Mark Zuckerberg anamiliki Facebook na instagram lakini yeye aliamua awe ananunua na kuvaa t-shirt za aina moja kila siku ili asubuhi asipoteze muda mwingi kuchagua nguo ya kuvaa, kwhyo kila siku anaonekana hajabadilisha t-shirt had watu wamemkariri ila hajali ye anaangalia mambo yake muhimu.
Wanaume wengi tunakuaga hivyo mwenye nguo nyingi ana shati/t-shirt 4, suruali 4, na viatu pea 3, unachotakiwa kuzingatia ni rangi ya nguo tu usipende nguo zinazo waka sana ukawa unaonekana kwa mbali Kama demu, shati 1 isipochafuka unavaa leo na kesho yaani siku mbili hapo maana yake wiki nzima inaisha hujaonekana na nguo moja mara nyingi
Kiatu kisipochafuka Kama we ni sharobaro unavaa siku 3 Kama ni mgumu mwenzetu unavaa wiki 1, ukirudi pale kwenye nguo kila ukibadilisha unafua usirundike nguo ndani, alaf wiki inayokuja unabadilisha suruali uliyo ivalia t-shirt flan wiki iliyopita unaibadilishia t-shirt, yaani hapo unamaliza mwaka mmoja hakuna anae kukariri kwa mavazi.
Mwanaume kuwa na nguo nyingi sana ni dalili ya kuleft group