Hivi huyu msemaji wa Yanga anadhani Rais Samia hajielewi?

Hivi huyu msemaji wa Yanga anadhani Rais Samia hajielewi?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Mimi ni shabiki wa Yanga (kiasi) ila kitendo cha huyu msemaji wa Yanga kutaka Jumatano kazi ndani ya ofisi za umma kuishia saa sita mchana siku ya Jumatano kwakuwa Yanga inacheza HAPANA.

Hata ingekuwa ni final bado hatupaswi kusitisha shughuli za umma kwa vitu vyenye tija kwa wachache huku maelfu na maelfu ya Watanzania wakikosa huduma muhimu kwenye ofisi za umma. Yeye anastawi kwa kuhamasisha mashabiki, na awapo uwanjani na maelfu ya washangiliaji hapo yupo kazini huku account ikipanda graph.

Rais Samia kataa hili ombi batili.

Huyu dogo ni jinga sana siku hizi hata waliomtuma wanafikiria kwa kutumia kalio...!
 
Nxhi ngapi zikichukua ubingwa au wakiwa live fainali wanapumzika.

Punguza userious na kasiriko aisee.

Mwagilia moyo na Yanga Afruca
Mara nyingi huwa ni timu za taifa lakini sio vilabu. Hauwezi kufanya jambo kama hilo kwa klabu fulani kwasababu
1) utaonekana una mahaba pekee juu ya hiyo klabu
2) unaowasitishia shughuli zao ni watu waliochanganyika katika upenzi wa vilabu sio wote ni Yanga bali kuna wa Azam, Simba, n.k hivyo halina tija kwao kuwasitishia mambo yao ya kiuchumi.
 
Na wengine hata mpira hawaujui
 
Yanga ni taasisi ndogo sana ya michezo kuliko BMT. Kama BMTwenyewe hawajataka watanzania kufanya hivyo, msemaji wa yanga anapata wapi jeuri ya kusema hivyo?
 
I think as much.
Kama wangekua serious, nadhani wange lodge ombi lao kwa rais kupitia channels za kiserikali (TFF-BMT-Wizara ya michezo). I think alikua anafurahisha genge tu, for the sake ya vibe na mzuka..!!
Yah sure...
 
Back
Top Bottom