Hivi hili suala la kuhudumia ni la mwanaume tu au hata mwanamke wanapokuwa kwenye mahusiano au ndoa?

Hivi hili suala la kuhudumia ni la mwanaume tu au hata mwanamke wanapokuwa kwenye mahusiano au ndoa?

Wanaume wanaume wanaume wa sikuhizi ni janga kubwa mno.
 
hili suala la kuhudumiwa kwa wanawake naona limekuwa sheria kwenye mahusiano au ndoa japo kuhudumia sio jambo baya lakini naona sasa limekuwa sheria.

yani unakuta hata kwa wale wenye kazi zao bado wanataka kuhudumiwa kwa hela za mwanaume kwenye kila kitu pekeyake hata kama mshahara ni sawa.

sasa hili suala naona kama ni ubinafsi, uchoyo na uvivu wa wanawake halina msingi kwenye mahusiano wala ndoa lazima kuwe kuna kuhudumiana hii ndio maana halisi ya kupendana na sio mwanamke ahudumiwe peke yake tu hata kama mshahara sawa hii sio sawa.

kwenye hili andiko langu simaanishi mwanamke asihudumiwe hapana ila lazima kuwe na usawa mfano pale mwanamke hela anayo na hana cha kuifanyia lakini anataka hela ya mwanaume katika mazingira kama haya huyo mwanamke hastaili kuhudumiwa lakini linapotokea suala la dharura na kwamba mwanamke hana kitu ndio asaidiwe lakini kumuhudumia mwanamke kitu ambacho anacho ni ubinafsi na uchoyo wake anaokuonesha.

Lakini pia vile vile kwa mwanaume anapaswa kusaidiwa na kuhudumiwa pale anapokosa yani mnapaswa kuhudumiana kwenye mahusiano na ndoa huu ndio upendo.
Mwanamke anatakiwa kuwa chini yako na kama unakubali mwanamke awe chini yako kubali kuhudumia haijalishi
ana hela zake au vipi.Kuna mwanaume kukwama hapo ndipo usaidizi wa mwanamke upatikane mbali na hapo apende yeye kutoa ila haitakiwi kulazimisha wala kumtegemea.
 
wewe upo chini ya wajumbe za mitaa na wajumbe hawakupi hela ya kula, wewe upo chini ya serikali lakini serikali haikupi hela ya kusuka,

Unaposema kuwa chini ya ndio kuwa ufanyi msaada wowote kwa mwanaume wako hata akiumwa humsaidii kwasababu upo chini yake hivi unajua unachokiongea lakini ?

Tunataka jamii ya ushirikiano na kusaidiana ndio dhumuni ya andiko langu!
 
Uchoyo labda kama hajakupenda , hajavutiwa na wewe ..
Zamani nlikuwa najua wadada ni wachoyo wa kutoa papuchi, wadada wengi wa sahivi uchoyo wao hauishii kwenye kutoa papuchi tu

Wadada wengi sahivi ni wachoyo wa msosi, tena msosi ni mkubwa, bites k.v kipande cha andazi tu, mtu anakunyima..na hujawahi mtongoza

Sijui Wana makungwi wao wa mtandaoni wanawafundisha kua inatakiwa wawanyime wanaume vitu , ata sielewi 😁😁🤣 Zesh Anastasia21 Mallerina Light saber To yeye
 
Mbona tulishakubaliana humu “Mwanamke Hana cha kuofa kwa mwanaume zaidi ya mbususu” kwanini mnapenda kurudisha topic za nyuma?? Muwe mnahudhuria vikao vya majumuisho humu 😹😹😹
 
wewe upo chini ya wajumbe za mitaa na wajumbe hawakupi hela ya kula, wewe upo chini ya serikali lakini serikali haikupi hela ya kusuka,

Unaposema kuwa chini ya ndio kuwa ufanyi msaada wowote kwa mwanaume wako hata akiumwa humsaidii kwasababu upo chini yake hivi unajua unachokiongea lakini ?

Tunataka jamii ya ushirikiano na kusaidiana ndio dhumuni ya andiko langu!
Mimi nimeongea kwamba ikitokea hataweza mke anawajibika kusaidia kuumwa ni pamoja na kutokuweza huko halafu mwanamke atakuheshimu na kukutii wewe ukiwa kama kichwa unayejua majukumu yako huwezi kutegemea ushirikiano kama mnachangia sijui 50/50
 
IUnapaswa kuwasaidia wote hata mchumba huu ndio upendo lakini lazima kuwe na usawa sio huyu chakula anacho alafu bado anamezea mate chakula chako huu ni ubinafsi kabisa.
Ubinafsi ni pale ambapo wote wewe na mke au mchumba wako mnatoka kazini mmechoka, ila mkirudi nyumbani unataka mke ndio aingie jikoni na afanye majukumu ya nyumbani huku wewe ukinyoosha miguu sebuleni, na ubinafsi mwingine ni huu wa kutaka wote msaidiane na mhudumiane ila mwanamke bado akutii na akuheshimu na wewe umtawale
 
Back
Top Bottom