Hivi haya mabanda ya Machinga kila kona Dar wameshindwa kuyadhibiti?

Hivi haya mabanda ya Machinga kila kona Dar wameshindwa kuyadhibiti?

Bila mabanda vijana wasio na ajira watafanya nini? Kuna nguvu kazi kubwa kuriko uchumi unavyoweza kuwatumia, nguvu kazi kubwa lakini uwezo wake unatumia kwa asilimia 5 tu,kila kijana anayeingia kwenye soko la kazi, lazima atatafuta Cha kufanya, apake rangi za kucha, auze leso mbili, atauza nyanya fungu mbili, atauza mahindi

Lakini ni shughuri ambazo hazikizi mahitaji yake muhimu, badala ya kuzalisha 100, uchumi unampa nafasi ya kuzalisha 10 tu, ndio hayo mabanda
Watu wachafu utawajua tu.
 
Kwa hiyo unapindisha SHERIA za mipango miji?
Hivyo mabanda na uchafuzi udumu.. hatimae kufika hadi ikulu nk nk..( kwa sbb ya kupata chai na iishe ya mamantili)?
Hiyo mipango miji inakusaidia nini ikiwa Watu wako wanalala na njaa .Sheria unatakiwa iwe unaleta ustawi wa jamii siyo kukomoa jamii .Yaani wewe unaweka Sheria inauowafanya Watu washindwe kufanya kazi Unafikiri unawasaidia au unawaangamiza. Sheria za hovyo na zisizoipendeza jamii ni batili na zikiendelea kulindwa huwa zinassbabisha Mapinduzi rejea mbalimbali duniani.
 
102011131.jpg
 
Kwa kweli taswira ya jiji imeharibika sana. Sokoine drive mbele ya Mahakama ya Rufaa, Kempiski hotel mpaka feri kuna mabanda machafu sana. Watu wanapanga mafungu ya bamia na matembele kwenye njia ya waenda kwa miguu.

Hata kama ni haki ya Wajasiriamali kufanya biashara. Si busara kuchafua kila mahali kwa mabanda na hasa mji mkongwe(maeneo ya posta) bora kuwe na sehemu yao maalum.

Mama lishe pia wanapika kwa kuni kila sehemu mjini kati. Lazima kuwe na udhibiti.
Kwakuwa umemaliza shule ukapata ajira wala hujawahi lala njaa unaona maishs rahisi Sana. Wenzako waliopitia msoto wameona maisha yasonge Watu wajishighulishe.Wewe unakuja oonhoo nyonyonyonyo kuni zimefanyafanyagani? Upuuzi mtupu. Ubishoo tu ambao hauns maana .
 
Pamoja na yote hayo hakuna aliyegongwa na gari na maisha yanasonga tu Watu wanapiga hela na Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Uchumi Kama hapa Tz IFM na CBE kutoka Mozambiq na Angola wanakuja kujifunza huo mfumo wa Uchumi na kuupeleka kwao wewe bado unabwabwaja tu huna unalolijua .
Una miaka mingapi chief?
 
Hoja dhaifu unatazamaje yenu wakati kituo kikubwa Cha mabasi kipo Morroco halafu unataka Machinga wakakae Jangwani na unasahau kwenye Mikusanyiko wa Watu ndipo Kuna wateja .Muwe mnawaza kwa upana siyo kiporojo au mnaona raha Watu wakifa njaa kwa kujifanya kuwa mmestarabika kiujinga.Wewe Kama umekulia maisha laini usifikiri wote wanayo hayo maisha .
Kwani kabla ya kujenga hayo mabanda barabarani mlikuwa mnakula wapi?
 
Kwani kabla ya kujenga hayo mabanda barabarani mlikuwa mnakula wapi?
Watu wengine sijui mnawaza Nini Yaani umesahau mama na Baba zetu Dada na Kaka zetu tokea miaka ya 2000 walivyokuwa wakipigwa na kudhalilishwa na Mgambo wa jiji na mabanda kubomolewa na masufuria yao kubebwa . Eti sahizi unauliza tulikuwa tunakula wapi ?
 
Ukiwa unakula bure au amemaliza tu chuo na kupata ajira huwa mnaona Maisha rahisi Sana na unakuja na viushauri vya kipuuzi na unasahau kuwa Kuna wenzako toka wamalize chuo hawajapata hata laki tano na imeshapita miaka kumi.

Huku tunakotafuta ridhiki Kuna Mambo mengi Sana nakushauri inakusaidia nini kupendeza usoni wakati huna uhakika wa Kula. Pakishapendeza hapo Morocco panawasaidia nini walala hoi .Acha ujinga Watu wanaishi maisha duni Sana na wanatafuta wateja popote walipo wamuuzie angalau hata pipi na karanga ili apate faida ya kupata kununua unga ale na wanae.

