Hivi inakuwaje mzazi anakua tegemezi Kwa mtoto ambaye amejitafuta Kwa jasho lake bila kumrithisha hata mbuzi mmoja

Hivi inakuwaje mzazi anakua tegemezi Kwa mtoto ambaye amejitafuta Kwa jasho lake bila kumrithisha hata mbuzi mmoja

Embu msituletee umagharibi hapa; mama yako kakuzaa kwa uchungu na baba yako alijikaza asihonge malaya au kunywea hela zote ili akulee , ulijinyea na wakawa wanapambana na kinyesi chako, ulikuwa unalia usiku mzima na wakakuvumilia na asubuhi na usingizi wote walitoka kwenda kupambana kwa niaba yako

Leo hii kisa na wewe unaweza zaa au kuzalisha unajiona umeshuka toka mbinguni kwa nguvu za roho mtakatifu

Kwa utamaduni wetu utaonekana ni mtu wa ajabu sana ukisema utoe haya mawazo uliyoyaandika kwenye huu uzi mbele ya hadhira
 
Huwa nashangaa unakuta mzazi anakua tegemezi Kwa kijana ambae amejitafuta Kwa jasho na damu amejipata mzazi anakua analandalanda kumnyonya huyu kijana Kwa lengo kwamba amemzaa kwani huyu mzazi yeye alizaa Ili amfanye mtoto punda yaani kiasi kwamba mtoto asipomsaidia mzazi anatangaza kutoa laana wakati na yeye alikua kijana kwahiyo anampa mzigo huyu mtoto baada ya kupambania familia yake anaanza kulea mzazi asiejielewa aisee mtu mweusi akili hana kabisa huu ni udiktekta mambo leo Kwa watoto ukweli usemwe nyie wazee msipende Ganda la ndizi
wazazi wawili wanaweza kulea watoto 8 ila watoto nane wakashindwa kuwalea wazazi wawili.
 
Hao watu ambao Mimi niwasaidie ni vilema au maana sijaja nao duniani nikurupuke tu kusaidia mtu ambae sio kilema na hata kilema ni kazi ya serikali kusaidia sababu tunatoa kodi
Omba Mungu akuweke kwenye position ya kutoa msaada
Asikuweke kwenye position ya kushitaki msaada
We saidia kama una uweZo, Mungu atakubariki zaidi
 
Back
Top Bottom