Hivi hii Tabia ya wanawake (wake zetu) kuacha simu ovyo ni ya wanawake wote ama mimi tu?

Believe it or not, huyo ndie mwanamke sahihi wa maisha ya NDOA.
Unaweza usinielewe leo, ila jitahidi asibadilike.
Mkuu nikweli sijawahi ona kiashiria chochote kiovu. Ila changamoto ni hiyo tu asee inakera sana hasa ukiwa na issue ya muhimu.Nikiwa najibu uzi hapa kwenye saa2 nimepiga simu nimkumbushe kuweka chakula cha vifaranga simu haijapokelewa mara3 amenipigia saa3 wanaenda kulala na aksema simu ilikuwa kitandani! leo hii hii nikiwa najibu uzi hapahpa....
 
Mkuu kuna vitu vya muhimu unataka uwasiliane na mkeo muda huo na unapiga simu haipokelewi
hujui huwa wanakera sana
Ni kweli ila mshukuru Mungu angalau changamoto yako ni hiyo. Kuna changamoto zinazovumilika na at least zina plan B (unaona kwamba unaweza kupiga simu kwa jirani na ukampata).

Wenzio wenye wake zao ambao kila siku wanatuletea visa vya kutuacha midomo wazi humu na kutoa points za kutosha kwa TEAM KATAA NDOA kwa % kubwa simu huwa zinahusika, hasa simu janja.

Sasa kama wa kwako hakuona uspesho wowote wa simu janja hadi ukamnyang'anya na kumpa kiswaswadu lakini nacho bado ni yaleyale ni jambo la wewe kumshukuru Mungu na kuvumilia changamoto zake. Siku akizoea simu atakuomba umpatie simu janja, na hapo itakuwa ni warning sign kuwa kabla hata hujakufa mambo yameanza kuharibika.

Zingatia pia bandiko lako limekuwa lalamiko pekee la ndoa hivi kwa kipindi kirefu humu ambalo halijatoa points kwa kataa ndoa😁
 
Yaani tupike na simu unataka tulipukiwe mkuu?
Majukumu yetu ya nyumbani hayaturuhusu kukaa na simu
Kufua ,kupika ,kusugua mabafu nk
Labda Fanya hivi mnunulie smart watch ya water proof anayoweza kupokea simu
Mi nauza 120,000 tu
 
Mhh sio wote yuko huyo shemeji yangu hujamaliza kuandika kisha jibu naona unaandika vipi tena yaani huyo mtumie hata msg saa 9 usiku anakujibu mpaka unashangaa hana kazi na mume wake yupo wapi. kwa ufupi anashida hakuna habari ikampita mpaka namuonea huruma sijui ndoa kama ataiweza. Nadhani bora ya huyo unayemuongelea.
 
Nadhani asilimia 98 ya wanawake wapo hvo..mimi wakwangu hata pesa ukimpatia utakuta anaweka hovyo mara dirishani mara nje uwani kwenye mawe mara sebuleni kwenye masufuria..hii tabia vip wanawake wengine wanayo?Simu ndo usiseme anaweza weka juu ya paa akasahau,, nimeamua kuwa mpole tu.
 
Wengi wapo hivyo, unatakiwa umpe training na mafunzo maalumu ya kutumia simu. Usitegemee atakuwa nayo mkononi saa zote ila mzoeshe kuwa kuna muda fulani lazima utapiga na yeye ategemee simu yako hata kama hautapiga basi yeye akupigie hata kukusalimia.

Nilipata hii shida ila baada ya kutoa mafunzo maalumu na kumkazia kwasasa mimi nisipopiga nikiwa kimya huwa naulizwa why nipo kimya siku nzima why sijamtafuta au leo nipo busy na jambo gani.

Mjengee utamaduni labda ikifika kila kuanzia saa tatu hadi saa tano asubuhi lazima upige,then mida ya lunch kuanzia saa saba hadi saa tisa utapiga tena, then utampigia kabla haujatoka kwenye mishughuliko kuja home. Akizoea atakuwa anategemea simu zako then utaona anakuwa karibu na simu muda mwingi.
 
Mwanamke asiepokea simu kwa wakati ni mwepesi sana ku deal nae.

Asubuhi ukiwa unatoka, tafuta sababu yoyote ile usimuachie hela ya matumizi, mwambie hata kuna mtu atakupigia simu akuletee, au unaeza kumwambia nitakupigia baadae nikuelekeze sehemu ukachukue.

Ikifika mida mpigie, piga mara moja tu, asipopokea usipige tena, sasa yeye ukifika muda wa uhitaji wake ataanza kukupigia, akipiga usipokee.

Kama anajuana na watu wengine ofisini kwako atawapigia, akipiga mjibu easy tu kama anavyokujibu yeye, nilisahau simu kwenye draw ofisini.

Kama hana contact za ofisini kwako, mkaushie mpaka kama saa kumi jioni hivi.

Hapa kama hujaacha hela ya kula utakua umemnyoosha vizuri, usihofu kuhusu watu wengine kwenye familia kushinda njaa, kwenye kuitaka heshima nyumbani kwako lazima waumie wanaohusika na wasiohusika.

Saa kumi flani ndio unampigia, unamwambia simu uliisahau kwenye kabati la ofisini.

Ukimchezea michezo hii mara tatu mara nne fulani, ataanza kukaa karibu na simu, maana ukimuahidi chochote, mida ikifika ni simu moja tu, asipopokea wewe ni mikausho.

Kuna time itafika, hata ukibeep kidogo mwenyewe anapiga fastaaaa.

Jifunze kutumia power uliyokua nayo kurahisisha mambo madogo kama hayo
 
Wewe una akili sana
 
Akiweka pesa ya matumizi hovyo, ukiikuta hiyo hela pita nayo, akikupigia kukuuliza kama umeiona mwambie ndio nimeichukua, nilikua na shida nayo nimeitumia.

Mwambie nitakutumia baadae, hiyo baadae ndo iwe baadae akipiga hupokei mpaka jioniiii, siku nzima akishinda njaa akili inakaa sawa.
 
Sasa unatuta mtu kavaa nguo haina mfuko anaanza vipi kuwa na simu kila mahali,.

Ila shukuru Mungu hana heka heka huyo za simu. Kuna wanawake masaa yote ni yeye na simu simu na yeye ni kuchat tu. Anapika huku anachat, anafua huku anachat nk.
Au anaficha maana mchepuko unaweza piga jaamaa yupo karibu
 
Yani hii ni wote mm natumia sana simu lkn kusahau kupo pale nishaaahau sokoni Zaid ya mara mbili unaweza weka ndani na ukaanza kutafuta😃
 
Nadhani wanawake wengi tuko hivyo,mi kwakweli nikiwa nyumbani nakuwa bize sana kiasi kwamba habari za simu nakuwa sina.Mmewangu alianza kulalamika ila badae naona alizoea tu japo kuna mda najitahidi kupokea au kama niko bize bize namjulisha kwa sms.
Majukumu ya kulea yanapoteza sana mda
 
Sasa unatuta mtu kavaa nguo haina mfuko anaanza vipi kuwa na simu kila mahali,.

Ila shukuru Mungu hana heka heka huyo za simu. Kuna wanawake masaa yote ni yeye na simu simu na yeye ni kuchat tu. Anapika huku anachat, anafua huku anachat nk.
Niliwahi kuwa na house girl wa hivyo akanishinda,maana hata ukitoa maelekezo hasikii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…