Siku ukimuona mama kabeba mtoto mgongoni na kajitisha beseni anauza mihogo au dizi ujue huyo anatafuta hela ya Kula tu siyo kufanikiwa. Acha dharau kwakuwa hujawahi lala njaa waliwahi kusota ndiyo waliowaruhusu hao Watu wafanye biashara maana wanajua nini maana ya njaa.
Hoja yako inatia kichefuchefu aisee. Kwani marais wengine waliopita walikuwa wanatatua vipi kero za machinga? Kila siku population inaongezeka. Km solution ya Machinga ni kuwaruhusu wavamie barabara na maeneo ya wazi ipo siku barabara zote zitakuwa hazipitiki. Na hapo ndipo zitaibuka kero zingine mbaya zaidi km ajali,uchafu uliokithiri na magonjwa ya mlipuko.

Mbaya zaidi kuna masoko yamejengwa kwa gharama kubwa yapo tupu watu wamekimbilia barabarani. Kisa eti kutetea wanyonge!
 
Akili ndogo elimu ya kukariri inakusumbua. Mtu mtaji wake Elfu 20 unataka akodi fremu milioni moja ya bei nafuu laki moja .Halafu unajiita Msomi sijui huwa mnafanya Nini huko shule!!!?
 
Akili ndogo elimu ya kukariri inakusumbua. Mtu mtaji wake Elfu 20 unataka akodi fremu milioni moja ya bei nafuu laki moja .Halafu unajiita Msomi sijui huwa mnafanya Nini huko shule!!!?
Wamachinga mpk down town
Mji unaonekana mchafu.....

Ova
 
Ukiwa unakula bure au amemaliza tu chuo na kupata ajira huwa mnaona Maisha rahisi Sana na unakuja na viushauri vya kipuuzi na unasahau kuwa Kuna wenzako toka wamalize chuo hawajapata hata laki tano na imeshapita miaka kumi.

Huku tunakotafuta ridhiki Kuna Mambo mengi Sana nakushauri inakusaidia nini kupendeza usoni wakati huna uhakika wa Kula. Pakishapendeza hapo Morocco panawasaidia nini walala hoi .Acha ujinga Watu wanaishi maisha duni Sana na wanatafuta wateja popote walipo wamuuzie angalau hata pipi na karanga ili apate faida ya kupata kununua unga ale na wanae.

Siku ukimuona mama kabeba mtoto mgongoni na kajitisha beseni anauza mihogo au dizi ujue huyo anatafuta hela ya Kula tu siyo kufanikiwa. Acha dharau kwakuwa hujawahi lala njaa waliwahi kusota ndiyo waliowaruhusu hao Watu wafanye biashara maana wanajua nini maana ya njaa.
Mtu anakwambia huwezi ishinkwa kuuza dodoki. Hivi kuuza dodoki kungekuwa hakumsaidii mtu kila siku angemkuta hapo.
Mtu akishazaliwa kila kitu anakikuta anaona maisha ni rahisi sana.
Kusema mtu awekewe utaratibu ni sahihi na hili sio kosa la machinga. hawaandaliwi maeneo na hata wakiandaliwa bei zinakuwa sio rafiki kwa muuza dodoki kulipia eneo. Na biashara ndogo ndogo za machinga huwa ni za kufata watu walipo. Mtu ni ngumu kutoka nyumbani eti anaenda kununua dodoki. Ni anatoka kwenye mambo mengine anakutana nayo ananunua hapohapo. Ila si kumletea dharau mtu kwenye biashara yake ili hali hata akikuomba mtaji wa kufanya hizo biashara za hadhi hawezi msaidia.
 
Barabara ya Uhuru toka Ilala boma mpaka stesheni hakuna njia za waenda kwa miguu.sehemu zao zote wameweka vimeza vyao.harafu wanajua kujenga hivyo vimeza vinatosha kabisa.Kilichofanyika sasa waenda kwa miguu wanapita barabarani wanahatarisha maisha mbaya sana.

Halafu vile vibajaji mataa ya msimbazi na uruhu ni kero nyingine kabisa. Ukipita town mamlaka za majiji zimeishia kushika wrong parking za wastaarabu wenye magari tu.

Hii imenikera sana wamenitoa Elfu 50 kwa wrong parking wakati legal parking zote ni stendi za bajaji sasa tutapaki wapi ila dar hasa kariakoo kuna upumbavu
 
Hìi sio solution. Watu kuweka mabanda mabaya barabarani sehemu ya wapita njia haiwasaidii lolote. Tena wengi wao watakuwa wanafanya shughuli haramu ili kukidhi mahitaji yao, huwezi kuishi kwa kuuza dodoki barabarani.

