lipo neno la maana sana umelisema kwenye maelezo yako linaitwa UTASHI.
utashi ni neema ya kipekee sana Mungu amemkirimia mwanadamu. Lakini kila moja wetu pia amepewa kipawa au karama ya kufanya mambo mbalimbali kwa manufaa yake na wengine.
Taratibu za Ibada na Misa kwenye haya tunayoyaita mahekalu ya Mungu ni kwa utashi wa kibinadamu yako hivyo yalivyo. Na mambo mengi ni Imaginary tu, mengine ni sahihi na mengine sio sahihi kiroho na kimwili. Na utatafuta kwa biblia but hutakuta huo utaratibu wa mavazi wala mpangilio wa Ibada inavyopaswa kua, eti kuna sehemu ya kupiga magoti, ingine kuinamisha vichwa, kusimama au kufumba macho..
Zaid sana,
katika agano la kale, ukikamatwa umeiba unakwatwa mkono au ikithibitika umefanya uzinzi unapigwa mawe hadi kufa.
Lakini kwa matashi makubwa ya kiMungu agano jipya limehuisha mambo yote na sheria kali na kuyatakatifuza kwa msamaha na hukumu nyingine za haki.
Pete ni Ishara ya upendo na utakatifu kama Ulivyo msalaba Mtakatifu.
Ni muhimu kuheshimu na kuitunza katika matashi mema na Mungu atakubariki sana,
Aimen 🙏