Hivi haya majina ya vitu vipya kwa Kiswahili nani huwa anatunga?

KISHKWAMBI ni neno tulikua tunatumia zamani zana 90s likimaanisha mtu mwenye kiherehere au anayeingilia mambo yasio muhusu
 
Friji inaitwa Jokofu
 
Yaani Kwa teknolojia wanafeli Majina ya Kiswahili. Afya ndio Usiseme. Mambo ya kimedicine inaleta lugha za Ajabu Ajabu. Selimundu
 
K
KISHKWAMBI ni neno tulikua tunatumia zamani zana 90s likimaanisha mtu mwenye kiherehere au anayeingilia mambo yasio muhusu
Kwa Wapate ni tusi. Huwezi tamka Upareni hiyo Kishi kwambi.
 
Drones wataita ‘ndege janja’
 
Juice ni sharubati na sio kinywaji tamu😆
 
Mkuu haya maneno wanayatoa wapi maana wakati vitu vipya vinaundwa hayakuwepo
 
Haya maneno ni magumu kama sio kiswahili vile halaf kutohoa maneno kutoka lugha nyingine sio dhambi eng kina maneno mengi tu ya kigiriki kikatin
 
Wako sahihi kabisa wanaeupaka kutohoa kila neno kutoka lugha za kigeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…