Bora watengewe maeneo ya masoko kwasababu kama ni sokoni watu wataenda tu kwa wingi na faida watakayopata itakuwa kubwa zaidi.
Siungi mkono utaratibu mbovu lakini,
acha dharau.. "Hawezi ishi kwa kuuza dodoki barabarani", kila siku ungekuwa unamkuta hapo?
 
Hata siku moja machinga hauzi sokoni. Duniani kote hili la kuhamisha machinga kwa kuwajengea au kuwatengea soko halijawahi fanikiwa. Hata sijui ni kichwa maji gani alimshauri JK kujenga machinga complex.
Kanuni ya machinga ni huwa anafata watu walipo sio watu wamfate yeye. Ila hata kama vibanda vinawekwa basi viwe katika hali ya usmart. Na maeneo yaliyofinya sana si lazima viwepo.
 
Watu wengine sijui mnawaza Nini Yaani umesahau mama na Baba zetu Dada na Kaka zetu tokea miaka ya 2000 walivyokuwa wakipigwa na kudhalilishwa na Mgambo wa jiji na mabanda kubomolewa na masufuria yao kubebwa . Eti sahizi unauliza tulikuwa tunakula wapi ?
Kabla ya huo mwaka 2000 mlikuwa mnakula wapi?

Nakuulizia hya sababu nakuona kabisa bado upo ndani ya box, hutaki kufikiri options zingine kwenye maisha zaidi ya kuuza vitu barabarani.

Waulize hao ndugu zako tokea mwaka 2000 wanafanya umachinga mpaka Leo hawajapata mtaji wa kufanya biashara inayoeleweka?
 
Nataka Dar iwe kama Ulaya.

Rais wetu alikua anasisitiza sana ila nahisi hawa watendaji wake hawamuelewi.

Wamachinga wameharibu uzuri wowote wa Dar ambao mtu angeufurahia kasoro tu eneo la jeshi lugalo ndio mtu ukipita unafurahia.

Flyover Ubungo ukigeuka tu pembeni ukiona mabanda ya machinga utam wote kwisha. Mlimani City ndio kabisaa ni takataka. Ukienda city centre maeneo ya kuanzia DIT mabanda kila kona hadi machizi wanalala humohumo.

Haya saizi Bagamoyo Road kuanzia Mwenge hadi Morocco pameanza kupendeza ila nawaambia soon uzuri wote unaisha machinga wanahamia. Hivi hizi mamlaka haziendi hata hapo nairobi tu zikajifunze vitu vidogo kama hivi? Ndio ulaya tutaifikia kweli?

Hatusemi biashara zisifanyike, ila tafuteni utaratibu sehem za uso wa barabara kuu zibaki zinavyopendeza. Au basi mtangaze maeneo yote ya mbele ya barabara kuu ni ya jeshi ili machinga waondoke wenyewe pabaki pazuri kama Lugalo.
Na wewe uliamini porojo za magufuli kwamba Bongo inaweza kuwa kama Ulaya ?
Kwa IQ ipi waliyonayo watawala wenu hawa mafisadi mtupu
 
Nataka Dar iwe kama Ulaya.

Rais wetu alikua anasisitiza sana ila nahisi hawa watendaji wake hawamuelewi.

Wamachinga wameharibu uzuri wowote wa Dar ambao mtu angeufurahia kasoro tu eneo la jeshi lugalo ndio mtu ukipita unafurahia.

Flyover Ubungo ukigeuka tu pembeni ukiona mabanda ya machinga utam wote kwisha. Mlimani City ndio kabisaa ni takataka. Ukienda city centre maeneo ya kuanzia DIT mabanda kila kona hadi machizi wanalala humohumo.

Haya saizi Bagamoyo Road kuanzia Mwenge hadi Morocco pameanza kupendeza ila nawaambia soon uzuri wote unaisha machinga wanahamia. Hivi hizi mamlaka haziendi hata hapo nairobi tu zikajifunze vitu vidogo kama hivi? Ndio ulaya tutaifikia kweli?

Hatusemi biashara zisifanyike, ila tafuteni utaratibu sehem za uso wa barabara kuu zibaki zinavyopendeza. Au basi mtangaze maeneo yote ya mbele ya barabara kuu ni ya jeshi ili machinga waondoke wenyewe pabaki pazuri kama Lugalo.
Ahadi ya mzee baba hiyo!
 
Yani ugumu wa maisha ulivyo, unataka nani atolewe kwenye vibanda wstakula wapi, ugumu wa maisha umewekwa na hali ya uchumi, ndiyo maana mkuu hawezi kuwavukuza
 
Back
Top Bottom