Hivi haya majina ya vitu vipya kwa Kiswahili nani huwa anatunga?

Sio magumu , kwa mtazamo wangu, Ila hatuja yazoea. Mbona, 'kifungashio' , 'barakoa' 'mubashara' yameshazoeleka.'!
Cha Msingi BAKITA waendane na ukuaji wa teknolojia, msamiati ukitoka
 
Mambo ya teknolojia yabaki kwenye lugha anzilishi, watu wanavumbua vitu sisi kazi yetu kuvibatiza majina tata, sidhan kama ni sawa
 
Sio Juisi ni Sharubati [emoji3][emoji3]
 
Neno lingine 'uke' huwa haikai ndo maana huwa halitumiki, sujawahi sikia mtu akitukanwa 'uke wewe'

Lakini nani? Hajawahi sikia mtu akitukanwa 'kkuma wewe'

Hata kiingereza sio kawaida kusikia mtu akitukanwa vagina lakini ni kawaida kusikia cu*t au pu**y
 
Mfulumbato = Clutch
 
Drone-ndege tiara
 
Neno lingine 'uke' huwa haikai ndo maana huwa halitumiki, sujawahi sikia mtu akitukanwa 'uke wewe'

Lakini nani? Hajawahi sikia mtu akitukanwa 'kkuma wewe'
Sasa uke si ni neno rasmi, ungesoma biologu katika shule za msingi za serikali, ungesikia hilo neno ila inaonekana umesoma english medium, darasani mwalimu hawezi kutumia neno k*ma, ama b*lo, darasani huko darasa la sita walimu hutumia maneno uke na uume
 
Haya maneno ni magumu kama sio kiswahili vile halaf kutohoa maneno kutoka lugha nyingine sio dhambi eng kina maneno mengi tu ya kigiriki kikatin
Kila lugha duniani ina maneno mepesi na maneno magumu (Kiswahili, Kilatini, Kigiriki, Kihadzabe, n.k).

Labda muwe na hoja nyingine, ila hii ya kutaka kiswahili kiwe na maneno yote mepesi mepesi (kwa kutohoa toka lugha zingine) mimi sioni kama lina mashiko.

Na ukipenda sana vitu laini laini, tepetepe au ndembendembe, utaanza kuamini hata neno "MFUNGWA" ni gumu mno, utapendekeza watu waliohukumiwa kutumikia adhabu gerezani waitwe "PRIZONA."

Sio sawa.

Kishkwambi daima, Kishkwambi milele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…