo... hakuna taratibu na upimaji wa banda!! Ilimradi ukiokota kiroba funika..ukijipatia Tamara chakavu zine.. ukijioatia bati bovu ekeza..hata mifuko ya plastiki wewe tandaza !! Yaani banda sii banda
Wala chaka si chaka..ni kama dampo la taka....
Ahsante manispa
 
Tatizo na siyo tatizo... hakuna taratibu na upimaji wa banda!! Ilimradi ukiokota kiroba funika..ukijipatia Tambara chakavu Ziba .. ukijiokotea bati bovu ekeza..hata mifuko ya plastiki wewe tandaza !! Ukipata torubali chafu bandika ....Yaani banda sii banda
Wala chaka si chaka..ni kama dampo la taka.taka...
Ahsante manispa.. hii ni kudharaulisha hadhi ya Jiji na miji...
 
Mi naona.....

Biashara zifanyike ila na utaratibu ufuatwe

Badala ya kujenga mabanda barabarani wachuuzi wote wapelekwe sokoni.
 
Maelekezo ya Jiwe, ni nani atakayetengua?

Ulaya yenyewe hajawahi fika!
 
Eti Hadi Chicago[emoji16][emoji16][emoji16]

Bongo kweli bahati mbaya! Unatetea upuuzi halafu unajiona bonge la mjanja.
 
Failing state, failing leadership....

Inasikitisha Sana Tanzania ya magufuli.
 
Acha ujinga ww......
binadamu mwenye akili anatakiwa apangilie mambo......
sio kufanya biashara hovyo hovyo Alaa!!
Nani mwenye Akili kwenye dunia hii Kama U,S,A na England,Rusia German Watu hawana pakulala na hawana vyoo na maisha yanasonga.Tatizo lako unakula bure na hujawahi lala njaa ndiyo maana unaongea Upuuzi wako .Toka shule ya msingi mpaka chuo kikuu Umesoma Private na hujawahi fukuzwa Ada halafu unakuja kubwabwaja hapa eti tuwe wastaarabu tupange mji kuwe Kuna masoko maalum hivi Unafikiri yule mlinzi anayelinda pale Morocco bus terminal na Morocco square au anayelinda pale Airtel anawza kwenda Kula Best bite? Acha Upuuzi uwe Unafikiri vizuri hao walinzi tunawategemea Sana na ndiyo wanaokula kwa hao mama ntilie pale kando ya barabara ,Umesahau kuwa maji ya kwenye hotel yanauzwa Bei ghali Sana Hali inawafanya hotelia wengi kununua maji ya kunywa nje ya hotelia yao?.Acha Upuuzi wewe Mtoto wa mama Unafikiri wale mafundi ujenzi Kule Masaki wanaweza kuingia hotelini sea clif kununua chakula ?. Acha Utoto angalia Hali halisi ya maisha kwa ujumla siyo siyo unachungulia tu .Maisha ya Nchi yakiwa Mazuri huwa yanajiseti yenyewe tu siyo kuamrishwa Kama vile unavyoona Watu walivyopungua kwenda internet cafe,kunyoa nywele kichwani kwa viwembe .
 
Hii ni U.S.A taifa lenye nguvu kubwa duniani .Eti kitoto Cha Bunju kinapiga kelele hhoo hee ustarabu .
 
Baseless..pointless !!
Sisi tutazame yetu na majiji yetu..
USAFI na tutunze mazingira yetu.. tusinyamaziane au kubebana ktk uendeshaji na utendaji.
Hoja dhaifu unatazamaje yenu wakati kituo kikubwa Cha mabasi kipo Morroco halafu unataka Machinga wakakae Jangwani na unasahau kwenye Mikusanyiko wa Watu ndipo Kuna wateja .Muwe mnawaza kwa upana siyo kiporojo au mnaona raha Watu wakifa njaa kwa kujifanya kuwa mmestarabika kiujinga.Wewe Kama umekulia maisha laini usifikiri wote wanayo hayo maisha .
 
Kwa hiyo unapindisha SHERIA za mipango miji?
Hivyo mabanda na uchafuzi udumu.. hatimae kufika hadi ikulu nk nk..( kwa sbb ya kupata chai na iishe ya mamantili)?
 
Shida sio WAMACHINGA WASIFANYE BIASHARA BALI MABANDA YAJENGWE KWA UTARATIBU UNAOHESHIMU MAZINGIRA, BARABARA NA WATEMBEA KWA MIGUU.
Idadi ya wateja (walaji) ni ile ile hata wakijenga mabanda mengi kama mchwa
 
Mwenye shibe hamjui mwenye njaa!!!

Ni kero hasa wanapoingia hadi kwa watembea kwa miguu but ukweli ndo huo,kwa sasa hakuna alternative way ya kufanya vijana wasukume maisha yao coz kama ni ajira hamna sasa kumbe wafanye nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida sio WAMACHINGA WASIFANYE BIASHARA BALI MABANDA YAJENGWE KWA UTARATIBU UNAOHESHIMU MAZINGIRA, BARABARA NA WATEMBEA KWA MIGUU.
Idadi ya wateja (walaji) ni ile ile hata wakijenga mabanda mengi kama mchwa
Kwahiyo unataka mwenye Tigo pesa ajenge Banda sawa na muuza miguu ya kuku na utumbo au Muuza leso za mtaji wa Elfu tano ajenge Banda Kama la Muuza mabegi.Halafu mnakaa mtaani nhoooo Mimi nimesoma Uchumi Eenhhe Mimi nyonyonyo Akili za hovyo kabisa wewe unaona kabisa Watu aliokaa pale hata wengine kununua tu Mwamvuli tu wanashindwa wanachomeka na jua muda wote halafu umwambie ajenge Banda .Hivi nyie Watu mnasomaga vyuo gani Hivyo mpaka mnafundishwa Upuuzi namna hiyo!!!!??.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…