Kuna kipindi funguo la geti letu ilisumbua,inasemekana hata vibaka walieeza kulifungua kwa kutumia vijiti!! Basi baba akamsimulia rafiki yake tolu wakiwa kilabuni,saa hiyi baba amelewa chakari,ila tolu alikuwa timamu kabisa,si unajua tolu huwa anachanganya maji mengi kwenye gongo ili aobekane kama anakunywa sana? Cha ajabu halewi,sasa si ndiyo tolu akamwahidi baba kumpa wachonga funguo mahiri kutoka mtaani kwake ili wamchongee funguo ya "maana"!baadaye baba aliporudi nyumbani na kutueleza adhma yake hiyo ya kuwapa mafundi wa tolu kazi ya kutuchongea fungup la geti mjomba alikuwepo,na akamkazia baba macho na kumwambia asithubutu kuwapa kazi hiyo mafundi wa Tolu,basi tolu AKAJA kesho yake akiwa na mafundi wake!! Baba akawatimua mafundi ila akamwambia tolu asiondoke kwanza hadi waongee,hapo ndiyo baba akamchana tolu kuwa hawaitaji mafundi wake,maana wale mafundi huwa wanapewa maagizo ya kuchonga funguo mbili,moja wanampa Tolu na nyingine wanampa mteja,so tolu akitaka kuingia kwetu muda wowote anachukua tu ile funguo ya pili na kuzama ndani!! Baba akakumbuka stori aliyopigiwa kilabuni jinsi jirani yake Papaa anavyoteseka kwa kuibiwa vijiko kila mara,tena siku nyingine anawakuta kabisa waizi wa vijiko wakiwa ndani,wakiulizwa mnataka nini ndani kwangu wanasema "hata sisi tulizaliwa hapa,ila tulitoka kidogo na sasa tumeamua kurejea" basi baba akaamua kumpiga ban tolu mazima!! Hata tolu akimsalimia yeye akawa anakaushia kikamanda,mwisho tolu aka maindi na kuamua kufanya yake,maana alijua kabisa kuwa baba ataenda mbele na kumshtua hata papaa kuhusu mwizi wa vijiko vyake!! Basi ndiyo ikawa hivyo!! Binamu ameshamwonya Mama asijipitishe pitishe kwa tolu,naamini mama atazingatia hilo, sasa hivi tunafurahia ulanzi wetu bila bugudha,tolu anatumaindi kiaina ila anawaza kama baba alimshtua mama kuhusu ilw ishu,kwa hiyo ametulia tu,ila tuombe Mungu tusiishiww chumvi na mama aende kuomba kwa tolu!! Maana hilo ndilo analosubiri Tolu! Ngoja nimalizie tumbaku yangu.