Hivi hii Tabia ya wanawake (wake zetu) kuacha simu ovyo ni ya wanawake wote ama mimi tu?

Sahihi mkuu kuna muda huwa natumia simu yake hata siku 2 akipigiwa ndo nampa na sijawahi ona shida.Changamoto ni hiyo moja wewe una shida hapo nyumbani na simu haipokelewi aisee unakereka hadi basi
 
Majukumu mkuu yqnamweka busy hakumbuki mambo ya simu tena unatakiwa ushukuru Mungu hana mambo mengi huyo ila inaonekana hujamweka chini seriously na kumweleza kwamba hii changamoto inakukwaza sana naamini akiona userious wako atabadilika
Mwanzani nilikuwa nataka hadi kumpiga kwa hasira maana leo umesema wee baada ya siku moja anauria lakini nikwambie mbinu zote hadi kumnyang'anya simu nimewahi lakini wapi.Ina kera basi tu
 
Mkuu ulikuwa unatikisa kiberit au unatafuta kiki kwa pikpiki
 
Huu ugonjwa nahisi kwao hauna tiba. Yaani nilijua ni mimi tu huku.

Mpaka unabaki kumuuliza hiyo ni simu ya mezani ama?
 
Mimi nilipokuwa na michepuko nilikuwa natumia akili nyingi kwa ajili ya kuficha simu na kufuta msg haraka sana.
Baadaye nikagundua najipa kazi ya bure maana mke wangu hata simu yake yenyewe hana mpango nayo.
Mkuu ulichosema nikweli mimi simu yangu akiishika basi anaingia youtube huko maana yangu bando ni nadra kuishiwa
 
hapana sio wote! ni wale wanawake waliostaarabika na kuheshimu ndoa zao!

Hawa wengine mkia wa ngiri juu wenye michepuko kibao simu ipo mkononi 24/7 na akilala inawekwa chini ya mto.. Passiword kila kona..ana mpaka dating apps hatari sana
Sasa mwanamke wa namna hiyo hiyo unapata wapi uhalali wa kumuita mke wako!!

Kuna uzi humu mwanamke na mme wake walikutana kwenye group la wasap la dating nikiupata nitauweka hapa
 
Sasa mwanamke wa namna hiyo hiyo unapata wapi uhalali wa kumuita mke wako!!

Kuna uzi humu mwanamke na mme wake walikutana kwenye group la wasap la dating nikiupata nitauweka hapa
wanawake wengine wana tabia ya kubadilika kadri muda unavoenda unakuta anaanza ku adapt tabia za kuficha simu e.t.c lazima kuna situation kama hiyo kwenye mahusiano.
Ndo maana nasema kuwa wanaume wengi sahizi wanaoa basi tu
 
Mkuu mimi huwa napiga mara2 au mara moja then napiga kwa jirani yangu wanaagizwa wtoto kumstua na nimeshazoea pia maana ubabe haukusaidia kitu
 
Ila wanawake mlio wengi mnazingua sana kwenye hii kesi ya kuacha simu mbali na nyinyi kuwa busy na mambo yenu! Mimi nisipokuwa tu na simu, naanza kujisachi muda huo huo mwili mzima.
wao hawajari hata ulalamike namna gani atajifanya kakuelewa kesho yake mwendo uleule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…